Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Ni kwelikati ya wabunge waliohama vyama Silinde kapata kura nyingi na ni muda mfupi sana anaweza kusimama hapo kwenye hilo jimbo.Ngoja wataamua wenyewe huko.
 
Kama mkristo na kama mtanzania naunga mkono hoja.. Sio kila kitu ni dini au kabila..
Unajua watu tunapenda sana kuendekeza mambo ya kijinga! Hata huko Zanzibar unaweza kukuta ni watu wenyewe tu wanajishtukia kwamba "Mkristo mimi, atanichagua nani huku" badala ya kuingia ulingoni ukakataliwe kwa vitendo badala ya kutumia hisia!

Watu tunasahau kwamba Mzee Sepetu alikuwa Mkristo na alihudumu Zanzibar kwa vyeo mbalimbali!! Sasa mtu ambae alihudumu kwa vyeo vikubwa ndo tuamini angegombea ubunge asingeupata eti kisa Mkristo!!!
 
Katika kura zilizonivitia ni hizi za Tunduma.
Silinde amehama kutoka Upinzani na hapo hapo akahama jimbo.
Ukitazama matokeo ya kura za maoni utaona ni kwa kiasi gani ameweza kujenga ushawishi ndani ya CCM katika muda mfupi.
Hapa ndio unaelewa ile hofu ya MNeC kutoka Tunduma.
All in All CCM inayo hazina ya taarifa ya mchakato ulivyoenda nchi nzima...yaani nani kashinda kwa kuchaguliwa bila kuhonga,nani kahonga na wakati gani alihonga.
Nani anakubalika na wananchi kwa ujumla nani ana uwezo wa kukinadi chama ndani ya jimbo,nje ya jimbo na kimataifa n.k

Kwa hiyo tushushe pumzi mchakato unaendelea.
Kigamboni Kuna mchezo umefanyika so bure,harufu ya rushwa na kukomeshana.

CC inatakiwa kufanya uchunguzi kwa Hawa wanaoteuliwa ili kupata viongozi bora na wenye maslahi mapana zaid kwa wananchi.
Watu wamebanwa maslahi yao Sasa wanaamua kuleta urafiki na kutumia kilambinu kutaka kuwatoa waliowabana ili waeze kuendelea kupiga.
 
Unachosema Ni sahihi kibamba ccm haina nguvu hivyo aliogopa kupetwa na John mnyika, kawe hata Kama angepita angekumbana na kisiki halima mdee, kimsingi makonda ni mwoga sana
Kigamboni lilikuwa ni jimbo Sahihi kwake, maana hata Upinzani hakuna Strong candidate mpaka muda huu ambaye katia nia. Kwa kama kama atapita kwenye mchakato wa maoni alikuwa anaiona Dodoma ile pale. Kimbamba na Ubungo ni safe seats za Chadema.
 
Source ITV
115756771_304855504258630_4608777629073981087_n.jpg
Kuna ukweli wowote kwamba Mwakyembe amegaragazwa?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa wapuuzi flani walihama wakapewa nafasi CCM saivi wamewanyoosha, Shukwani ziwaendee CCM na mwenyekiti wao. Mwenyekiti kashamaliza teuzi za UDAS, URC, UDC, U-RAS waliopoteza watajutia nafasi walizopoteza.

  • Mtulia
  • Katambi
  • Kafulila
  • Nassari

Wateule walioacha teuzi nao wamegaragazwa

Wasanii waliojiforogoa kwamba wanaipenda CCM nao CHALIIIII
Walishalipwa mshiko wao wakala pesa ikaisha
 
Kigamboni Kuna mchezo umefanyika so bure,harufu ya rushwa na kukomeshana.

CC inatakiwa kufanya uchunguzi kwa Hawa wanaoteuliwa ili kupata viongozi bora na wenye maslahi mapana zaid kwa wananchi.
Watu wamebanwa maslahi yao Sasa wanaamua kuleta urafiki na kutumia kilambinu kutaka kuwatoa waliowabana ili waeze kuendelea kupiga.

Nyie acheni mchezo mchafu. Mtu wenu hakubaliki, period. Hilo la Kigamboni ni picha ya halisi ya uchaguzi utavyofanyika October.
 
Name recognition ndio factor kubwa nimegundua.

Kiwango ambacho wamesikia jina lako kwenye jamii, hata kama ni kwa udaku.

Erick Shigongo anashindaje siasa za ubunge?

Namshangaa Amber Rutti hajagombea.
Shigongo tangu 2010 anagombea huko kwao mpk leo.
 
Katika kura zilizonivitia ni hizi za Tunduma.
Silinde amehama kutoka Upinzani na hapo hapo akahama jimbo.
Ukitazama matokeo ya kura za maoni utaona ni kwa kiasi gani ameweza kujenga ushawishi ndani ya CCM katika muda mfupi.
Hapa ndio unaelewa ile hofu ya MNeC kutoka Tunduma.
All in All CCM inayo hazina ya taarifa ya mchakato ulivyoenda nchi nzima...yaani nani kashinda kwa kuchaguliwa bila kuhonga,nani kahonga na wakati gani alihonga.
Nani anakubalika na wananchi kwa ujumla nani ana uwezo wa kukinadi chama ndani ya jimbo,nje ya jimbo na kimataifa n.k

Kwa hiyo tushushe pumzi mchakato unaendelea.
Tuwekee matokeo hapa
 
Back
Top Bottom