Mungu mkuu amuongezee maisha marefu mh Tundu Lissu. Ni jasiri mmoja aliyejitoa mhanga kuwatetea mamilioni walioumizwa katika kipindi cha miaka mitano. Inahitaji roho ya chuma kufanya anayofanya Mheshimiwa Tundu Lissu. Pamoja na madhila yote aliyopata, jemedari huyu hajakata tamaa kuendeleza harakati za kuhakikisha misingi ya haki na utawala bora inatamalaki katika nchi yetu pendwa ya Tanzania.
Rai yangu kwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani, wabunge wa CHADEMA na wapenda haki wote wazidi kumuunga mkono Mteule huyu wa Mungu ili ukweli wa kurejesha haki ukubaliwe na watawala madhalimu wa awamu hii ya tano.
MUNGU MBARIKI TUNDU LISSU, MUNGU UBARIKI UCHAGUZI MKUU, MUNGU WEZESHA USHINDI KWA TUNDU LISSU.