Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa amesema uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.

Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100.

Wale wapotoshaji wa miaka 100 mara Mkataba wa Milele waje tena na jipya.
 
Unahukumu kitu ambacho akijatokea kwa chuki zako binasfi kwani wewe ulikuwa unataka nini haswa?
Hili deal liliwekwa Kwa kificha hapo mwanzo.Kelele zisingepigwa ilikuwa Tanganyika inakwenda kuliwa.Kelele zimesaidia haya mambo kuwekwa wazi nakurekebishwa faster vipengele vyenye utata.Bigup TEC,CDM,Wanaharakati(Dr.Slaa,Mwabulusi,Mdude,Sifa na mchungaji aliyefungwa)🤔
 
Ila kwa maoni yangu kumoa forum Huyo mjomba ni matumizi mabaya ya muda. Analeta uhamasishaji sehemu ambayo haiihitajiki. Watu washasaini.
Waafrika hatujali muda, ndio maana hadi leo ni zaidi ya miaka 60 ya uhuru lakini hatuwezi kuendesha bandari yetu wenyewe.
 
Huo mkataba wa miaka 30 kutoka milele naomba tuuone kabisa! Sasa kama ni kweli inabidi wana CCM wawaombe radhi watanzania waliokuwa wanapinga bandari kuuzwa milele …..
Ni wazi Samia kabadili gia angani
 
Pesa yq DP ndiyo italipa walimu mara kumi ya hiyo.
Pesa ya Gesi ya Mtwara imetumiwa wapi?
Pesa ya Mgodi GGM imetumiwa wapi?
Fedha ya Tanzanite umeiona wapi?
Deni la Trilioni zaidi ya 60 kwa miaka 2.5 imetoka wapi kama tuna fedha?
Fedha zaTANAPA zimekwenda au zinatumika wapi?
Am very sorry to say that, some youth are using their "tool to sit" in other words 'bataks" to think and reason.
 
Naangali hapa hafla la utiaji saini mkataba wa Bandari,

Kuna mzungu anamwelekeza mwarabu nini Cha kufanya,

Na aliposaini mahala pake, anakataa kwenda kupata picha ya pamoja.

Sasa naelewa, nyuma ya Mwarabu wa DP World yupo mkoloni wetu.

HAKIKA, kumbe Mwarabu ni kibaraka wa mzungu.

Bado Tutaona mengi.
Hii tangu mwanzo ndivyo ilivyo Mwarabu anatumika tu wakoloni wamemtumia mwarabu kupitia dini yake.
 
Back
Top Bottom