Wanajeshi kwa waliohusika na tukio hili wawajibishwe

Hata Kama jamaa ingekuwa ni makosa yake lakini haikupaswa kuingiza gari humo alipotakiwa kuingiza gari! Kujipeleka mahali ambapo utakuwa huna utetezi wa aina yoyote ndio kosa la kiufundi alilofanya mshikaji.. kwani tunafahamu hulka za hao jamaa raia huwa wanatuchukulia kama watu tusio na haki na wenyewe ndio wenye mamlaka ya kufanya uwezavyo!.

Nini kama wangembambikia kesi nzito nayeye ameshajitia dosari ya kuingia chini ya utawala wao..?
Mwanaume upo kwenye mazingira yako unategemeaje nguvu ya mtu mwengine ambae yupo mbali ambapo mpaka aje afike chamoto utakuwa ushakiona! Ati mjomba wangu mbunge!..😂

Aliposimamishwa hiyo ndio ilikuwa nafasi yake ya kutoroka na sio kukubali kuingia kwenye mdomo wa mamba,ambae nae barabarani sio mahala pake!

Wito wangu.. hakuna aliejuu ya sheria hivyo watu wa usalama tumieni mamlaka yenu pale panapostahili,ubabe na majivuno sio kitu chenye afya pale ambapo hapastahili...

Mamlaka zinazohusika zinapaswa ziingilie kati na ziwawajibishe kila mmoja kwa haki ili kudhihirisha hakuna aliejuu ya sheria,pia kila mtu lazima awe na utambuzi binafsi katika nafasi aliyonayo vitu vyengine hivi vidogovidogo vitawavua nguo muonekane si lolote si chochote ktk nafasi mlizonazo.
Naomba kutoa ushauri kwa vijana na hizi smartphone zao, si kila kitu ni cha kushoot video au kupiga picha.

Hayo maeneo ni strictly prohabited kupiga picha wala video.
 
Naomba kutowa ushauri kwa vijana na hizi smartphone zao, si kila kitu ni cha kushoot video au kupiga picha.

Hayo maeneo ni strictly prohabited kupiga picha wala video.
Sijazungumzia upigaji picha mkuu, ila Ahsante kwa kumbusho.
 
Utanijua Mimi ni Nani Imeanza kwa kasi,
Hawa vijana siku hizi wanadhalilisha idara,
Wanataka mzena paonekane ni mahala pa kuamulia traffic cases,ile ni sehemu nyeti sana

Wangempeleka hata oysterbay kwa wahusika,ilikuwa inatosha.

Alafu kingine hawa watu wetu maana yake ile VIDEO Wamekosa ufahamu wa kuifuta,wanadhalilisha hiyo kombat na idara..
 
Na ndipo hapo ninapokuja na huu uzi kuwa kosa la jamaa ni kukubali kuingiza gari mule kwenye mamalaka za watu wengine maana wanaweza kukufanya lolote,na hata baadae ukaonekana wewe ndio mwenye makosa!

Neno "jamaa" ndipo linapokuwa tenge. Kiwakilishi "jamaa" kwa "dogo" kiswahili kina goma.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Unafikiri ule mtutu huwa unalengwa tu kama manati..? Mihadarati walihakikisha kuwa imo mule..? Mkuu ni hatari zaidi kujiingiza kwa hao jamaa ktk namna hiyo na hiyo video ndio Imemsaidia naona huwajui hao jamaa.😂
Mnaandika vitu msivyovijuwa, pale ni makumbusho usalama wa Taifa na makazi pia ya walinzi wa viongozi.

Hao wenye kombati ni makirikiri walinzi wao Usalama wa Taifa, hata Makonda alivamia clouds na hawa.

Haya Mav 8 yenye vimulimuli mkiyaona barabarani muwe mnayapisha yapo above law za sheria za barabani, wanaweza kupita hata na Rais bila kujuwa wakiwa kwenye oparesheni zao bila kutumia msafara rasmi wa Rais.

Tatizo la vijana wa sasa ujuwaji umezidi hizo gari zipo juu ya sheria za barabarani ila ukiwa kiburi endelea kubisha tu.
 
Jinga kabisa wewe zipo juu ya sheria ipi hebu acheni nidhamu ya uoga!. Sio kila muda ni wa mamlaka by the way uzi wangu unazungumzia jamaa kukubali kuingia humo na kosa ni la kitrafiki.
 
Hata Kama jamaa ingekuwa ni makosa yake lakini haikupaswa kuingiza gari humo alipotakiwa kuingiza gari! Kujipeleka mahali ambapo utakuwa huna utetezi wa aina yoyote ndio kosa la kiufundi alilofanya mshikaji.. kwani tunafahamu hulka za hao jamaa raia huwa wanatuchukulia kama watu tusio na haki na wenyewe ndio wenye mamlaka ya kufanya uwezavyo!.

Nini kama wangembambikia kesi nzito nayeye ameshajitia dosari ya kuingia chini ya utawala wao..?
Mwanaume upo kwenye mazingira yako unategemeaje nguvu ya mtu mwengine ambae yupo mbali ambapo mpaka aje afike chamoto utakuwa ushakiona! Ati mjomba wangu mbunge!..😂

Aliposimamishwa hiyo ndio ilikuwa nafasi yake ya kutoroka na sio kukubali kuingia kwenye mdomo wa mamba,ambae nae barabarani sio mahala pake!

Wito wangu.. hakuna aliejuu ya sheria hivyo watu wa usalama tumieni mamlaka yenu pale panapostahili,ubabe na majivuno sio kitu chenye afya pale ambapo hapastahili...

Mamlaka zinazohusika zinapaswa ziingilie kati na ziwawajibishe kila mmoja kwa haki ili kudhihirisha hakuna aliejuu ya sheria,pia kila mtu lazima awe na utambuzi binafsi katika nafasi aliyonayo vitu vyengine hivi vidogovidogo vitawavua nguo muonekane si lolote si chochote ktk nafasi mlizonazo.
Hivi alipochomekewa kwenye mataa ya mwenge,angeamua kuibadilisha njia,hata kama alikuwa anaenda moroco,angeingia sinza,juu kwa juu mpaka moroco,ingetokea nini?tatizo la watu wa dar kupenda ubabe kwa kila kitu,vitu vingine ni vya kupotezea,bongo hakuna demokrasia,Wala sheria,watu kibao wanabsmvikiziwa kesi,kuuliwa,
Hao jamaa,wanaweza kujitetea kwamba wewe ni jasusi au unatumiwa na majasusi wa nje,wanaweza wakapandikiza hata passport bandia kwenye gheto lako kuonyesha wewe ni raia wa Rwanda au Kenya,wakaonyesha hata picha ukiwa unapewa mafunzo ya kijeshi,sasakwanini utake Shari na watu usiowajua?wakati mwingine tujifunze kupotezea ishu zisizo na faida,wangempiga risasi pale pale?,angepata faida gani?
 
So we unaona angefanyaje..?
 
Jinga kabisa wewe zipo juu ya sheria ipi hebu acheni nidhamu ya uoga!. Sio kila muda ni wa mamlaka by the way uzi wangu unazungumzia jamaa kukubali kuingia humo na kosa ni la kitrafiki.
Akili zako hazina tofauti na hao waliopiga video eneo la kijeshi.

Hizo ni gari za oparesheni huwa hazisimami popote, zinaweza kumbeba hata mkuu wa nchi bila kutambulika.

Huu ubishi wenu utawafikisha pabaya, kitu usichokijuwa unapoelekezwa jaribu kuelewa.
 
Dah! Mkuu we ni mwalimu wa kiswahili nini..?
Mi sijakuelewa bado ndugu yangu!😂

"Jamaa" laweza simama badala ya "njemba" lakini si "mtoto, binti au kijana mdogo yaani dogo".

Tofautisha "kajamaa, kijamaa, na jamaa." Matatu hayo ni tofauti.

"Wajuba wale wangependa tutumie neno jamaa kudogosha uovu wao. Hawa wamemwonea dogo."

Naomba kutoa hoja.
 
Hivi alipochomekewa kwenye mataa ya mwenge,angeamua kuibadilisha njia,hata kama alikuwa anaenda moroco,angeingia sinza,juu kwa juu mpaka moroco,ingetokea nini?tatizo la watu wa dar kupenda ubabe kwa kila kitu,vitu vingine ni vya kupotezea,bongo hakuna demokrasia,Wala sheria,watu kibao wanabsmvikiziwa kesi,kuuliwa,
Hao jamaa,wanaweza kujitetea kwamba wewe ni jasusi au unatumiwa na majasusi wa nje,wanaweza wakapandikiza hata passport bandia kwenye gheto lako kuonyesha wewe ni raia wa Rwanda au Kenya,wakaonyesha hata picha ukiwa unapewa mafunzo ya kijeshi,sasakwanini utake Shari na watu usiowajua?wakati mwingine tujifunze kupotezea ishu zisizo na faida,wangempiga risasi pale pale?,angepata faida gani?
😄😄😄 Ganja mixer makushabu Ni hatari Sana.
 
Akili zako hazina tofauti na hao waliopiga video eneo la kijeshi.

Hizo ni gari za oparesheni huwa hazisimami popote, zinaweza kumbeba hata mkuu wa nchi bila kutambulika.

Huu ubishi wenu utawafikisha pabaya, kitu usichokijuwa unapoelekezwa jaribu kuelewa.
Unapokuwa na majukumu makubwa ya kulinda viongozi, kuna mambo hayawezi kuwa kipaumbele.

Barabarani kuna mambo mengi yanatokea kila wakati, na hayo mav8 watu wanayo ambayo ni private.

Mwanausalama unapoliendesha kunaweza tokea ubishani wa kawaida huko barabarani.

Mwanausalama anayejua maadili yake hawezi acha anachofanya na kumfatilia raia wa kawaida ambaye walipishana kidogo huko barabarani.

Labda kama ameona hatari yenye kiwango cha kusababisha usalama kutokuwepo.

Wale askari hawakuwa sahihi. Walipaswa wampuuze yule mtoto. Tuna tatizo la kutatua mambo madogo kwa kutumia nguvu kuuuuubwa kwa ajili ya utambuzi.

Unaacha kazi zako mnashuka na mabunduki na magwanda kumshughulikia mtoto mmoja mliyepishana kwenye mataa. Huenda wala hakukutokea ajali, wala hakukutokea mauaji ila mambo ya kawaida ya kupishana barabarani.
 
Wabongo kwa kukuza mambo tupo vizuri ila kujipigania kwa mambo ya maana tupo vibaya
 
Majasusi hao nawaamini sana ila wameniangusha sana. Dawa ya kudhibiti video iliyorekodiwa na simu papo hapo ni kuroot simu au kuiteketeza simu siyo kudelete video .kuna app na namna nyingi za kurejesha video iliyorekodiwa video ukafanikiwa kukamata simu hakikisha simu hiyo inakuwa mpya kabisa au unaiteketeza kabisa na usithubutu kuleta huruma maana Utajifedhehesha,Utaharibu kazi,Utafukuzwa kazi,utaaibisha familia na taifa lako au idara yako.
Kama ikitokea hujui kabisa wafuate Agent wa serikali aliyebobea kwenye elimu ya IT na unayemuamini akisaidiwa. Tafadhali msifanye uzembe huu mnafedhehesha Idara maana usijitetee kuwa wewe siyo IT Man Sisi Raia tujua nyie Mnajua vyote na ukiharibu tunajua Upeo wa Idara umeishia hapo.Mwisho nawapongeza Mlitumia hekima sana maana hakuna sehemu inayoonesha waziwazi kuwa Mnavunja haki za Binadamu
 
Ulichokiandika umekielewa?
 
Back
Top Bottom