Hahaha nasikia hata Polepole na Bashiru wana mpango wa kumpigia kura Lisu wamechoka kutishwa kufukuzwa na Magufuli.
 
By the way wana ccm ,act,cuf,chadema na wengineo ni watz na ni ndugu taifa moja.Ugumu wa maisha,taabu na mateso ni kwa wote.
 
Bila kusahau wasira,ngereja,Lowasa na maige
 
Haswaaa 😊😊😊 miongoni mwao Ni hawa Tulia wewe😊😊😊😊😊 wenzako wankucheka unaharisha pekeako tu🤣🤣🤣
 

Attachments

  • VID_48221104_221141_428.mp4
    3.2 MB
Mimi pia ni mccm. Kura yangu siipeleki lumumba katu.
 
Haiingia akilini tuna Bandari ila wafanya biashara wanachukua nguo Uganda nchi inayo tegemea bandari ya Mombasa na Dar es salaam.

Burundi hawana bandari ila magari kwao ni cheap sana kuliko Tanzania.

Hii inapaswa kuongelewa pia make tuna kodi za kukomoana sana
 
Mhe. Lissu salaam, pole na majukumu na mizungunguko yako ya kunadi sera zinazotugusa sie tulio wanyonge haswa. Binafsi nimekuwa nikikufutilia kwa karibu kampeni zako popote kwa njia ya mtandao na agharabu niliwahi kuhudhuria kwenye uzinduzi wa kampeni moja mkoa wa nyanda za juu kusini, hakika Mungu akulinde.

Kuna mambo mengi yakuleta matumaini umekuwa ukiyaeleza vizuri namna utakavyo yashughulkia kwa kweli inatia moyo. Lakini kuna jambo moja bado hujaliweka wazi sana namna utakavyo shughulika nalo na hili unalijua lina kundi kubwa la watu na unalijua vizuri.

Binafsi pia ningependa uliongee kila pahala unapokwenda kunadi sera (nitalieza). Kwakifupi niorodheshe mambo unayoyaeleza vizuri na hayana shaka ili uliongeze na hilo liwe miongoni mwa haya(msomaji waweza ongeza ambayo nimesahau) .

1. Kila mtanzania kumpatia bima ya afya
2.Kuongeza mishahara kwa watumishi(mujibu wa sheria)
3. Kulipa malimbikizo kwa watumishi.
4. Kurudisha fao la kujitoa
5. Kupunguza makato bodi ya mikopo mpaka 3% ya awali
6. Kutoa mikopo kwa waombaji/ wanafunzi wote elimu ya juu.
7. Kulipa fidia kwa wahanga waliobomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara na kuwafariji wahanga wa tetemeko Kagera.
8. Kuondoa kitambulisho cha ujasiliamali kwa machinga na wengineo
9. Kuwapatia watanzania katiba mpya(ya Jaji Warioba).
10. Kurudisha ardhi iliyopokwa kwa wananchi.
11. Kuwatoa magerezani Mashehe wa uamsho(na wanaharakati waliobambikiwa kesi).
12. Kuunda tume ya maridhiano kwa viongozi waliojihusisha kunyanyasa raia bila makosa ukiwemo wewe, kuuweka bayana wa mambo hayo na sababu ya kufanyika kwake na kisha kusamehana.
13. Kuondoa vikwazo kwa wakulima (kundoa kodi za magetini, kuwa na soko huru na upatikanaji rahisi wa pembejeo za kilimo pamoja na bei zake).
14. Kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara(kuondoa kodi mpaka kufika 10%, kuifumua upya TRA, nk).
15. Kuweka mazingira safi ya Uwekezaji ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.
16. Kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kumpa maarifa mwanafunzi na sio kuongeza ufaulu tu bila kuwa na maarifa. (Kuaandaa wasomi watakaoajirika popote duniani na kuwa katika soko la ushindani).
17. Kuzipa nafasi sekta binafsi kuratibu shughuli zao kwa uhuru na kuifanya serikali kuwa msimamizi na kuzipa mazingira safi ya shughuli zao.
18. Kuwa na serikali za majimbo na viongozi wake kupatikana kwa kuchaguliwa ama kuondolewa na wananchi(kurudisha nguvu na mamlaka kwa wananchi).
19. Kulinda na kutetea haki, utu, na uhuru wa kila raia.
20. Kujenga uhusiano mzuri na mataifa mengine(Diplomacy Restoration)ambayo pengine yamezorota hivi karibuni.
21. Kuondoa laana ya rasilimali(wananchi kutobugudhiwa/kubezwa kwa rasilimali zinazopatikana maeneo waliopo/yanaowazunguka). Raia kuwa wanufaika kwa rasilimali zinazopatikana mahala walipo.
22. Kurudisha uhuru wa vyombo vya habari (kuondoa sheria kandamizi za utoa aupokeaji wa habari)
23. Kuondoa kinga ya viongozi na kupunguza mamlaka ya Rais. (Kuweza kushtakiwa akifanya makosa). nk nk

Kwa uchache hayo ndiyo nayasikia mara nyingi na yanatugusa mojakwamoja. Sasa hitaji langu nitajikita kwenye namba 16 kwa sababu kwa namna moja ama nyingine vijana na wazazi wameathiriwa vibaya mno na hili.

MFUMO WA ELIMU na AJIRA kwa VIJANA
------------------------------------------------------
Mh. T. A. Lissu kama unavyojua mfumo wa elimu umekuwa ukituandaa vijana kuwa tegemezi(dependents) yaani soma, faulu, na uandaliwe ajira. Mfumo huu hautupi uwezo wa maarifa na kisha kupambana na mazingira bali uajiriwe baada ya kuhitimu. Hiki ndicho kinachogharimu wasomi wengi na kufifisha matumaini kwa wazazi wanaosomesha vijana wao. Nimeridhika na namna unavyotaka sekta binafsi zipunguze tatizo la ajira lakini ujue kuna kundi lililomaliza vyuo toka 2015-2020 almost 6years halina ajira rasmi na liliandaliwa na mfumo huo tegemezi wa elimu.

Hivyo basi ningependa katika kampeni zako ungeliongelea katika kila mkutano wa kampeni ipi mipango mikakati ya dharura ya kushughulika na kundi hili kabla ya kuanza na mfumo mpya wa elimu. Kumbuka hawa vijana ni kundi kubwa wao na wazazi/walezi wao wanataka kujua hatma yao na namna utawafanya wawe kwenye ajira rasmi.

Serikali ya sasa nikama haina mipango yoyote juu ya hili na ndio maana kumekuwa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa miaka hii mitano. Hawa ni vijana waliosomeshwa na wazazi maskini kwa kuuza mazao yao, mali zao, mashamba, mifugo ili tuu wapate elimu.

Katika kundi hili ni wachache wanaopatiwa ajira rasmi agharabu kwa wale wenye ndugu walio na nafasi kubwa serkalini ila the rest wapo mitaani. Kwa heshima yako naomba utoe mwongozo kwa vijana, wazazi au walezi kila mkutano wako wa kampeni maana ni tatizo la nchi nzima.
Asante na kila la kheri katika mapambano yako. (Nashuku katika kampeni zako jana 27/09/2020 Musoma umeanza kuliongelea kiundani, ningependa liwe ni endelevu kwa kila mkutano wako).
Naomba kuwasilisha.
 
Suala la ulinzi wakura ni wajibu na jukumu la kila mpenda Haki na Taifa letu la Tanzania.Tusimwachie Mh.Lissu na CHADEMA peke yao.
Tumefurahishwa sana uungwaji mkono mkubwa wa Lissu kila kona ya nchi. Kwa kweli Lissu ameshashinda kikubwa ni kudhibiti wizi wa kura tu.
 
Chadema wa jf kwenye kujifariji mpovizuri.
tukutane October 28 ndo mtajua watanzania hawana utani kwenye sanduku la kura.
Nanukuu mwasilishaji wa huu uzi kipandee...

"Hoja ya magufuri imebaki kuwa ni watu wajiajiri wakati yeye mtoto wake Jesca amemwajiri wizara ya mambo ya nje, mwingine amempa RAS iringa .hao walishindwa kujiajiri hadi awaajiri. Watoto wa wanyonge ndio wanaohimizwa kujiajiri"

Mama angu mzazi alinambia usimpigie kura Magufuli 2020

Anaenda mbali kanambia ametunza kweny kabati degree 3 za watoto wake

Leo hii mtoto wa Raisi binti mdogo wa Raisi anapewa kazi wizara ya Mambo ya nje....

Ukiwa mtoto wa Raisi Ni mfano Hai KWA vijana kuhusu kujiajiri....maana
hawezi kulalamika mtaji
hao ndio walikuwa watu wa kutengeneza fursa KWA vijana wengine wajiajiri

Mtu mwenye akili timamu ataelewa na anaelewa uchungu

Tena WAZAZI walio somesha watoto wao na Still... wapo wapo nyumbani uta waambia nini?
Wamekosa hata Kazi ya upolisi au magereza au JW
Wamepelekwa huko Jkt kupotezewa muda wao wa MIAKA miwili

Hao walimu wa BAED wangepelekwa primary school wakafundishe ELIMU yetu ingepanda thamani.

KINACHO FANYIKA MNYONGE WA NCHI HII ANAZIDI ZOHOFISHWA AWE MNYONGE ZAID NA ZAID
 
atilie mkazo kuhusu FAO la kujitoa.... kazi nyingi sector binafsi ni kazi ya mikataba.. mkataba unapoishi tunatamani tuchukue pesa zetu tukajiajili wao wanazikatilia ni kuendelea kutufanya wanachi kuwa masikini ili hali wanapiga pambio la vijana kujiajili. maneno na vitendo haviendani.
 
Lissu atakuwa rais wa Twitter na Facebook sio Tanzania ambayo mwasisi wake ni hayati Julius Nyerere.

Hawezi kumkejeli mwasisi wa taifa halafu unataka uliongoze taifa hilo hilo.
 
Nampenda lissu kwa kutetea haki. Tunapaswa kuwa na Rais mpenda haki.Mtanzania yeyote ana haki zake ziheshimiwe.
Mkuu mwogope mwanasiasa anapokuwa jukwaani.
Wote wakiwa hapo huwa na sifa moja...waongo!
28/10 kafanye yako kwa kufariji nafsi yako na urudi kupambani kuihudumia familia yako. Usimtegemea mwanasiasa kwa maneno yake matamu jukwaani.
 
Pia, Utamaduni mpya uliasisiwa na CCM MPYA nchini, yaani utekaji wa watu na ubambikaji wa kesi zisizo na dhamana kwa wananchi wasio na hatia
 
HOJA HIZO ZINAWAGUSA WATANZANIA WENGI WANAONYANYASWA NA WERIKALI ONEVU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…