JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Nimekutana na hii video TikTok na maelezo haya, kuna uhalisia wowote wa hili? == Taswira inayozidi kujitokeza ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inazidi kuibua maswali mengi kuliko majibu, huku vitendo vya baadhi ya viongozi vikionekana kukiondoa chama hicho kwenye misingi ya kidemokrasia na kukisogeza karibu na mtindo wa magenge ya kihuni. Katika video inayosambaa kwa kasi, baadhi ya wanachama na viongozi wanaonekana wakizushiana vurugu kufuatia maswali yaliyoibuliwa kuhusu kampeni ya kuchangisha michango inayofahamika kama ‘Tone kwa Tone’. Badala ya kutoa majibu ya kistaarabu na ya uwazi kuhusu matumizi ya fedha hizo za wanachama, baadhi ya viongozi wanatuhumiwa kutoa amri ya kushambuliwa na kupigwa kwa wanachama...
Wazee wa chadema wameamua kujitoa sababu Amina viongozi wa chadema wana Mipango michafu nda ya taifa letu, ni dhahiri Mipango waliyonayo ni ya Liguria nchi yetu sababu ya tamaa zao ndio maana hata wazee wa chama wameona hawawezi kuwa sehemu ya uchafu wanaoupanga Pia ukumbuke kuwa ndani ya chadema kuna wizi na upigaji wa pesa za michango ambazo viongozi wa chadema wanagawana na kwenda kuzifanyia anasa night club na madem
Wakuu NImekutana na huu ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa X ingawa sijaiona je uhalisia ni upi? "tulifanya makosa wengine kwa kujua wengine kwa bahati mbaya, wengine waliondoka kwa sababu ya mifumo iliyo kuwa inalalamikiwa.,,msituhukumu kwa mapito yetu Bali fungueni Milano karibiaheni wakosaji Wanao jutia na kuomba msamaha, haturudi kutafuta vyeo Bali kuongeza Nguvu ya kumuondoa mkoloni mweusi ili tuapte katiba mpya #Free tundu Lissu Je mtatuhukumu Hadi lini? Kama Kuna adhabu ttupe ili tuitumikie lakini turudi kwenye njia ya Mapambano"
Siku za hivi karibuni, taifa la Afrika Kusini limeendelea kukumbwa na changamoto ya kuongezeka kwa mashambulizi na vurugu za chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Maandamano hayo yanadaiwa kulenga kuwaondoa raia wa kigeni nchini humo. Pamoja na kuendelea kwa matukio hayo, kumekuwa pia na ongezeko la matumizi ya picha za zamani na picha zilizohaririwa kwa teknolojia ya akili unde (AI) katika kuelezea matukio ya sasa yanayoendelea nchini humo. Moja ya chapisho lililosambaa kupitia chombo cha habari cha Mwananchi lilikuwa na kichwa kisemacho, “Ukaburu unarejea Afrika Kusini”, kikitumia picha ambayo kwa uhalisia ilipigwa mwaka 2015 wakati wa machafuko yaliyolenga raia wa kigeni katika eneo la Johannesburg Central Business District (CBD)...
Kumekuwepo na chapisho linalosambaa kwenye mtandao wa Facebook likimuonesha Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, akipiga magoti mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake ya siku moja nchini Tanzania. Je ?ni upi uhalisia wa chapisho hilo la picha ambalo lina sambaa kwa kasi kwenye mitando ya kigiditali..
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa katika mitandao ya kijamii, hususan Facebook na Instagram, likiwa na nukuu inayoambatana na video inayodaiwa kuwaonesha waandamanaji wakishambuliwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Chapisho hilo linadai kuwa tukio hilo linahusiana na hali ya hivi karibuni ambapo raia wa kigeni wanadaiwa kushambuliwa na kulazimishwa kuondoka nchini humo.
Kumekuwepo na chapisho la video kwenye mtandao wa Facebook likidai kuwa Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akiwa pamoja na watendaji mbalimbali wa serikali wakiwemo mawaziri, walionekana wakiendesha baiskeli katika mji wa Isfahan wakielekea kukagua miundombinu kwenye maeneo ambayo yalikabiliwa nma mashambulizi makali ya vita. katika hilo Chapisho hilo lilisambaa likiwa na ujumbe unaosema: "Rais wa Iran 🇮🇷 akiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali, wakiwemo mawaziri, wakielekea kwenye ukaguzi wa miundombinu ndani ya mji wa Isfahan kwa kutumia usafiri wa baiskeli. Ikumbukwe mji huo ni miongoni mwa miji iliyoshambuliwa sana." Hata hivyo, kupitia ufuatiliaji wa kidigitali kwa kutumia njia ya manneo mhimu na vyanzo vingine vya habari...
Back
Top Bottom