Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
-
NEWS ALERT
Kutoka Tanga Mjini kituo cha Ngamiani Kusini kijiji cha Jamhuri B karani wa uchaguzi anawajazia watu sehemu za mgombea na kutiki kabisa kisha kumuelekeza kwenda kutumbukiza kwenye sanduku bila na mwananchi kuchagua MEKO.
@TumeUchaguziTZ huu ni uchaguzi wa hovyo sana
 
-
#UchaguziUpdate
Wananchi wa Jimbo la Same Magharibi wamemdhibiti mgombea Mbunge wa CCM Mathayo David Mathayo baada ya kuwasili kituoni huku akiongozana na magari mawili yanayodhaniwa kuwa na maboksi ya kura.
 
-
Mgombea ubunge Chadema Jimbo la Muheza @yosepherfkomba ameng'atwa na msimamizi mkuu wa kituo baada ya kutaka kufahamu kilichopo ndani ya mkoba huo, alipokataa kumonyesha akataka kutoka nje na huo mkoba, Yosepher akamzuia ndipo alipomjeruhi kwa meno..
 
Nimetoka kupiga kura katika kituo kimoja hapa Dodoma(Kikuyu),kwa hakika muitikio uko chini mno.Hakuna watu kabisa!!
 
-
#UpdatesUchaguzi

Kituo cha kupigia kura ofisi ya kijiji cha Mungushi, jimbo la Hai, wananchi wamefika saa 1 asubuhi lakini hakukuwa na karatasi za kupiga kura. Wamesubiri hadi saa 3 ndipo karatasi zikaletwa. Ilipofika saa 4 karatasi zikadaiwa zimeisha, na kutakiwa kusubiri. Tangu saa 4 wananchi hao wanasubiri karatasi hadi muda huu. Walipoona zimechelewa wakaanza kulalamika.

DC Sabaya amefika na kuwataka waendelee kusubiri. Walipohoji wasubiri hadi muda gani, Polisi wakafyatua risasi hewani kwa madai ya kuwatuliza. Kisha kukamata watu wawili kwa madai ya kupiga picha bila ruhusa na kuwasweka rumande kituo cha polisi Bomang'ombe. Hadi sasa haijulikani karatasi zitafika saa ngapi ili wananchi hao waendelee kupiga kura.!
 
Huu uchaguzi ni BATILI huyo anayejiita MWENDAWAZIMU akishirikiana na tumeccm na polisiccm wameuvuruga uchaguzi huu.

Iundwe Serikali ya mpito ya watu 5 hadi 10 kwa kipindi cha kati ya miezi sita hadi 12 ili waweze kuipitisha rasimu ya Tume ya Warioba kama Katiba yetu mpya kuja na namna ya kupata Tume huru ya uchaguzi na haya yakishakamilika ndiyo uchaguzi urudiwe.

Huyo Jiwe aondoke Ikulu haraka sana na asiwe na access na Serikali ya mpito ili kutunza ushahidi wowote kuhusu uhuni mbali mbali uliofanyika katika kuvuruga uchaguzi huu ikiwemo uchapaji wa karatasi za kupigia kura ambao unadaiwa kuna ufisadi wa hali ya juu wa billions za walipa kodi.
 
-
Mgombea ubunge Chadema Jimbo la Muheza @yosepherfkomba ameng'atwa na msimamizi mkuu wa kituo baada ya kutaka kufahamu kilichopo ndani ya mkoba huo, alipokataa kumonyesha akataka kutoka nje na huo mkoba, Yosepher akamzuia ndipo alipomjeruhi kwa meno..
Wacha ang'atwe tu maana hizo pochi ni mali za mtu binafsi, anakagua kama nani??
 
-Mwenyekiti wa Jimbo la Kigoma Mjini Bwana Suleiman Simba amekamatwa na Polisi Kituo cha kupigia kura cha Stendi Mpya kata ya Kasingirima, alikuwa anazuia kura ZILIZOKWISHAPIGWA kuingizwa Kituoni. Usalama wa Taifa ndio wanafanya kazi hiyo
 
Leo nilipoingia kupiga kura nimekutana na makarani ambao walikuwa wakinakili namba za KITAMBULISHO CHANGU CHA MPIGA KURA kwenye Karatasi ya kupigia kura.

Hizi taarifa zikiingizwa kwenye system basi itakuwa ni shughuli nyepesi kujua mimi nimepigia kura chama gani.

Sasa endapo zitaanza itikadi mfano, kazi wapewe wa vyama fulani tu au mikopo wapewe watu fulani tu basi hii itachochea sana mpasuko mpya,
Acha uoga bhana hakuna mtu wa kuingiza mamilioni ya makaratasi ya kura Tz nzima kwenye system.

Mna hofu ya nini?
 
Back
Top Bottom