Kwa hiyo wewe unaona afadhali Wachina wapewe kuliko wa Tanzania (wazawa)? You are a sale-out
 
Kamanda Asiyechoka,

"Eleza jinsi wachina wanavyopewa kandarasi ambazo hata wazawa wanaweza kuzifanya, sasa mzunguko wa pesa haupo, sababu wakilipwa pesa zinaenda China. Ila wazawa hawapewi hizi kazi wakati wanao huo uwezo kuzifanya."
 
"Eleza jinsi wachina wanavyopewa kandarasi ambazo hata wazawa wanaweza kuzifanya,sasa mzunguko wa pesa haupo,sababu wakilipwa pesa zinaenda China. Ila wazawa hawapewi hizi kazi wakati wanao huo uwezo kuzifanya."
Mfano mdogo tu ni mradi wa DMDP, umeboresha barabara za mitaani Temeke. Mitaa ya uswahilini kama Yombo. Hizi ni za kumpa mchina ajenge badala ya mzawa?

Majengo mengi tu ya vituo vya afya yanajengwa na wachina. Unadhani mzawa hawezi kufanya hii kazi? Kisa ni ghorofa moja au mbili?

Pesa hizi zinalipwa wachina zinabaki hapa Tz?
 
Yote haya yamefanyika chini ya usimamizi wa Serikali dhaifu, dhalimu, za kijambazi, za CCM miaka yote. SASA CCM imebadilika lini? Huko tayari kwa lipi? Mbona unajikanyaga kijinga? Ondoa liCCM madarakani likafe Kama KANU tuingize new mentality and new philosophy.
 
Mama lishe gani ambae yuko hoi? Maana sikuiziii umeona mgambo wa kumwaga vyakula vya mama lishee??? Mama lishe sikuizi wanapika vyakula adi barabarani, wala hakuna wakuwaulizia ata kidogo. Acha uvivuuu fanya kaziiii.
 

Wewe endelea kutafakari. Kwani madiri unayoyasema mjomba wako Magu si ndiyo amayapaisha maradufu! Uwanja wa Chato siyo dili? Mayanga constructors siyo dili! Upotevu wa 1.5 trioni (sasa ni 2.4 trioni) siyo dili? Jesca kuwa DAS siyo upendeleo Kama zamani? Mawaziri wengi kutoka Geita siyo upendeleo? Mtoto wa Dada kuwa Paymaster General je? nk. nk. Kichwa chako kisiwe mzigo , kifikirishe. Wewe unasifu mambo ya kitoto ya mamalishe kuuza bagia na chai barabarani??!! Hivyo una akili wewe. Ndiyo kuendesha nchi hivyo? . Tatizo ni system zima imeoza. Futa hii Serikali tuanze upya. CCM imeshindwa na Magu wako ameiharibu zaidi.
 
Nani mmiliki wa mayanga contractors
 

Uwanja wa chato ni wa Watanzania wote hata wewe utatumia. Hiyo tirion 1.5 ilikuwa kiki ya zito kabwe ambayo imeshabumaa. Na yule mchezesha igizo la hizo tirion, amesha timuliwaaa. Kwa jpm hakuna madili tena, kwani yangekuwepo msingelilia mitandaoniiii.
 
Mwenye uchi siku zote huwa na papara,ndio maana hata wakijiunga na wenzao wao ndio hutaka top layer kwanza.
 
Ukitaka kujua Tundu lissu ni mgombea wa hovyo na anawakatisha tamaa bavicha,ni jinsi miongozo,ushauri na maelekezo yalivyo mengi humu kuliko kuwahi kutolewa kwa mgombea yoyote.

Inaonekana Tundu Lissu anatoka nyumbani amepanga kabisa kuongelea sera, lakini kwa kuwa hana sifa za urais, akifika jukwaani anapotea, anapandisha hasira anaanza kuelezea risasi na uwanja wa Chato.

Watu wanataka ugali yeye anaelezea uwanja wa Chato, kana kwamba chato sio Tanzania.
 
Hatari sana kwamba Mafisadi hawahatarishi usalama wa nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…