BADO MAKONDA NI MSHINDI
Na, Robert Heriel
Makonda anayohaja ya kuwashukuru sana watu wa kigamboni. Kwa kweli matokeo aliyoyapata kwake ni kama ushindi kutokana na kuwa, mpinzani wake alikuwa anatetea ubingwa.
Tofauti ya kura 68 ni ndogo sana.
Ukiangalia matokeo katika maeneo mengine utaona watu wakiachwa kwa mamia ya kura, wengine wakiadhibiwa kwa kushindwa kufikisha kura kumi tuu.
Makonda bado ni mshindi, na unapaswa umshukuru Mungu na watu wa kigamboni kwa kura ulizopata.
Naamini utaibuka kidedea huko mbeleni. Kila la kheri.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300