Na: Mh Tundu Lissu

Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu. Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara. Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo.

Haijarudisha hata senti moja. Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja.

Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja. Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja. Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani.

Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa. Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao.

Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.
 
Tatizo kuna wafanyakazi baadhi ni wajinga tu wanashindwa kuelewa kuwa kuna maisha baada ya kuustaafu yani kutwa nzima kushabikia mbogamboga wakiishastaafu ndio uwa akili zinawarudi kwa muda ila wanashindwa kutambua mchawi wa pesa zao na maendeleo yao ni CCM.
 
Anatakiwa kuahidi commitment ya serikali yake kutathimini deni la serikali kwenye mifuko ya jamii na kuwa baada ya hapo serikali yake itahakikisha deni lote linalipwa kwa kipindi ambacho wataona inafaa.

Anatakiwa pia kuahidi kuwa wataweka wataalam ambao watatathimini miradi yote ya mifuko ya jamii yakiwemo majengo kama yanaendeshwa kwa faida na kuona uwezekano wa aidha kuibadili matumizi yake au kuiuza ili kuondokana na gharama za uendeshaji. Sambamaba na hilo, watasimamisha uwekezaji mpya wa miradi mpaka marekebisho ya mifuko yakamilike na kuona kuwa inarudisha uwezo wake wa kulipa mafao ya wastaafu
 
Imethibitika kuwa kote ilipotumika hii sera imeleta matokeo chanya kwa wakazi wa maeneo husika Kisha kwa taifa zima.

Hii Ni kurudisha mamlaka kwa wananchi juu ya matumizi ya rasilimali zinazo patikana katika maeneo yao kwa ajili ya maendeleo.

Mfano gesi ya mtwara ilipaswa watu wa mtwara wawe na maamuzi ya jinsi ya kuitumia Kwanza kwa manufaa na Maendeleo ya Wana mtwara Kisha sehemu nyingine inakwenda ktk maeneo mengine ya nchi.

Kadhalika dhahabu ya mikoa ya Shinyanga Geita, Mara, nk.
Kahawa ya Kagera, Kilimanjaro hivyo hivyo, tumbaku ya Tabora na Songea.
Tanzanite ya Mererani, nk.

Huu Ni utaratubu ambao ukitumika utapunguza tatizo la umaskini na kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo husika. Tofauti na sasa ambapo maamuzi yote yanatoka serikali kuu, na mbaya zaidi Ni kuto wajali wakaazi wa maeneo yenye kuzalisha utajiri ndani ya nchi.
 
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu. Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara. Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika. Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara.

Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja. Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao.

Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa. Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.
 
Kabisa mimi sitakaa niipigie ccm kura hata mgombea awe mzuri vipi kutokana na hii kadhia ya mafao yangu kupangiwa lini nichukue yaani kila kona ni shida wakulima shida wafanyakazi shida
 
Msichagua watu wasiomanika, msichague watu watakaokuja kutawala kwa matakwa ya watu wengine. Na si ajabu zikarudishwa hapa lockdown wakati Mungu ameshaimaliza.

Mwisho wa kunukuu.
 
Ela yangu mpaka leo sijaipata nayo dai katika mfuko mmoja wapo , ela ya ukosefu wa ajira. Unaelekea kuisha mwaka sasa.
 
Nimefuatilia kwa karibu mikutano ya kampeni ya Chadema na nimegundua Chadema hawainadi kabisa ilani ya uchaguzi pamoja na sera za chama chao.

Wanachofanya wagombea wa Chadema akiwemo Tundu Lisu ni kuiuliza serikali maswali na kisha kujijibu.
Tunaofuatilia mikutano yenu tunataka kusikia mkinadi sera na kutueleza mtatufanyia nini kama wanavyofanya wagombea wenzenu wa CCM.

Badilikeni makamanda.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mikutano yao imekuwa sehemu ya bunge live, kuhoji serkali kwa maswali ya papo kwa papo.
 
Mwanzo bwashee mlisema hatagombea ataenguliwa, mkaja mkasema hawana sera wanaongea matusi tu, sasa mnasema wamejikita kuwauliza maswali serekali, kwani wewe hujui kama ndio kazi ya chama cha upinzani hiyo bwashee. Moja wapo ya kazi zao ni kuihakiki serekali, kuionesha serekali kuwa haijafanya kitu mbele ya wananchi. Ni jukumu la upinzani kuibana serekali kwa maswali na ni jukumu la serekali kuyajibu kwa ufasaha sio kwa hasira.
 
Mlikuwa mmezoeshwa “lollypops”, sasa vya kutafuna hamuwezi tena! Miaka mitano ya serikali kutokuulizwa maswali imepita Buashee. Tulia sindano ipenye kunako.
 
Mtu ambaye ameumizwa kwa sababu alizozitaja kua ni mambo ya kisiasa, kisha wakatitokeza watu kwenye mitandao ya kijamii wakiwalaumu wasiojulikana kwa kushindwa kumuondoa, bado amerudi kwenye ardhi yake, ameamua kuifia ardhi yake. Huyu ni mzalendo anayepaswa kuungwa mkono na watanzania wote, tumpe nchini mifumo yote ya kiutawala ya mkoloni ifimuliwe wananchi waifaidi nchi yao.

AMEANZA KULITUMIKIA TAIFA MUDA MREFU SANA?
Wakati huyu mtukufu wetu akipiga makofi bungeni kupongeza RICHMOND, IPTL, ESCROW,EPA nk, Tundu Lissu wakati huo analala mahabusu za polisi kwa tuhuma za uchochezi kwa kuwatetea wananchi walioporwa ardhi zao huko Kisasida Singida bila kuwadai chochote, alilala polisi mgodi wa Nyamongo kuwatetea wananchi wasiokua na utetezi kisha wakashindwa.
Mtu kama huyu utakosaje kumuita mzalendo.

CCM IMEJAWA HOFU YA LISSU( LISSUPHOBIA)
Wanachofanya CCM siyo kwamba wanamchukia Lissu, wanaelewa kabisa kua mifumo ya utawala ya nchi yetu ni mibovu ikiwa ni pamoja na katiba mbovu, kwahiyo wanajua akiingia Lissu hakuna jiwe Litakalosalia. CCM sasa haipambani kutetea shida za wananchi, inapambana kumzuia Lissu asiingie Ikulu ili walinde maslahi yao na familia zao.
 
Tundu
Mwinyi
Mkapa ..

Jakaya
Kawawa
Makamba
Nyerere.

Umegundua nini kwenye haya majina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…