Yupo vizuri. Yule wa upande mwingine ni mweupe sana kichwani na ni mnafiki sana na pia ana roho mbaya kama nyoka
 
Kwa comments hizi, na

Kwa kinachoendelea kwenye siasa, na hisia za watu inaonyesha Taifa lina maumivu na majeraha makubwa ambayo yanapaswa kutibiwa, kuponywa, na kupewa tumaini.

Mungu tupe mtu atakaesimama kwa zamu yake kutengeneza mahala palipomoka.

Taifa linamhitaji mtu wa namna hii
 
1).Pia asisahau kurudisha maduka ya Jeshi duty free shops
2) Kuna kitu wanasiasa hukisahau na Ni muhimu kwa uchumi na ustawi wa watu Ni
SUSTAINABLE URBAN AND RULAL PLANNIG" au upangaji wa miji na vijiji ili kuondoa makazi holela,

hatuwezi kuwa na population ya 60+ mil. Bila kupanga makazi na shughuli za kiuchumi

Mheshimi raisi Lissu likumbuke hili liwe kwenye vipaumbele vyako
 
Watanzania mwaka 2015 waliyahitaji mabadiliko, lkn hawakumuhitaji kiongozi muimla, walimchagua Lowassa bali kwa uhuni wa kimfumo akaletwa Pombe. Wameshaleweshwa kwa pombe haramu ya yule ambaye hawakumchagua.

Watanzania kwa mara nyingine tena hawataki kuleweshwa kwa itikadi chafu yenye kuwatia unajisi. Hawataki tena kuletewa madarakani mtu wasiyemtaka, bali wanamtaka kiongozi wa nchi awe kipenzi chao.
 
Naomba nikiri. Nilimpa kura JPM 2015 na kumfanyia sana kampeni humu jukwaani but he has disappointed me big time!!
Kwa jinsi ninavyoiona Tanzania ikizidi kudidimia kiuchumi, kiutawala hasa kwenye misingi ya utawala bora na haki, kimaendeleo hasa katika kubadirisha maisha ya watanzania kuwa mazuri na ya kupendeza sioni namna naweza mchagua Magufuli mwaka huu!! No way!!
 
Mods wa JF siyo kila thread ni ya kumerge, mnapoteza latest hot issues eti kwa sababu content zinashabihiana na mada ya wiki iliyopita, mnasababisha watu waliosoma mada wiki jana wasione umuhimu wa kusoma ya leo.
Kwenye siasa 24 hours ni nyingi sana kubadili upepo. Acheni kumergemerge threads mnapoteza moto, na mzuka, na kufuatilia habari

Sasa habari ya J'mosi utaimerge vipi na habari ya Jumatatu wakati mambo mengi yeshatokea hapo katikati? –Mnaboa na mnazingua kichizi sometimes.
 
Jamaa ana akili mpaka basi
 
Eti sumu haionjwi kwa kidole!! Mwaka huu ni heri kuionja "sumu" mpya kwa kiganja. Hata kama hatafanya chochote, walau tutaanza sehemu flani
 
Ni nani alipigwa risasi 16 kisha akapona?nitajie hata mmoja tofauti na Lissu.Kupona kwake ni mpango wa Mungu ili Tanzania ikombolewe katika nyanja zote.

Lissu ameandaliwa na Mungu kuwa rais wa Tz.Mungu mbariki Lissu,Mungu wabariki watanzania wote wampe Lissu kura za ndiyo Oktoba 2020.

Wauaji,Wachawi,Wavunjifu wa amani,Wapiga risasi watu,Watekaji,Waweka mapingamizi feki,Wanaojifanya wazalendo wakati si wazalendo washindwe kwa jina lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…