Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Ngoja Kwanza tuangalie Afya za hawa Wasanii waliopata Ajali mbaya leo zinaendeleaje, Israeli akiwataka tutafanya akiwasamehe wala hatutofanya.

Wale wasanii walikuwa wakifanya mambo ya laana.
 
Umekosa kabisa kazi ya kufanya maana 2020 Watanzania tunaenda kumchagua tena Dr Magufuli ili amalize maendeleo Kwa watanzania
 
Alisema yeye kaletwa kwenye mkutano kw nguvu ili kuongeza idadi ya mahudhurio pia kasema yeye hana cha kusema kuhusu uchaguzi huu ila analazimishwa kuongea.

Nilipata hicho ki clip...nasikia kuna ingine kuna mama simiyu kamuumbua mheshimiwa na maneno makali bado sijaipata
 


Nawasikia watu mara oh Lisu azungumzie sera, atafanya nini katika nyanja mbali mbali za kijamii etc! All this is rubbish kama hakuna UHURU! Lissu yuko sahihi, kitu cha kwanza ni ku- regain our FREEDOM IN ALL WALKS OF LIFE AMBAZO ZIMEVURUGWA/ ZIMEPOLWA NA UTAWALA WA AWAMU YA TANO! Haya ya sera na upuuzi wowote awe anarushia rushia tu!

Waamshe watu akili kuwa wanaonewa, wanadhulumiwa, wanateswa, wanapotezwa, wamenyang'anywa UHURU WAO na mengine. Baadaye rushia kidogo habari ya sera, atafanya nini wakimpa kura za kushinda.

Mandela na wenzake wapigania uhuru wote duniani, walipigania UHURU wao kwanza, kuhamasisha watu wajitambue kuwa hawako HURU, haya ya sera yalikuwa kidogo katika harakati zao!
 
Hakika huyu ni mwiba mchungu kwa CCM ,kila anapo pita anamwaga sumu kali, mtindo wake wa kujinadi Ni hatari anaanza kwa kuwakumbusha watanzania maumivu waliyo yapitia kwa miaka hii mitano ,maumivu ambayo ukiyafuatia yanagusa karibu maisha ya wananchi wote, akimaliza Hilo ndo anaingia kwenye kauli mbiu inayotumiwa na chama chake, UHURU, HAKI, NA MAENDELEO YA WATU.

Anafafanua jinsi wananchi wanavyo takiwa kuwa huru katika kutoa mawazo yao, anaelezea jinsi ambavyo wananchi wanavyo paswa kutendewa haki hasa katika maslahi yao ya kila siku, na mwisho anazungumzia juu ya maendeleo kuwa Ni kwa jinsi gani inavyo paswa kuinua na kukuza maisha ya mwananchi. Na mwisho anakuja na na sera mbadala jinsi gani chama chake Kita tenda ili kubadili maisha ya mtanzania.

Mambo ambayo ameyatilia mkazo ni:
1: Mfumo waelimu yetu kuwa ni mbovu.
2: Bima ya Afya kwa wananchi wote.
3: Kurejesha mahusiano na urafiki kwa mataifa.
4: Kuangalia na kuurekebisha Mfumo wetu wa Kodi.
5: Kufutilia mbali vitambulisho wanavyo uziwa wamachinga.
6: ujenzi wa miundo mbinu, na katika hili anasisitiza kuwa huu ni wajibu wa Serikali zote zilizo ktk madaraka hulitenda.
7: Kuinua Pato la taifa sambamba na uchumi wa mwananchi wa mwananchi wa kawaida. Nk.

Na kwa vile sasa Kisha maliza kungukia Kanda zote, amehamia kwenye miji, wilaya na vitongoji.

Pamoja na kuwa CCM wanajopo kubwa la wanao shiriki kampeni wakizunguka karibu nchi nzima, lakini bado Tundu amewameza wote ktk kampeni za mwaka huu kwa kufuatiliwa na maelfu ya wananchi.

Na kwa hili naona jinsi ambavyo ana ivunjavunja CCM na kuifutilia mbali.
 
Hivi Bunge la Tanzania linakubaliana na agenda za Magufuli au lina pitisha miswaada ya sheria?
Bunge ni kama sehem ya nguo ya Magu siku hizi, halisimami lenyewe. Na endapo akirudi tena ikulu, tutarajie mengi ya ajabu.
 
Kwa uandishi huu kama ndio barua yakuomba kazi haisomwi utaikuta kwenye shimo la taka.
 
Kwa uandishi huu kama ndio barua yakuomba kazi haisomwi utaikuta kwenye shimo la taka.
Wewe jibu hoja kila Mara nawaambia suala LA kuandika ni kipaji cha mtu angalia content,ndio maana waafrika mtazidi kuwa wa hivyo hivyo,unaangalia vitu vidogo sana,kuandika na kusoma ni vitu vya kufundishwa lakini upeo wa MTU haufundishwi ni mungu alivyoumba,hoja kuwa nimeandijaje hivyo haitakusaidia ndio maana kuna MTU ni muandisi nzuri,mwingine ni muongeaji mzuri mwingine ni mtendaji mzuri sasa kwa vile wewe ni zwazwa na tobolisu mwenzio ndio maana mnajadili MTU kujua kuongea lugha ya malkia ni usomi au kujua kupangilia maneno ni kujua jambo,lugha ni kiunganishi ndio maana kuwa viziwi na mabubu na bado wanawasiliana hivyo jaribu kusoma nilichoandika ukielewe kuna mengine ni ya typing inarusha lakini hoja imejibiwa dili na hill choko wewe.
 
Du.....! Kuna mtu anaweza summarize hii porojo!labda Kuna la element la point!
 
Lissu tafadhali ongelea na figisu suala la FastJet, naamini uchwara atakurupuka na kudakia ili ndege zirudi angani... tumemisi 'flights' za bei chee!
 
Wanaccm wengi wanafuatilia lissu, kwa kificho, mh. Mmoja tulimfumania chooni anasikilza hotoba ya raisi Tundu lisu
 
Back
Top Bottom