Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Kwani bashite amekatwa? Mbona mnaongea ongea tu kama mpo snapchat!?
 
Mwambie Bashite aliyekutuma kuwa huu ndiyo muda wake wa kwenda kuendelea na kazi yake ya upishi kwenye meli ya wagiriki
IMG-20200720-WA0055.jpg
 
Wanabodi,
Kile kipute kigumu kuliko vyote cha kura za maoni CCM ni jimbo la Kawe
ambapo watu 176 wamejitokeza kuwania jimbo hilo.

Mimi mwana JF wako, Pasco Mayalla niko usawa huu kutuletea Live kipute hiki Kutoka Ukumbini wa Kiramuu Hall hapa Mbezi Beach, kushuhudia Upigaji Kura za Maoni CCM, Wagombea 176 Kuchuana Kumposa Halima Mdee Ili kumuoa, kumtuliza na Kumpumzisha awe mama wa nyumbani, archie jimbo, atulie kulea mume, watoto na kujenga familia.

Nani Kuibuka Kidedea?!.

Andamana nami.

Paskali
 
Bado kamari ya roho mbaya haijakaa ukisikia nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza 🤣😅🏃
 
Hivi wanaruhusu hao wote 176 kujinadi mbele ya wanaCCM au wameshawachuja?

Kigamboni wameonyesha njia inayopaswa kufuatwa na wana Kawe. Watu kama Gwajima wenye ndimi mbilimbili na wanaogeuka kwa speed mara 100 ya kinyonga hawafai. Fyekelea mbali. Gwajima akitaka kupanua akapanulie kanisani kwake
 
Viti maalum havitolewi kwa walioomba kura za wananchi wakashindwa kuzipata. Kwa Makonda akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndiyo the most prestigious position kwa wakuu wa mikoa halafu akaipiga sadaka alikosea sana. Ni afadhali kutumbuliwa na mtu mmoja aliyekupa madaraka hayo kuliko kushindana na watu wengi na ukaonekana kuwa hufai.
Na safari hii dhana na tuhuma za upendeleo wa kubebwa zinawekwa sawa.
 
Hahahaaaaaaaaa a ASA ASA Mpwaaaaaa balaaa siasaa wachatule mamboyetu badalayakuwazaa PESA walizogaia wajumbe BADOO wamenyooshwaa
CCM original wanapiga spana hatari

Ova
 
Ni wazi hata MaCCM hayakupendezwa kabisaaaaa na biashara ya kununua Wabunge wa upinzani. Waliojiuza wengi hadi sasa wamepigwa chini. Wengine wamepata kura nusu ya umri wao. Ni wakati sahihi, hata kwenye teuzi hizo wasipate, watakula walipopeleka mboga.
Peter Lijualikali Kura 4 ....WANA IZENGO WAMEMUAMBIA MWENYEKITI WAO KWA NGUVUUUUUUUUU KUWA WALIKUWA HAWAPENDEZWI NA TABIA YA KUNUNUA WABUNGE NA MADIWANI NA KULAZIMISHA WAGOMBEEE .........
 
Hizi kura za maoni binafsi naona zinakosewa, tena kwa vyama vyote, sioni maamuzi ya wapiga kura kwenye hii michakato yakiheshimiwa. Mtu unampigia kura anashinda, halafu bado unakuja kuambiwa bado kuna vikao vya juu ndio vitaamua nani awe muwakilishi wa jimbo husika.

Huyo Mwenyekiti wa kikao cha ngazi ya juu nae anakwambia "itategemea siku hiyo nimeamkaje", kama hali ndio hiyo, kwanini hivyo vikao vya juu visiwe vinaamua moja kwa moja nani awe mgombea, badala ya kupotezeana muda kumpa mtu kura za ushindi halafu mwisho wa siku bado mnabaki kwenye kitendawili msiwe na jibu kama mliyemchagua atapitishwa na vikao vya juu?!
 
Back
Top Bottom