Watu hawatoacha kujichukulia sheria mikononi endapo uonevu huu utaendelea,eti paki gari pale Mimi sipaki nalizima nakaa hapo hapo.

huwezi kuja kusimama mbele yangu wakati naendesha halafu ushuke uniambie paki pale na manguo yako ya kiraia.

kisa tu umenyoa una kipara ndio nijiongeze au kisa umevaa kaunda suti ndio nijiongeze,yani nisingeweka gari pembeni na hapo hapo ningezima gari,mpaka nione traffic ndio ningetoa gari kuweka pembeni.

Hii nchi sio ya usalama wa TAIFA kama kaona sawa kuchomeka mbele yangu na kusimamisha gari ndio staili mpya ya kusimamishana hapo sawa. Lakini dogo kuwekwa pembeni na kukubali na raia asie na uniform n uzembe na uoga na kutojiamini.
 
Hao ndio wale waliokuwa wanatumiwa na Magufuli kufanya uharamia maeneo mbalimbali nchini.
 
Hawana Shughuli za kufanya baada ya mwendazake kuondoka.kazi iliyokuwepo ni kudeal na wapinzani.Samia hataki kusumbuana na wapinzani kwa hiyo utaona hawana kazi yoyote hivyo kukaa idols siku nzima.Ndio wanatafutiza kazi za kujishikiza ili kumshtua mama kuwa nao wapo kazini.
 
Afrika tunayo nidhamu ya kutishana na kuitiana woga. Picha za aerial view mfano google maps ni hatarishi kiusalama zaidi hizo picha za simu ya mkononi. Some security precautions are simply outdated.
 
Makosa yanaweza kutokea pande zote hao ndugu zetu katika medani ila hata huyo bwana na ist yake ni wale wale tu,pale aliposema mjomba wangu mbunge atanitoa nikaona baasi huyu ni aina ya wale watu wasumbufu hadi mtaani kisa tu anajuana na fulani kisa tu yeye fulani kisa tu ana watu fulani ikumbukwe kuna wakati mpaka uwapate hao watu wa kukusaidia ushachakaa vibaya mno huyo bwana ist nae wale wale
 
Nafikiri kuna zaidi ya hii story. Kama amechomekewa tu sioni kwa nini asimamishwe tena inawezekana baada ya hapo kuna kilichotokea ambacho mjomba wa mbunge hakisemi.

Kama kuna kingine mjomba asingekuwa cool hivyo. Isitoshe kwa sauti hata maneno tu anaonekana ni dogo kweli kweli.

Hakujaribu kukimbia wala kukaidi. Tambua mnene yule alikuwa mbele muda mrefu na hata lane nyingine pia.

Ila jamaa zetu hawa si ajabu akashtakiwa kwa ugaidi na miamala ya simu ikapatikana.
 
Usibishe. Iliwahi kunitokea. Mi nimesimama kwenye taa nyekundu. Nasubiri ya kijani. Nyuma kuna roli liko kwenye mwendo. Dereva hana mpango wa kusimama. Alivyofika tu kwenye taa, zikabadilika zikawa kijani. Na mimi nikaondoa gari. Najua mimi ndio wa kwanza mbele kwa wale tuliokuwa kwenye mstari wa kusibiri taa za kijani. Alipopita taa, akabadili njia. Akatoka kushoto kwake akaja kwangu kulia, akanibana kabisa nikakosa njia. Nikasisima ghafla. Matairi ya nyuma ya roli lake yakanikosakosa by inches. Akaendelea kama vile hajafanya kitu chochote. Ningekuwa na bunduki na mimi siku hiyo ningeua mtu.
Uko sahihi.
Kwasababu anasema taa zimemruhusu, sasa zilimruhusu yeye mwenyewe??

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kwa mara nyingine,tuonyesheni umoja na mshikamano katka hili hata kama wengine halituhusu ila ifike MAHALI Jamii Forum iogopwe.

Tupaze sauti,Hili tukio lifike linapostahili kufika na wenye connection watuletee mrejesho,mimi kazi yangu nikutia NUKTA uzi upande hewani kila nitakapohisi umepooza.

Huna cha ku comment tia NUKTA uzi upae hewani hadi hao waliohusika hapo kila mtu apewe stahiki zake na iwe mwanzo na mwisho huu uonevu,Tukiamua wananchi sisi kwa sisi inawezekana.

Hamna cha katiba mpya hapa Maamuzi ni yetu wenyewe tuamueni TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…