Watumishi wa umma Unajua wengi wamekuelewa ila hawawezi kujionyesha kwa sababu ya kulinda ajira zao.
Watumishi hao wa umma ni pamoja hawa wakurugenzi, wakuu wa wilaya pamoja na wakuu wa mikoa.
USHAURI:
Naomba sana katika kampeni zako hawa watu usiwatangazie UBAYA au KISASI kwa sababu tu ni wateule wa Rais , Bali uwaahidi utawasaidiaje kulinda ajira zao ukiwa Rais ukizingatia maisha yao yapo kwenye hizo ajira kwa maana kwamba wanasomesha, wanategemewa, wanasaidia ndugu na wazazi wao kupitia ajira hizo.
Kwahiyo katika kampeni zako hakikisha unajitahidi kutoa maneno ya faraja yanayo akisi hatma yao wewe utakapo kuwa Rais.
KUMBUKA : Kundi hili la watumishi wa umma wana mchango mkubwa sana kwenye ushindi wako wa Oktoba 28 , sio tu kukupigia kura , bali ni pamoja na kutenda HAKI katika uchaguzi huu.
Vinginevyo kama hawatapata hatma ya maisha yao watazilinda Ajira zao kwa gharama yoyote.