Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Kwa hiyo tumekubaliana wote mikataba mahsusi ya bandari isaniwe! Inasainiwa kibabe tu au tayari inaeleweka muda wake wa mwisho?
 
Pesa ya Gesi ya Mtwara imetumiwa wapi?
Pesa ya Mgodi GGM imetumiwa wapi?
Fedha ya Tanzanite umeiona wapi?
Deni la Trilioni zaidi ya 60 kwa miaka 2.5 imetoka wapi kama tuna fedha?
Fedha zaTANAPA zimekwenda au zinatumika wapi?
Am very sorry to say that, some youth are using their "tool to sit" in other words 'bataks" to think and reason.
Wewe ulitakeje kuhusu Bandari?
 
Wewe shida hata usikilizi kinacho ongelewa hapo na ni wazi mkataba umefanyiwa marekebisho na mkuu wa bandari kasema wazi maoni ya wananchi yamezingatiwa …au wewe usikilizi?
Pata nakala kwanza ya kilichosainiwa Leo, ujiridhishe. yawezekana Ritz yupo sahihi.
 
Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa.

Naona maoni mengi ya kina Mwabukusi & co yamezingatiwa kwa kiasi fulani...
 
Naangali hapa hafla la utiaji saini mkataba wa Bandari,

Kuna mzungu anamwelekeza mwarabu nini Cha kufanya,

Na aliposaini mahala pake, anakataa kwenda kupata picha ya pamoja.

Sasa naelewa, nyuma ya Mwarabu wa DP World yupo mkoloni wetu.

HAKIKA, kumbe Mwarabu ni kibaraka wa mzungu.

Bado Tutaona mengi.
Kwa andiko hili kuanzia leo na ku ignore kumbe wewe ni mjinga kiasi hiki? Sikutegemea kabisa kuwa unaweza kuwa na mawazo kama haya kichwani kwako.
 
TEC nawaona na vibandiko vyao vya pinki.

Umewashuka.
Haya mambo kwako mama ni mazito ni sawa na kumpiga chuma jiwe. TEC hawawezi kuudhuria kama vile vifungu walivyovikataa havijafanyiwa marekebisho, hiyo ni sawa na kujipaka kinyesi. Hapo vipengere vimesharekebishwa na wameviona jinsi vilivyorekebishwa na ndio maana wamehudhuria. TEC noma.
 
Pata nakala kwanza ya kilichosainiwa Leo, ujiridhishe. yawezekana Ritz yupo sahihi.
Mimi namsikiliza mkurugenzi wa TPA na tunaamini anachokisema ni kweli kuwa wamesikiliza maoni ya watu ..sasa ni miaka 30 sio mia au milele…lakini bado tutakuwa na shauku ya kuona hayo marekebisho!

Kwenye hili TEC,Chadema,Slaa,Mdude na Mwambukusi wanastahili kupongezwa sana
 
Bado TEC+MWABUKUSI , SILAA, wanaendelea kua Mashujaa wa Taifa hili.

Hili limethibitishwa na Makamo wa Rais, kukiri ya kwamba, wamesikiliza maoni ya Watanzania, na hatimaye wamekuja na Mikataba hii!!.


Mwabukusi Oyeeee
Nikweli maoni yetu serikali imeyasikia na watanzania wote. Hii ni serikali sikivu tufanye maendeleo sasa watanzania.
 
Back
Top Bottom