Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Naomba kutoa ushauri kwa vijana na hizi smartphone zao, si kila kitu ni cha kushoot video au kupiga picha.
Hata Kama jamaa ingekuwa ni makosa yake lakini haikupaswa kuingiza gari humo alipotakiwa kuingiza gari! Kujipeleka mahali ambapo utakuwa huna utetezi wa aina yoyote ndio kosa la kiufundi alilofanya mshikaji.. kwani tunafahamu hulka za hao jamaa raia huwa wanatuchukulia kama watu tusio na haki na wenyewe ndio wenye mamlaka ya kufanya uwezavyo!.
Nini kama wangembambikia kesi nzito nayeye ameshajitia dosari ya kuingia chini ya utawala wao..?
Mwanaume upo kwenye mazingira yako unategemeaje nguvu ya mtu mwengine ambae yupo mbali ambapo mpaka aje afike chamoto utakuwa ushakiona! Ati mjomba wangu mbunge!..😂
Aliposimamishwa hiyo ndio ilikuwa nafasi yake ya kutoroka na sio kukubali kuingia kwenye mdomo wa mamba,ambae nae barabarani sio mahala pake!
Wito wangu.. hakuna aliejuu ya sheria hivyo watu wa usalama tumieni mamlaka yenu pale panapostahili,ubabe na majivuno sio kitu chenye afya pale ambapo hapastahili...
Mamlaka zinazohusika zinapaswa ziingilie kati na ziwawajibishe kila mmoja kwa haki ili kudhihirisha hakuna aliejuu ya sheria,pia kila mtu lazima awe na utambuzi binafsi katika nafasi aliyonayo vitu vyengine hivi vidogovidogo vitawavua nguo muonekane si lolote si chochote ktk nafasi mlizonazo.
Hayo maeneo ni strictly prohabited kupiga picha wala video.