Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bravo my Lord .... though huku Yorkshire tunatamka, bravo me Lord 😁Asante. Lissu anahitaji kuungwa mkono. Ameibeba Tanzania ya kipekee sana kichwani pake. Tusipomchagua Lissu na kumweka ikulu mwaka huu 2020. Watanzania tutajuta milele
Shikamoo Slaa 2010
1).Pia asisahau kurudisha maduka ya Jeshi duty free shopsKwa kweli tangu juzi kawe, jana segerea na Leo Arusha Tundu Lissu ameanza kutema sera kali kweli
Zinahusu maisha ya mwananchi mmojammoja na Taifa kiujumla
Uzuri wa sera zake kuna zile ambazo ziko specific kwa mji husika na kuna zile ambazo zinahusu nchi nzima
1. Lissu kazungumzia ugumu wa maisha ya mfanyakazi na jinsi atakavyoyaboresha kwa kulipa malimbikizo yote wanayodai na kuwalipa nyongeza zao za mishahara za kisheria(annual increments)
2. Amezungumzia uonevu wanaofanyiwa wafanyabiashara wetu na kwamba ataundoa
3. Amezungumzia kuhusu elimu bora na siyo bora elimu, amezungumzia kuhusu elimu ya ujuzi wa kazi siyo ya kukariri
4. Amezungumzia kuhusu viwanda na kuvutia mitaji ili kutoa ajira kwa vijana wetu
5. Amzezungumzia kuhusu diplomasia yetu iliyoshuka na jinsi atakavyorudisha mahusiano bora ya kimataifa
6. Amezungumzia bima ya afya kwelikweli siyo hii ambayo wazee wetu wakishastaafu wanaambiwa waongeze hela ili waweze kuwekwa kwenye bima ya magonjwa nyemelezi ya wazee
7. Amezungumzia kuhusu kuirejesha Arusha kuwa kitovu cha utalii
8. Amezungumzia kuhusu katiba mpya, ameonyesha ubovu wa katiba ya sasa ambayo imelinyima hata bunge uwezo wa kuanzisha hoja ya namna ya kutumia pesa za nchi isipokuwa tu kama hoja hiyo imeanzishwa na serikali.
9.Amezungumza kuhusu haki za watu, ametetea masheikh walio jela kinyume cha sheria, kwa mfano amesema Arusha peke yake kuna Masheikh 70 wako jela achilia mbali wale masheikh wa uamsho.
10. Amezungumzia kuvunjia wananchi nyumba kikatili etc
11. Kszungumzia mzigo mzito wa makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na amesema atashusha makato hayo kwa mwezi kutoka 15% hadi 3% ya mshahara kwa mwezi
12. Amezungumzia kuhusu adha za vitambulisho vya kimagumashi vya wamachinga amesema ataondoa mzingo wa shilingi 20000 ya kitambulisho cha wamachinga pesa iliyoanzishwa na Bashite na Magufuli
13. Amesema ataanzisha sheria ya haki ya mlipa kodi "Bill of taxpayers rights" ili waweze kulindwa kisheria badala ya utaratibu wa sasa ambao wafanyabiashara wanaonewa sana na TRA na hawana pa kukimbilia, kila wanapokimbilia wameshafungwa minyororo
14. Amezungumzia kuhusu uhuru wa habari, kuwa ataondoa sheria kandamizi zilizotungwa na Magufuli kumlinda yeye badala ya kusaidia taaluma kukua
15. Amesema ataomesha matumizi ya hovyo ya pesa za serikali, siyo rais akiamka asubuhi anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake ambapo ndege inatua mara mbili kwa mwaka siku anayoenda kula Christmass na pasaka
16. Lissu anazungumzia kuhusu UHURU, HAKI, MAENDELEO
Kwa kweli Lissu unatisha baba endelea kupiga spana mwana wa Tanzania
Ukimbana aende kwenye mdahalo simply anaweza ikimbia ikulu.Mdahalo na Lisu ataweza?
😂😂😂 umenikumbusha mbali sana mkuu!!Bravo my Lord .... though huku Yorkshire tunatamka, bravo me Lord 😁
Pamoja MkuuImeisha hiyo
Naomba nikiri. Nilimpa kura JPM 2015 na kumfanyia sana kampeni humu jukwaani but he has disappointed me big time!!Watanzania mwaka 2015 waliyahitaji mabadiliko, lkn hawakumuhitaji kiongozi muimla, walimchagua Lowassa bali kwa uhuni wa kimfumo akaletwa Pombe. Wameshaleweshwa kwa pombe haramu ya yule ambaye hawakumchagua.
Watanzania kwa mara nyingine tena hawataki kuleweshwa kwa itikadi chafu yenye kuwatia unajisi. Hawataki tena kuletewa madarakani mtu wasiyemtaka, bali wanamtaka kiongozi wa nchi awe kipenzi chao.
Kuna mboga mboga kibao zimasema zitampigia kura lisu na mbadoooDar haijafanya uamuzi wa kuwapiga chini Chadema. Nina picha kubwa sana ya Dar . Naona kama Dar ndo sehemu ambayo Lissu ataongoza kwa kura!!! Time will tell.
Jamaa ana akili mpaka basiKwa kweli tangu juzi kawe, jana segerea na Leo Arusha Tundu Lissu ameanza kutema sera kali kweli. Zinahusu maisha ya mwananchi mmojammoja na Taifa kiujumla. Uzuri wa sera zake kuna zile ambazo ziko specific kwa mji husika na kuna zile ambazo zinahusu nchi nzima....
Subiri shoooMagufuli anatosha, hizi zingine mbwembwe tu