Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Rais hajashauriwa na wenye elimu tu, kwa mkataba kama ule hata wasio na elimu waliona wazi kuwa tunapeleka nchi shimoni. tungekuuliza wewe sana ambaye unaumia kwanini vipengele vinavyowapendelea waarabu vimeondolewa. imeisha hiyo.
Km unaamini asie na elmu anaweza kumshauri Rais basi ndio ujue umuhimu wa kuacha pombe za moshi.
Utadhurika kabla ya siku zako.
Acha gongo dogo
 
Simba keshokutwa kama DP World Dar.
Meli 400 za DP World kuja moja kwa moja bandari ya Dar.
zikija tutashukuru, hata mimi magari nitakuwa naagiza uarabuni sasa kwa bei ndogo kabisa na yanafika kwa uwepesi kwasababu wao ndio wanaendesha. ila sio kwa mkataba ule mliokuwa mnataka kututumbukiza shimoni., na tusingestuka ninyi mlishakubali kuuza nchi. nje ya mkataba ule, yaani sasaivi, hata wangewapa DSM port yote mi sina shida.
 
Km unaamini asie na elmu anaweza kumshauri Rais basi ndio ujue umuhimu wa kuacha pombe za moshi.
Utadhurika kabla ya siku zako.
Acha gongo dogo
wananchi hadi darasa la saba wamepiga kelele, na Rais amesema amezingatia maoni ya kila mtu aliyesema. hao kina mdude hawana hata elimu ya chuo, ila wana akili kuliko wewe. though najua kwa hakika hata wewe mimi nimekuzidi elimu. ila sina majivuno ya elimu kama wewe.
 
Kuna mambo mawili serikali ya samia inachanganya kulazimisha mkataba mbaya kati ya tanzania na dubai kuhusu bandari. Ule mkataba na dubai wa kibeberu kuhusu wao kupewa hati miliki miradi ya kujenga na kuendesha bandari zetu zote umekataliwa na wananchi. Kwanza mkataba ulikua kinyume na sheria ndio maana wakataka kubadili sheria jambo halikufanyika. Sasa kupewa DPWorld kuendesha bandari hatuna uhakika ni chini ya huo mkata au ni kwa msingi wa kandarasi iliyotangazwa na bandari. Ingefaa jambo hili liwekwe wazi na kama hakuna mahusiano masharti ya DP kupewa kuendesha bandari ya dar es Salaam yawekwe wazi kwa wananchi kuona.
Sababu ya hawa wahuni kulazimisha uwekezaji wa DP world hazina wala uzito ila kuonesha uzembe mtupu na kutowajibika kwa viongozi. Wanatoa mfano wa ufanisi wa mombasa bandari shindani na dar es Salaam ila jambo hawasemi mombasa haina uwekezaji wa nje bali inaendeshwa na shirika la bandari la kenya KPA.
 
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/N6izYMjIOaI?si=O_YQZdZcwAOJWWpD

MKURUGENZI MKUU WA TPA, PLASDUCE MKELI MBOSSA

Uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.

Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100. Watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kampuni ya DPW.

Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Rais Samia amesema haikuwa rahisi kufikia makubaliano haya lakini walisikiliza na kufuatilia maoni na hoja za kila mtu hivyo hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa ambao Serikali iliunda jopo la wataalam kufuatilia maoni hayo.

Kwa ujumla na kipekee kabisa, Rais Samia ameshukuru watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.

Amewakaribisha watu wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania ili kuinua uchumi na kupunguza umaskini wa watu.

Mawazo ya wawekezaji wa ndani kupewa bandari ni mazuri na ya kizalendo lakini yapo mbali na uhalisia. Katika kusiani mkataba huu, maslahi mapana ya nchi yamezingatia maslahi mapana ya nchi.

Bado kuna vitu havipo wazi wanawekeza vitu vya thamani Gani ??
Na wakodisha Kwa $ ngapi Kwa Mwaka kwa hiyo miaka 30 tunategemea kupata Kiasi Gani , na hiyo kupitia utendaji wao WA miaka 5 tusiporidhika , tukavunja mkataba nini madhara kwetu na pia kwao Kwa kushindwa kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba.
Huu mkataba naufananisha na Ile hadithi ya naomba niweke shingo Tu kitandani mwishowe ni kusukumizwa kabisa.
 
Safi sana.

Asante Yesu nchi yetu sasa imejifunza kuweka siasa za uzandiki pembeni na kuanza kufanya mambo ya msingi kwa maendeleo ya kweli

Kazi iendelee
Nakubaliana na raisi SSH kuwa wananchi wamekuwa na mchango mkubwa kwa kufikia makubaliano. Isingekuwa hivyo, tusingepata mkataba huo. Kwa hiyo washukuriwe wote walioshiriki kukosoa MOU ambayo iliandikwa na kutiwa sahihi kiovyo kabisa!
 
Back
Top Bottom