Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Kwa kweli tangu juzi kawe, jana segerea na Leo Arusha Tundu Lissu ameanza kutema sera kali kweli
Zinahusu maisha ya mwananchi mmojammoja na Taifa kiujumla
Uzuri wa sera zake kuna zile ambazo ziko specific kwa mji husika na kuna zile ambazo zinahusu nchi nzima

1. Lissu kazungumzia ugumu wa maisha ya mfanyakazi na jinsi atakavyoyaboresha kwa kulipa malimbikizo yote wanayodai na kuwalipa nyongeza zao za mishahara za kisheria(annual increments)

2. Amezungumzia uonevu wanaofanyiwa wafanyabiashara wetu na kwamba ataundoa

3. Amezungumzia kuhusu elimu bora na siyo bora elimu, amezungumzia kuhusu elimu ya ujuzi wa kazi siyo ya kukariri

4. Amezungumzia kuhusu viwanda na kuvutia mitaji ili kutoa ajira kwa vijana wetu

5. Amzezungumzia kuhusu diplomasia yetu iliyoshuka na jinsi atakavyorudisha mahusiano bora ya kimataifa

6. Amezungumzia bima ya afya kwelikweli siyo hii ambayo wazee wetu wakishastaafu wanaambiwa waongeze hela ili waweze kuwekwa kwenye bima ya magonjwa nyemelezi ya wazee

7. Amezungumzia kuhusu kuirejesha Arusha kuwa kitovu cha utalii

8. Amezungumzia kuhusu katiba mpya, ameonyesha ubovu wa katiba ya sasa ambayo imelinyima hata bunge uwezo wa kuanzisha hoja ya namna ya kutumia pesa za nchi isipokuwa tu kama hoja hiyo imeanzishwa na serikali.

9.Amezungumza kuhusu haki za watu, ametetea masheikh walio jela kinyume cha sheria, kwa mfano amesema Arusha peke yake kuna Masheikh 70 wako jela achilia mbali wale masheikh wa uamsho.

10. Amezungumzia kuvunjia wananchi nyumba kikatili etc

11. Kszungumzia mzigo mzito wa makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na amesema atashusha makato hayo kwa mwezi kutoka 15% hadi 3% ya mshahara kwa mwezi

12. Amezungumzia kuhusu adha za vitambulisho vya kimagumashi vya wamachinga amesema ataondoa mzingo wa shilingi 20000 ya kitambulisho cha wamachinga pesa iliyoanzishwa na Bashite na Magufuli

13. Amesema ataanzisha sheria ya haki ya mlipa kodi "Bill of taxpayers rights" ili waweze kulindwa kisheria badala ya utaratibu wa sasa ambao wafanyabiashara wanaonewa sana na TRA na hawana pa kukimbilia, kila wanapokimbilia wameshafungwa minyororo

14. Amezungumzia kuhusu uhuru wa habari, kuwa ataondoa sheria kandamizi zilizotungwa na Magufuli kumlinda yeye badala ya kusaidia taaluma kukua

15. Amesema ataomesha matumizi ya hovyo ya pesa za serikali, siyo rais akiamka asubuhi anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake ambapo ndege inatua mara mbili kwa mwaka siku anayoenda kula Christmass na pasaka

16. Lissu anazungumzia kuhusu UHURU, HAKI, MAENDELEO

Kwa kweli Lissu unatisha baba endelea kupiga spana mwana wa Tanzania
Sijaona la maana hapo, anaongea mambo yasiyo na uhalisia
 
Magufuli anatosha, hizi zingine mbwembwe tu
Ila hizo hoja zote ni nzito sana!! Na tukisema ukweli awamu ya 5,zote imezipuuzia kabisa, kama wananchi wangekuwa wanasikiliza sera na kuzifanyia kazi haki ya mungu, mapeeema sana!! Ila kwa kuwa ndio wale wale.... Ila hakuna mtanzania hata mmoja ambaye haguswi na hoja hizo hapo juu!!! Hizo hoja ni kama maji, isipokugusa hii, inayofuata lazima tu ikuguse!!!
 
Hawa watu wa Arusha hawana shukrani, wamesahau kama Profesa Magufuli ameifufua ile reli ya mkoloni iliyokuwa imekufa.

Na juzi kati mshakunaku polepole alikuja kumsifia master wake.
Hiyo nayo treni au ni makumbusho ya Taifa, watoto waone mkoloni alivojenga reli ya kuhamisha raslimali zetu. Labda wifanye kambi ya CCM ya kuandaa mapingamizi ya uchaguzi.
 
Bora hata angekuwaa anayala kistaarabu,anatafuna huku anaongea,mama unataka kupanuliwa wapi mama,huko mbelee...dah
Dah ile clip nilicheka sana, yaani utadhani jamaa aliyetokea interior huko asiyejua hata ustaarabu wa mjini, Meko kama sio kulindwa anaweza kuvua viatu akiiona lami.
 
Hawa watu wa Arusha hawana shukrani, wamesahau kama Profesa Magufuli ameifufua ile reli ya mkoloni iliyokuwa imekufa.

Na juzi kati mshakunaku polepole alikuja kumsifia master wake.
Reli alijenga mkoloni na bado akatimuliwa, ije kuwa huyu Pombe!!
 
Kwa kuwa hashidi inabaki kuwa kelele tu
Sera siyo lazima zitekelezwe za aliyeshinda tu. 2015 alishinda JPM wa CCM, lakini sera nyingi za CDM zimebebwa na CCM. Moja tu katika nyingi ni ya Elimu bure, japo utekelezaji wake ni jambo linalohitaji mjadala mwingine.
 
Back
Top Bottom