Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Nimesikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Tundu Lissu kwenye Kampeni zake mkoani Mara Hakika hakamatiki!!
Ili kumshinda Lissu kwenye Sanduku la kura itabidi CCM waibe vile hawajawahi kuiba tangu mfumo wa multipartism uanze.....!!!

Ujinga mtupu! Unatanguliza kuibiwa kura ili iweje? Lissu tumemfahamu leo? Tanzania tunataka mtendaji, kama ni maneno alishayasema miaka yote, yametusaidia nini? Hoja hoja to where? Hii siyo dunia ya hoja. Tunataka CHADEMA na CCM watueleze watakachofanya siyo hoja utadhani ni darasa la kufundisha wanasheria. Kila siku ni ahadi za kurekebisha sheria! Too cheap!

Mpiga kura kama wewe ni mtu dhaifu tu, ndo maana nasema CHADEMA munashikilia kuishinda CCM badala ya kuhangaika na hoja za matatizo ya wa-TZ. Unavyoona Lissu akishinda hata CHADEMA itashinda? au huoni tofauti ya hayo mawili
 
Kete muhimu kwa ushindi wa Lissu

1. Fao la kujitoa
2. Makato ya HESLB
3. Masoko ya mazao ya biashara na chakula
4. Haki za watumishi wa umma
5. Vyeti feki na wafanyakazi hewa
6. Bomoabomoa
7. Uhuru wa bunge na mahakama
8. Wafanyabiashara
9. Kesi za kubambikia
10. Ubaguzi, ubabe, na ukatili
11. Utekaji na mauaji
12. Ukali wa maisha
13. Uminyaji wa haki na demokrasia
14. Mikataba ya siri ya madini, zabuni za sgr nk
15. Upotevu wa matilioni ya fedha
16. Ufisadi
17 . Kikokotoo cha pension ( kuanzia 2023)
18. Elimu bure kabisa
19. Miundo mbinu mibovu vijijini
20. Maji, umeme, na mawasiliano vijijini.
 
Lisu ndie mtetezi halisi wa wanyonge wasionewe, na sio yule miaka 5 tu kajenga kwao mahoteli na uwanja wa ndege akipewa kumi je.
 
Lisu Hana kashfa yeyeto hata nukta si ya wizi, ufisadi, udini, ukabila, ukanda, visasi.
Amewahi watoa gerezani watz 250 Tena bure waliobambikwa kesi waozee jela na mzee wa lupaso walipopinga kuporwa ardhi yao yenye madini Mwanza, shinyanga na Mara.
 
Amegusa mule mule kwenye shida za watz soon yule aliyewakana vitambulisho vya machinga ataiga
 
CCM kwa sababu ya wingi wao bungeni wamekua wakipisha sheria za kumkandamiza mtanzania huku wakijinani watetezi wa wanyonge mfano aslimia 15 za bodi ya mikopo, mafao ya wafanyakazi huo ni mwiba kwa wanyonge
 
NEC ya Mahera mteule wa Magufuli inaonekana haijitambui na imechanganyikiwa[emoji1787][emoji1787]
NEC Hawajui kuwa Wana-deal na Wakili MSOMI na nguli wa Sheria Tanzania.....!!!
Wameshaonesha wazi kuwa wana mpango wa kugushi matokeo. Kwao, Magufuli alishashinda na anangoja tu kutangazwa. Wanaogopa mtu mwingine anayesema ana uhakika wa kushinda na haki isipotendeka, hapatatosha, wanaona wazi kuwa tishio linawahusu. Ukweli ukiangalia kampeni za Lissu, ukisikiliza maoni ya Watz walio wengi, Lissu atashinda kwa kishindo. Hii inasumbua tume kwa kuwa hawako tayari kwa hilo. Watatangazaje mshindi asiye Magufuli?
 
Watanzania hawahawa wasiojielewa wanaoenda kuburudika show za bure kwenye mikutano ya ccm na matokeo yake ccm hujisifia nyomi?hawa ambao washamba wa magari ambao wanajazwa kwenye malori na kepelekwa kwenye mikutano ya ccm?

Hawa watu bado hawajajielewa hivyo hawawezi kuitoa ccm katika hali kama hiyo,mijitu inaenda kwenye kampeni ila ukiwahoji wakuelezee walichokielewa kwenye hizo kampeni hawaelewi kabisa yani wanajazana pale tu sababu wamekosa kazi za kufanya wakati huo.

Halafu mtu unakaa unaanza kufikiri watu kama hao ndio wataitoa ccm.
 
Watumishi wa umma Unajua wengi wamekuelewa ila hawawezi kujionyesha kwa sababu ya kulinda ajira zao.

Watumishi hao wa umma ni pamoja hawa wakurugenzi, wakuu wa wilaya pamoja na wakuu wa mikoa.

USHAURI:
Naomba sana katika kampeni zako hawa watu usiwatangazie UBAYA au KISASI kwa sababu tu ni wateule wa Rais , Bali uwaahidi utawasaidiaje kulinda ajira zao ukiwa Rais ukizingatia maisha yao yapo kwenye hizo ajira kwa maana kwamba wanasomesha, wanategemewa, wanasaidia ndugu na wazazi wao kupitia ajira hizo.

Kwahiyo katika kampeni zako hakikisha unajitahidi kutoa maneno ya faraja yanayo akisi hatma yao wewe utakapo kuwa Rais.

KUMBUKA : Kundi hili la watumishi wa umma wana mchango mkubwa sana kwenye ushindi wako wa Oktoba 28 , sio tu kukupigia kura , bali ni pamoja na kutenda HAKI katika uchaguzi huu.

Vinginevyo kama hawatapata hatma ya maisha yao watazilinda Ajira zao kwa gharama yoyote.
 
Inasikitisha Sana. Ila wakae wakijua siku zote ya kuwa nguvu ya umma inapoamua jambo daima huwa haishindwi hata mara moja. Jibuni hoja zake kama vile anavyozitoa hadharani. Hizo njama mnazompangia hazitafanikiwa.

Kama ni wivu kwa kuwa Tundu Lissu ameonekana kuwa na mamilioni ya wafuasi hawataweza kuififisha nyota yake kwa mtindo huo.

Watanzania wameamua safari hii wapo na Tundu Lissu katika boti moja wakiwa naye hadi destination au mwisho wa safari yenyewe ambapo ni pale mjengoni iwe ni Dar au Dom. Viva Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom