Mtu ambaye ameumizwa kwa sababu alizozitaja kua ni mambo ya kisiasa, kisha wakatitokeza watu kwenye mitandao ya kijamii wakiwalaumu wasiojulikana kwa kushindwa kumuondoa, bado amerudi kwenye ardhi yake, ameamua kuifia ardhi yake. Huyu ni mzalendo anayepaswa kuungwa mkono na watanzania wote, tumpe nchini mifumo yote ya kiutawala ya mkoloni ifimuliwe wananchi waifaidi nchi yao.
AMEANZA KULITUMIKIA TAIFA MUDA MREFU SANA?
Wakati huyu mtukufu wetu akipiga makofi bungeni kupongeza RICHMOND, IPTL, ESCROW,EPA nk, Tundu Lissu wakati huo analala mahabusu za polisi kwa tuhuma za uchochezi kwa kuwatetea wananchi walioporwa ardhi zao huko Kisasida Singida bila kuwadai chochote, alilala polisi mgodi wa Nyamongo kuwatetea wananchi wasiokua na utetezi kisha wakashindwa.
Mtu kama huyu utakosaje kumuita mzalendo.
CCM IMEJAWA HOFU YA LISSU( LISSUPHOBIA)
Wanachofanya CCM siyo kwamba wanamchukia Lissu, wanaelewa kabisa kua mifumo ya utawala ya nchi yetu ni mibovu ikiwa ni pamoja na katiba mbovu, kwahiyo wanajua akiingia Lissu hakuna jiwe Litakalosalia. CCM sasa haipambani kutetea shida za wananchi, inapambana kumzuia Lissu asiingie Ikulu ili walinde maslahi yao na familia zao.