Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Walioko huko watupe picha Betty ya joto lilivyo, Mbeya, Kigamboni, Arusha, Misungwi nk japo mie nabashiri vinara kuwa nje ya tatu bora.

Nayasubiri kwa hamu ya misungwi ,kigamboni,kawe,
Natumain mnyeti anagombea misungwi
 
Uchaguzi2020 Zoezi la kuhesabu kura katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa limekamilika na Waziri wa Aridhi William Lukuvi ameibuka mshindi kwa kupata kura 453. Lukuvi - 453 Kiyoyo - 16 Mwilinge - 5 Kidunye - 5 Kalinga - 4 Mfilinge - 4 Kushoka - 0 Chengula - 0 Gange - 0
 
kigamboni imetoka hiyoo, sasa ni dhahiri maiti za watu zitaendelea kuokotwa coco beach kila siku….
 
KURA ZA MAONI KINONDONI: ZAMARADI APATA KURA MBILI Mtangazaji zamaradimketema amepata kura mbili kinyany’anyito za kura za maoni jimbo la Kinondoni. Kura zilivyohesabiwa kwa uwazi mbele ya wagombea wote pamoja na wajumbe. Abbas Tarimba 171” Idd Azam 78 Kalapina 1
 
Kuhusu Kigamboni naomba mwenye matokeo ya uhakika awe anatujuza.

Ieleweke Kigamboni ndipo anapogombea aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na ambaye kwa namna moja ama nyingine aligusa watu wengi walio kubaliana naye na walio kuwa hawakubaliani naye.

Hivyo kwa mada hii naomba tujuzane kwa yanayojili huko Kigamboni.
Sikujua kama Makonda ni maarufu kiasi hiki,!
 
Makonda Chali kabisa. Ndugulile kamuacha mbaaali
 
Back
Top Bottom