Kweli Kabisa, inabidi amzibe Magufuli mdomo...kunadi sera mpya za Chadema ni kupoteza muda, inatosha kumpiga Magufuli kwenye makosa yake, na mauongo yake
 
Hahaha angekuwa na hiyo intelligence usingehitaji kumshauri mgombea Upinzani vitu rahisi namna hiyo, yeye mtaji wake ni kama 50 Cent, kupigwa risasi, baasi!
 
Kuna mikoa ambayo lazima tumuulize JO POMBE anaendaje..

1. KAGERA
Aliwaambia hakuleta tetemeko.
Lissu ukifika huku mwaga sera, halafu waulize ikiwa aliwaacha na kuwananga hivyo, tena alikwapua na hela za michango..

2. MTWARA, LINDI.
Ishu ya korosho inawaumiza mpaka leo.
Mwaga sera, halafu waambie CHADEMA haitotumia jeshi au polisi kuingilia biashara hiyo, wanunuzi kutoka nje watakaribishwa kwa uhuru mpate bei nzuri.

3. Kule nchi ya Tanzania Visiwani.
Anaenda kuwaambia nn?

4. Zipo wilaya kama
- Butiama ujenzi wa barabara ya Arusha tangu akiwa waziri haujakamilika, kisa imepewa kampuni yake ya MAYANGA.

- KAKONKO, KASULU, KIBONDO
Kote huko barabara haikamiliki kisa kampuni yake ndo inajenga.
Wanajenga leo, kesho wanafumua.


N.k
 
CCM Wala hatuna kazi ya sijui kutafuta takwimu Wala.Popote tunapokuwa kazi yetu Ndogo tu kuwaambia wananchi mwenye macho haambiwi tazama

Barabara hiyo mpya mnaiona hamuioki wanajibu tunaiona.Kazi ya CCM hiyo

Hospital mpya hiyo mnaiona hamuioki wanasema tunaiona .Kazi ya CCM hiyo

Huduma nzuri ofisi za serikali mnaziona hamuziomi? Tunaziona .Kazi ya CCM hiyo

CCM hatuhitaji kuwapa lecture ya vitu vya jutunga Kama Chadema sababu they have nothing to show of their own !!!

Watu hawahitaji maelezo mareeefu !!! Wanajua uongo

Watu wanafurika mikutano ya CCM kwenda kwanza kuipongeza kwa iliyofanya na pili kusikiliza kingine kipi wanaenda fanyiwa

Hawaendi tu kusikiliza Kama kwenye mikutano ya Upinzani
 
Kunadi sera ni pamoja na kuonyesha mapungufu, kutokutosha kwa mpinzani wako kisha ukawashawishi wananchi jinsi wewe unavyotosha kuwazidi
Tangu 1995 njia hii imefanywa na wapinzani wote lkn haikuwai kuzaa mtunda. Nyie watoto wadogo ni bora kukaa kimya hamjui tunatoka wapi tunakwenda wapi.
 
Kunadi sera ni pamoja na kuonyesha mapungufu, kutokutosha kwa mpinzani wako kisha ukawashawishi wananchi jinsi wewe unavyotosha kuwazidi
Wala sio strategy sahihi kumponda mke wa mwenzio kuwa Ni Malaya hakumfanyi mkeo Malaya kuwa mtakatifu

Ndio maana kwenye interview mfano waombaji walioomba kazi wako elfu mbili Wakati nafasi Ni moja swali ambalo huwa gumu kulijibu Ni kwa Nini tukuchukue were tuwaache wengine elfu moja Mia Tisa tisini na Tisa? Huwezi kuelezea udhaifu wao kujenga hoja yako

Unajikita only kwenye strengh zako tu ndio maana CCM kampeni zetu Zina concentrate kwenye strength zetu tu hatuhangaiki na weakness za upinzani after all they are weak why waste time kueleza weakness ya mtu ambaye Kila mtu anamwoma weak? Mfano mtu ni kiwete Huwezi Simama jukwaani masaa unaeleza kuwa huyo mtu Ni kiwete !! Unapotezea muda watu
 
Pia awakumbushe wananchi jinsi watoto waliosoma private wanavyonyimwa mikopo na bodi ya mikopo ...pia wafanyakazi walivyonyimwa kupandishwa madaraja hasa walimu
 
Mrema hana IQ ya Lissu

2015 CCM ilichapwa asubuhi na mapema
Kwahiyo Dr. SILAA, EDWARD nao walikuwa vilaza? Lisu naye alikuwepo pia.

Mbinu ya kunadi mapungufu imetumika miaka 25 na imeprove kufeli sana. Endelee hivyo hivyo bila kutangaza sera mtavuna makapi.

Hata hivyo kwa katiba yetu, wapinzani wataendelea kusindikiza. Vipi walioenguliwa wameisharudishwa?
 
Ninyi kweli "weupe", badala ya kumuhimiza Lissu afafanue ilani yake kinaga ubaga watu waelewe Chadema inaweza kufanya nini tofauti na kilichokwisha fanywa na kinatachotarajiwa kufanywa CCM, bado mnabaki kupiga kelele ambazo watu hawana taimu nazo. Mwambie Lissu aWaeleze wananchi ninamna gani ataifumua TRA na kisha kuleta mbadala wake utakao fanya kazi bora zaidi ya TRA ya sasa. Pia aeleza namna atakavyolipa fidia kutoka " mfukoni mwake"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…