Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Kwenye mikutano yako

A. Anza kuwakumbusha wananchi ulaghai wa CCM kwa kutoa ahadi za uwongo kwa wananchi kwenye ILANI YAO ILIYOPITA NA MIKUTANO YAO YA KAMPENI.

1) Wakumbushe wananchi jnsi CCM ilivyoahidi katiba mpya kwenye ilani ya mwaka 2015 lakini Rais Magufuli akakataa baada ya kuapishwa akadai eti hakuinadi kwenye ksmpeni wakati imo kwenye ilani yao-Waulize wananchi kama wanaweza kuendelea kuwaamni watoa ahadi za uowongo

2)Wakumbushe wananchi ahadi ya CCM iiyoko kwenye ilani yao ya 2015 kuwa watatoa milioni 50 kila kijiji—Mpaka sasa hawajatoa hata thumni, Waulize wananchi wana sababu gani za kuendelea kuamini watu waongo

3)Wakumbushe wananchi namna Magufuli alivyoahidi kugawa laptop kwa kila mwalimu ili imsaidie kuboresha ufudishaji—Waulize wananchi ziko wapi hizo laptop na pia waulize wananchi kwa vipi waendelee kuamini watu wasioishi neno lao?

4) Wakumbushe wananchi namna ilani ya uchaguzi ua CCM ya mwaka 2015 inavyozugumzia kuendelezwa kwa sera ya kilimo kwanza lakini Magufuli alipoingia tu miongoni mwa vitu alivyoanza navyo ni kuifutilia mbali sera hiyo licha ya kuwa ni mpango upo katika ilani yao ya mwaka huo

5. Wakumbushe wananchi jinsi Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ilivyosema kuwa watoto watakaopata ujauzito serikali haitowafukuza shule—Wakumbushe jinsi Magufuli alivyoingia madarakani alivyokana ilani yake mwenyewe kwa kusema kuwa hao mabinti wakipata mimba atawafukuza shule za serikali kwa sababu hasomeshi wazazi.

B) Anza kuwaambia wananchi Ulaghai wa CCM ya sasa na hivyo Wasiiamini tena kuipa kura

1. Bashiru aliuambia umma kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu hawatotumia wasanii—Uongo mtupu, leo CCM wamegeuka waandaaji wakubwa wa disco za hadhara, juzi dodoma kulikuwa na wasanii zaidi ya 100. Kwa sababu CCM hawana sera za maana za kushawishi wananchi, wanasafiria nyota za wasanii

2)Wakumbushe wananchi kauli ya Magufuli mwanzoni mwa mwaka huu kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki—Lakini mpaka hivi sasa tangu njama za kuengua wapinzani na kuvuruga uchaguzi ili CCM ipate ushindi wa mezani inaonyesha namna kauli kutoka kwa viongozi wa CCM jinsi zisivyo za kweli

C) Kila kituo cha kampeni utakachokwenda anza kupre-empt na kuneutralize Talk points za CCM
1. Tafuta rebuttal nzuri sana ya Ishubya SGR hii usipinge ujenzi wake, pinga namna inavyojengwa, tafuta data za mikopo ya ujenzi wa reli hii na itaavyowatia umasikini watoto wetu kwa sababu ya deni la Taifa kupaa sana. Waonyeshe wananchi kuwa unaunga mkono ujenzi wa SGR ila kwa mpango mbadala (chukua ule mpango wa ACT wazalendo wa kujenga SGR kupitia PPP), na pia mataaluma ya reli tunaagiza nje, tunapeleka mabilioni ya dola nje badala ya kuboresha kwanza Liganga na mchuchuma ili chuma chetu cha ndani ndo kijenge mataaluma hayo, ili pesa hiyo ndefu na ajira zibaki ndani badala ya kuwapelekea wajapan dola hizo na ajira kwao

2. Kuhusu Stieglers, Usiupinge mradi bali pia kosoa namna ya ujenzi wa mradi huo, tafuta data unajengwaje, wananchi wananufaikaje, je kuna technology transfer au tunaishia kuwa wabeba zege na mafundi mchundo tu?. Waambie wananchi kuwa ukiacha Stieglers wewe utajenga Vinu vingine vya umeme kwa kutumia gesi ya Mtwara, umeme utakaokuwa mwingi kuliko utakaozalishwa na Bwawa la Stieglers. Stieglers itazalisha around Megawatts 2000 na ushehe, wewe plan yako ionyeshe utaleta umeme wa gesi mkubwa mara tatu ya huo

3. Kuhusu ndege, hiyo endelea kuponda, piga spana kwelikweli, ni mradi feki

4. Kuhusu kujenga uwanja wa ndege Chato, yaani hii usiiache kila mahali, piga spana, piga nyundo, siliba kwelikweli

C). Kwenye kutafuta kura kutoka kwa makundi maalum ya kijamii

1. Kwa waislamu, tumia kauli indirectly kuwa "Sitoteua watu kwa wingi kuliko wangine kwa sababu ni wa imani yangu bali nitateua kwa vigezo na vigezo ninavyovitska vipo kwa watu wa imani zote—Hapa utakuwa umemchapa Jiwe konzi moja nzito mno na Waislamu watakuelewa sana maana teuzi za Jiwe zinanuka udini mno na waislamu linawachukiza sana hilo

2)Endelea kuwasemea Masheikh waislamu, Jana umefanya kazi nzuri sana Arusha kwa kuwasemea Masheikh 70 wa arusha walioko ndani.
Pia endelea kuwasemea Masheikh wa Zanzibar (Usitumie neno Masheikh wa uamsho, hilo neno ni divisive, Tumia tu neno Viongozi wa dini ya kiislamu walioko jela), Wakumbushe waislamu kuwa Magufuli amrshasamehe wafungwa wa kila aina wakiwemo waliofungwa kwa ubakaji lakini anaona tabu kuwaachia Masheikh

3)Kundi la wanawake, wakumbushe wananchi jinsi Magufuli alivyoteua wanawake wachache mno katika serikali yake kulingsnisha na Kikwete, hii itasaidia kuneutralize soft power ya uwepo wa makamu wa rais mwanamke katika tiketi yake.
Umefanya kazi nzuri kumsiliba Maguful kwa kauli zake tata juu ya wanawake, kauli ile ya jogoo usiiache, endelea kupiga spana, kauli ile ya kupiga mashangazi endelea kupiga nyundo, kauli.

Endelea kuwakumbusha wanawake kuwa mwaka 2015 Msgufuli aliwaahidi kuwatua ndoo kichwani, yaani akimaanisha kuwaletea maji. Lakini badala ya kuwaletea maji kwa kasi ya kutosha yeye anachukua pesa ananunulia ndege na kujenga uwanja wa ndege Chato

E. Endelea kuwakumbusha wananchi juu ya Ufisadi

Ishu ya Trilion 1.5 zisizo na maelezo yenye mashiko bado ipo kwenye kumbukumbu za wananchi, japo waliunda kamati ya kuwasafisha, lakini maelezo yao hayana mashiko, Endelea kuwakumbusha wananchi juu ya utata wa Trilion 1. 5
Usisahau kuwakumbusha wananchi Jinsi CAG Assad alivyotimuliwa kwa kusimamia taaluma yake ya uhasibu na pia jinsi manunuzibya ndege yasivyokaguliwa kutokana na Jiwe kuweka ishu za ndege chinibya ofisi ya rais ambayo haikaguliwi na CAG

F. Usisahau ishu ya Maji na Kilimo
Maji bado ni tatizo kubwa, hili umepwaya kidogo, hujaligusia kabisa katika hotuba zako
Pia Kilimo hujakizungumza in details, tafuta mpango mkakati wa kuuza sera zako za kilimo kwa wananchi, waambie wwnanchi serikali yako itakavyowatafutia soko la mazao yao kupitia balozi zilizo nje. Badala ya mabalozi kukaa huko nje na kuuza sura, waanze sasa diplomasia ya kiuchumi ikiwemo kuwatafutia wakulima wetu masoko ya mazao yao ya kilimo.

G. Usiache hata kidogo kuwakumbusha wananchi magumu ya kiuchumi waliyopitia, uwe unawauliza kwenye kia mkutano wako, Je wako tayari kuendelea na mifuko iliyokauka kwa miaka mingine mitano?. Waulize wananchi je bado wanataka kuendelea na vyuma kukaza?. Waulize wananchi kuwa wako tayari kuendelea kukamuliwa na trafiki buku tano tano ili zikang'arishe viatu vya Trafiki?

H. Lissu baba, wakumbushe wananchi juu ya adha za faini ya tochi za Trafiki —Waambie wananchi kuwa hutogeuza tochi chanzo cha mapato, bali utaongeza hata speed limit kwenye barabara kuwa 80 hadi 100 kulingana na mahali husika, badala ya 50 hata sehemu zilizowazi kabisa.

Aisee kaka Lissu, Ukiendelea kumwaga sera zako ulizoanza kumwaga kisha ukaongezea na hizi CCM watatafutana!

Piga Spana kaka
Kweli Kabisa, inabidi amzibe Magufuli mdomo...kunadi sera mpya za Chadema ni kupoteza muda, inatosha kumpiga Magufuli kwenye makosa yake, na mauongo yake
 
Hahaha angekuwa na hiyo intelligence usingehitaji kumshauri mgombea Upinzani vitu rahisi namna hiyo, yeye mtaji wake ni kama 50 Cent, kupigwa risasi, baasi!
 
Kuna mikoa ambayo lazima tumuulize JO POMBE anaendaje..

1. KAGERA
Aliwaambia hakuleta tetemeko.
Lissu ukifika huku mwaga sera, halafu waulize ikiwa aliwaacha na kuwananga hivyo, tena alikwapua na hela za michango..

2. MTWARA, LINDI.
Ishu ya korosho inawaumiza mpaka leo.
Mwaga sera, halafu waambie CHADEMA haitotumia jeshi au polisi kuingilia biashara hiyo, wanunuzi kutoka nje watakaribishwa kwa uhuru mpate bei nzuri.

3. Kule nchi ya Tanzania Visiwani.
Anaenda kuwaambia nn?

4. Zipo wilaya kama
- Butiama ujenzi wa barabara ya Arusha tangu akiwa waziri haujakamilika, kisa imepewa kampuni yake ya MAYANGA.

- KAKONKO, KASULU, KIBONDO
Kote huko barabara haikamiliki kisa kampuni yake ndo inajenga.
Wanajenga leo, kesho wanafumua.


N.k
 
CCM Wala hatuna kazi ya sijui kutafuta takwimu Wala.Popote tunapokuwa kazi yetu Ndogo tu kuwaambia wananchi mwenye macho haambiwi tazama

Barabara hiyo mpya mnaiona hamuioki wanajibu tunaiona.Kazi ya CCM hiyo

Hospital mpya hiyo mnaiona hamuioki wanasema tunaiona .Kazi ya CCM hiyo

Huduma nzuri ofisi za serikali mnaziona hamuziomi? Tunaziona .Kazi ya CCM hiyo

CCM hatuhitaji kuwapa lecture ya vitu vya jutunga Kama Chadema sababu they have nothing to show of their own !!!

Watu hawahitaji maelezo mareeefu !!! Wanajua uongo

Watu wanafurika mikutano ya CCM kwenda kwanza kuipongeza kwa iliyofanya na pili kusikiliza kingine kipi wanaenda fanyiwa

Hawaendi tu kusikiliza Kama kwenye mikutano ya Upinzani
 
Kunadi sera ni pamoja na kuonyesha mapungufu, kutokutosha kwa mpinzani wako kisha ukawashawishi wananchi jinsi wewe unavyotosha kuwazidi
Tangu 1995 njia hii imefanywa na wapinzani wote lkn haikuwai kuzaa mtunda. Nyie watoto wadogo ni bora kukaa kimya hamjui tunatoka wapi tunakwenda wapi.
 
Kunadi sera ni pamoja na kuonyesha mapungufu, kutokutosha kwa mpinzani wako kisha ukawashawishi wananchi jinsi wewe unavyotosha kuwazidi
Wala sio strategy sahihi kumponda mke wa mwenzio kuwa Ni Malaya hakumfanyi mkeo Malaya kuwa mtakatifu

Ndio maana kwenye interview mfano waombaji walioomba kazi wako elfu mbili Wakati nafasi Ni moja swali ambalo huwa gumu kulijibu Ni kwa Nini tukuchukue were tuwaache wengine elfu moja Mia Tisa tisini na Tisa? Huwezi kuelezea udhaifu wao kujenga hoja yako

Unajikita only kwenye strengh zako tu ndio maana CCM kampeni zetu Zina concentrate kwenye strength zetu tu hatuhangaiki na weakness za upinzani after all they are weak why waste time kueleza weakness ya mtu ambaye Kila mtu anamwoma weak? Mfano mtu ni kiwete Huwezi Simama jukwaani masaa unaeleza kuwa huyo mtu Ni kiwete !! Unapotezea muda watu
 
Missile of the Nation,
Hiyo itakuwa siyo mkutano ya kunadi sera bali kukumbushana yaliyopita!
Tulia Jo...
Screenshot_20200901-054243.jpg
 
Pia awakumbushe wananchi jinsi watoto waliosoma private wanavyonyimwa mikopo na bodi ya mikopo ...pia wafanyakazi walivyonyimwa kupandishwa madaraja hasa walimu
 
Mrema hana IQ ya Lissu

2015 CCM ilichapwa asubuhi na mapema
Kwahiyo Dr. SILAA, EDWARD nao walikuwa vilaza? Lisu naye alikuwepo pia.

Mbinu ya kunadi mapungufu imetumika miaka 25 na imeprove kufeli sana. Endelee hivyo hivyo bila kutangaza sera mtavuna makapi.

Hata hivyo kwa katiba yetu, wapinzani wataendelea kusindikiza. Vipi walioenguliwa wameisharudishwa?
 
Ninyi kweli "weupe", badala ya kumuhimiza Lissu afafanue ilani yake kinaga ubaga watu waelewe Chadema inaweza kufanya nini tofauti na kilichokwisha fanywa na kinatachotarajiwa kufanywa CCM, bado mnabaki kupiga kelele ambazo watu hawana taimu nazo. Mwambie Lissu aWaeleze wananchi ninamna gani ataifumua TRA na kisha kuleta mbadala wake utakao fanya kazi bora zaidi ya TRA ya sasa. Pia aeleza namna atakavyolipa fidia kutoka " mfukoni mwake"!
 
Back
Top Bottom