Wanajeshi kwa waliohusika na tukio hili wawajibishwe
Kwani kuchomekewa ndio kugongwa.ni mambo ya kawaida tu ili mradi mungu ameepusha hamjagongana.bahati nzuri picha yake imeonekana haya wenye kujua sheria mumsaide kama inawezekana apaye haki yake.
 
Hii Tabia ya kuonea raia kisa tu ofisa wa usalama wa Taifa kakwaruzana na waendesha magari barabarani inatoka wapi?
Hii inaonyesha kuwa tuna Usalama wa Taifa incompentent, wasiojua kazi zao, ambao wanatumia nafasi zao kuonea watu.

Ni wapi katika majukumu ya usalama wa Taifa, Usalama wa Taifa unafanya kazi za Trafiki barabarani?

Leo hii ofisi na premise za usalama wa Taifa zinaenda kutumika kama parking ya kukamatia raia eti kisa raia kakwaruzana na ofisa mmoja huko barabarani ni ushamba wa hali ya juu na ni kuipaka Idara matope.

Tunataka Idara ya Usalama wa Taifa TISS imchukulie hatua za kinidhamu huyo ofisa anayeonekana kuleta kiburi kwa kutumia kazi yake kuonea watu.

Kibaya zaidi anaamrisha raia anyang'anywe simu yake bila search warrant au bila kufuata sheria za kipolisi, huu kama siyo ujambazi ni nini.

Huu utovu wa nidhamu ukomeshwe mara moja, hatutaki usalama wa Taifa unaoendeshwa kihuni.

View attachment 2182358
Jamaa mwenyewe pia ni walewale, akipata nafasi naye anaweza umiza watu. Mwishoni anasikika ati mjomba wake ni mbunge, atamtoa tu.
 
Kaka ninakupongeza kwa kuwa SMART na kurekodi. . .ijapokuwa sijapenda uliposema una mjomba wako MBUNGE. Kingune hilo jamaa na askari wenye uniform ni WAJINGA KWELI. Binafsi sio askari na sina mafunzo ya uaskari.....lakini kwa akili ya kawaida walijiweka ktk RISK .....maana jamaa wangekuwa na convoy ya waarifu wangeingia kiurahusi sana na kuleta madhara makubwa humo ndani
Salute mingi.....excellent!!!!!!
 
Rudi shule kasome vizuri uelewe tena ikibidi mpaka Kipara kikuote kichwani.

Sheria iko wazi kabisa kuwa muhimili mmoja haupaswi kuingilia muhimili mwingine kikazi.

Ndiyomaana unaona ofisa TRA hawezi kufanya kazi ya ofisa TBS, na Ofisa TPA hawezi kufanya kazi ya TAA.
TRA ,TBS, TPA, TAA nk sio mihimili ya nchi inayozungumziwa kwenye sheria. Hizo ni taasisi/mashirika ya umma.
Mihimili inayozungumziwa kwenye sheria ni
  • Serikali
  • Bunge
  • Mahakama
 
Zingatia umri na uzoefu wa dogo kimaisha ...
Yaah huenda chalii hajapitia ama alh kiumri si mtu mzima sana, hata sauti yake inadhihirisha hilo.

Ila hapo hakutakiwa kusubiri huyo jamaa ashuke angesepa zake ama lah yeye ndie ambae angeanza kushuka labla yake.

Jamaa katumia hiyo nafasi kujitetea yeye na kuaminiwa kabla dogo hajashuka akiami yupo kwenye haki na ana mashahidi.
 
Ukiangalia vizuri hiyo video utaona kabisa video imepigwa ndani inaonyesha mlinzi yuko wapi, kuna walinzi wangapi getini vitu ambavyo havionekani Google maps.
Kwan kipi kimemfata mwenzie mchukua video au eneo lililochukuliwa video?
Hiv kwan huyo alierekodi hio video alikuwa na nia ya kurekodi hilo eneo? Ama wao (hao wanamwambia chuchumaa) ndio wametengeneza mazingira ya eneo lao kurekodiwa
 
Kwanza una uhakika gani huyo mtu kaonewa?

Pili clip inaanza kuonesha akilalamika na kuamriwa kupaki gari yake, haioneshi chanzo cha iyo tafrani ni nini? Una uhakika gani kuwa huyo afisa ndo mwenye kosa?

Tatu tangu lini kuambiwa upaki gari kukawa kuonewa?

Nne kupiga picha kwenye eneo ambalo hairuhusiwi kupiga picha Au kuchukua video ni kosa!
Kosa kwa mujibu wa sheria gani? Tutajie kifungu
 
Yaah huenda chalii hajapitia ama alh kiumri si mtu mzima sana, hata sauti yake inadhihirisha hilo.

Ila hapo hakutakiwa kusubiri huyo jamaa ashuke angesepa zake ama lah yeye ndie ambae angeanza kushuka labla yake.

Jamaa katumia hiyo nafasi kujitetea yeye na kuaminiwa kabla dogo hajashuka akiami yupo kwenye haki na ana mashahidi.

Utoto wa dogo umemponza. Utakuta hata leseni hana.
 
Hayo mambo yanafanyika nchi zenye raia wengi wasiojielewa na wenye maisha ya bora liende, hewala hewala.
Kwenye nchi ambazo utawala wa sheria unafanya kazi sawa sawa polisi wa barabarani tu ndio wanahusika kutoa muongozo wa matumizi ya barabara wakati wa hali ya kawaida ya amani kwenye nchi.
Mfano nchi ipi?
 
Fikiria, kamtoa kwenye mataa (kwa kumfanya kijana amfuate nyuma) hadi hapo kwao, lengo ni nini..?? Probably "hujanijua Mimi ni nani, ngoja nikuonyeshe". Unaweza fikiria kidogo ni umbali gani kutoka walipoanza kutofautiana hadi hapo kwao, kwann hakumzuia huko...?? Acheni ulimbukeni, kila mmoja akiwa hivyo hatutafika
Nimesikiliza na kuangalia clip yote sijaona sehemu imetamkwa unajua Mimi nani?
 
Back
Top Bottom