Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Wangerekebisha kanisa lingetwambia, kwa kuwa kanisa halijatuambia basi serikali imepuuza wananchi, kanisa, na watalaamu wote waliopinga mkataba huu.
 
maaskofu walishapewa mwaliko na walijua wanaenda kwenye utiaji saini, hivyo it wasn't a surprise to them. na kama hujaelewa, kuna vipengele vingi tu vimebadilika, usije kuwa unapiga domo hapa ukifikiri hawajasikilizwa au upo kama vile awali, hujajua. Samia kasikiliza wananchi na kabaidlisha, walimwingiza king mama na walikuwa wanataka aharibikiwe ili apate shida kwenye uchaguzi 2025, amestuka na kawabwaga huko.
Si ni nyie mlisema IGA ndo mkataba mama HGA haiwezi kwenda kinyume na IGA? Mmebadili gea angani tena.
 
Si ni nyie mlisema IGA ndo mkataba mama HGA haiwezi kwenda kinyume na IGA? Mmebadili gea angani tena.
HGA na IGA ni vitu tofauti haviingiliani kabisa.

Mfano wa HGA ni kama vile wewe aje mgeni iwenu halafu umpe kanuni za hapo kwenu mfano umwambie, hapa ukienda matembezi kurudi mwisho saa tatu usiku, mlango unafungwa, wanafunguliwa mbwa wa ulinzi, hatoki mtu kukufungulia baada ya saa tatu usiku.

mgeni akikubaliana na masharti hayo halafu akichelewa kurudi aking'atwa na mbwa hakuna wa kumlaumu.

Huo ndiyo mfano wa HGA kwa mlioenda shule kusomea ujinga.
 
Dangote alivyoanza oparesheni simenti alikua anauza elfu 7 kwa mfuko, hiyo ilikuwa ni Dar mwaka 2016, ila makampuni yaliyokuwepo tayari yakashinikiza kuwa bei ipande na kuwa elfu 11 kama wanavyouza wao, ikabidi Dangote afuate nyayo zao.
Mwenyekiti wa kampuni ya Taifa Group, Rostam Aziz amekutana na Rais wa Zambia, Haikande Hichilema na kufikia makubaliano ya kuwekeza katika kuzalisha jmeme wa kutumia gesi nchini humo.

Rostam alikutana na Rais huyo katika Ikulu ya Lusaka Zambia jana Ijumaa akiwa ameandamana na… twitter.com/i/web/status/1…
 
namshukuru kwamba amerekebisha vipengele, amesiikiliza ushauri na sauti ya watanzania. lakini, sioni kama ana strength za kutosha, kwanza ilikuweje akataka kuiiingiza nchi kwenye msala wa mkataba kama ule bila kugundua, manake washauri wake hana na sijaona kama amewachukulia hatua. hapo hatuwezi kusema ni strong. ingekuwa nchi za wenzetu alikuwa anatakiwa ajiuzulu mara moja kwasababu udhaifu wake umeonekana waziwazi na hana hata cha kujivunia kwenye mkataba huo, asije kuja kusema yeye ndiye alisaidia uwekezaji, watanzania ndio wamesaidia, yeye alikuwa anatupeleka shimoni kina mwabukusi wakatukomboa kwa msaada wa Mungu.
Hakuna mkataba uliosainiwa kabla ya huu.
 
kichwa chako kimejaa kamasi. kama tusingesema nchi ilikuwa inaingia shimoni. hata Mh. Rais amekubaliana na sisi akaondoa vipengele vyote tata tulivyotaka viondoke, lakini wewe kwasababu ya dini ulikuwa radhi nchi itumbukie as long as mabwana zako waarabu watafaidi.
Sasa kama kila kitu kimerekebishwa mdude kwanini anaendelea kusema maandamano ya kupinga kuuzwa bandari yapo palepale tarehe 9 November? Huyu mdude ni kichaa?
 
Tunashukuru kupata za ndani haya DP-WORLD waingie kazini tuchape kazi. Mama samia anaupiga mwingi sana 2025 - 2030
 
Sio kweli kwani mkataba uliosainiwa leo ni kati ya TPA na DPW usichanganye makubaliano na mkataba
 
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
Wameshushuka shuuu, wanajitowa kimasomaso tu.

Wamechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Leo yalikuwa yamenuna kweli.
 
Back
Top Bottom