hii sio sawa, anatibiwa kama nani..

gharama za wagonjwa wengine hapo muhimbili wasio na mbele wala nyuma nazo Serikali itazibeba? tuwe serious kidogo.
Kwa hiyo akiachwa ndio hao wengine watatibiwa.
Acheni kujenga Taifa la watu wenye roho mbaya. Mnaeneza chuki lakini hazitawaacha salama.
Serikali imefanya jambo jema sana.

Kumbe Kuna watu wenye roho mbaya wengi sana kwenye nchi hii. Nilikua siamini ili ni wazi kuwa watanzania Kwa Sasa ni Taifa lenye watu wenye roho mbaya sana.
 
Jay anapaswa kusaidiwa ikiwa kakwama, Ila wanachohoji hao pia kina mantiki kwa maana Kuna maelfu ya watu ambao wamekufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Kusema tusubiri apone ndio raisi aambiwe, nadhani huu ni ujinga.
Ina maana raisi hajui watanzania wengi hawawezi kumudu matibabu?
 
Michango isitishwe sasa
Maana kwenye vimedia uchwara
Naona watangazaji washaanza...
Kuwaomba watu watoe hela

Ova
Hivyo unavyoviita vimedia uchwara ndivyo vilivyosikika hadi Ummy katoa neno.Vimedia uchwara vinatufaa cc wanyonge kwani havibagui
 
Neno roho mbaya limekaa karibu sana mdomoni mwako.
Hao hawamchukii Prof j
Malalamiko ya wananchi wengi kushindwa matibabu yapo miaka nenda rudi, ndio maana unaona hadi kina malisa wanaanzisha challenge za kusaidia hao watu japo bado kwa kiasi kikubwa wengi wanashindwa kufikiwa.
Serikali inapaswa initathmini kuwa wale wananchi wengi ambao hawana vipato watasaidiwaje kupata matibabu
 
Hiyo sio nongwa. Tatizo sio yeye kusaidiwa. Asaidiwe privately.

Ni discrimination kutumia pesa ya umma kumsaidia mtu mmoja ilhali watu wengine walio katika situation kama yake wakiachwa kujipigania wenyewe!
What difference does it make 🤷 ni wivu tu mtakuja kumchawia hata age basi ili mfurahi.
 
Waziri aanze sasa kupitia mahospitali kuangalia wote wasio na uwezo ili serikali igharamie matibabu....
Unataka tuamini kuwa alipotembelea Muhimbili wagonjwa wengine walikuwa wameruhusiwa kwenda nyumbani akamkuta Prof peke yake?
 
Watanzania tubadilike, wewe na hao ndugu mliowataja kila siku mnayapigania maisha yenu wenyewe tena wengine hata maisha ya ndugu wa tumbo moja hamna muda nayo.. yeye katika kupigania maisha yake pia aliwekeza kwenye jamii kwa kuwagusa watu mbalimbali hasa kwa kutumia kipaji chake, muache avune alichopanda na wewe kwa nafasi yako gusa maisha ya watu na wewe watu wataguswa na maisha yako acha nongwa. Hapo chini kuhusu bima umenena vyema ila sio kubeza kusaidiwa kwake kwani wasanii wangapi wanaumwa kwa nini Profesor J.. Kila mtu atavuna alichopanda.
 
Ule usemi wa aliyenacho huongezewa na asiye nacho hata kile kidogo alichonacho hunyang'anywa ndio unatimia kwenye mazingira haya.
 
another wasted sperm,
kwani serikali haijui kuna hao 'wengine' wakikata roho kila kukicha hapo hapo Muhimbili (na kwengineko) huku wakikosa hata 10k ya matibabu ?
Huduma za afya bongo ghali sana walala hoi wengi wanateseka mm ndugu yangu amefanyiwa operation ya kichwa hapo Moi lakini ameshindwa kupata uchunguzi zaidi na huduma nyingine baada ya kutoka ICU sababu bado ana deni ikapelekea arudi tu tujikusanye aende tena . Na tulikutana na mwamba mmoja hana kitu katoa pesa na anadaiwa mgonjwa bado hajapona jamaa akafikia uamuzi amtelekeze mgonjwa asepe maana hana hata mia ya kuanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…