Haya nakusaidia
Nenda search button ya hapa JF andika neno escrow. Zitakuja nyuzi mbalimbali za kipindi hicho. Jisomee ujipe ufahamu.

Usisumbue watu hapa
Kwahiyo unapiga kelele tu na hujui hata maana ya escrow. Elimu yako ya madrasa ifiche maana utaonekana punguani.

Hapa tunajadili fact siyo mipasho ya akina Khadija Kopa.

Jibu swali Escrow ni nini?
 
Huyo mama anapotupeleka aisee sio kabisa, kama hizo ndo hoja anawapa kabisa mzishikie mabango, basi naamini kabisa kipa katoka pale.
 
Unayo elimu ya kutosha ya masuala ya mikataba?, unaweza kuuweka hadharani ubovu wa huo mkataba?.
Hivi DPw kuwa na haki miliki kutoka bandari ya Tanga hadi Mtwara ni hali ya kawaida? Bado bandari zote around lake Tanganyika, Victoria Na Nyasa? Tena bila ukomo?
 
Hivi kumbe waislamu ndio wajinga wanaotakiwa kutetea uovu?
 
Nahisi wewe ni kitumbua zaidi. Kama meaning ya a word escrow siwezi ku Google na kupaste hapa?

Unaniona mimi kilaza mwenzako eeeh?
Wewe andazi wa Madrasa unataka kutuletea mipasho. Jibu swali Escrow ni nini?
 
Mungu unamjua vizuri au unapiga siasa za upambe tu?. Wamepita marais tulioambiwa ni machaguo ya Mungu na bado miili ya watu ikaendelea kuokotwa ndani ya viroba pale Coco Beach, kina Roma Mkatoliki wakafanyiwa kitu mbaya na kuamua kuhama nchi.

Mungu ni mamlaka ya juu kabisa yanayomuongoza binadamu, sio haki ya kuyasema kama vile tunaongelea mpira wa Yanga na Simba.
 
0. Kwa hiyo ibara ya 18, inakupa nafasi wewe peke yako, TEC HAINA NAFASI HIYO?

1. Hivi umewaelewa TEC kweli? Kwani wanaupinga UWEKEZAJI au wanaupinga MKATABA? Usipoona tofauti ya kuupinga uwekezaji na kuupinga mkata huo, basi huna hoja.

2.
Findings zao zimetaja vipengere vinavyopingwa. Na ukiangalia, hata akina Prof. SHivji na wengine wanaopinga wantajaja vipengere vile vile..!! Yaani kila anayepinga, anataja vipengere vile vile. Kama nawe huwezi ona matatizo ya vipengere vinavyotajwa, omba ufanunuzi upewe. Mfano nikuu;lize, MKATABA HUO UNA UKOMO? Kama unao, NI WA MUDA GANI?

3. Wala siyo hafu ya maslahi ya kidini. Wewe unayesema hivi wala huweki vifungu vya katiba wala mkataba vyenye kuhalalisha hoja yako. Unaongea tu bila reference yoyote toka popote nje na ndani ya mkataba. Wapingaji wote wametoa vipengere vyenye shida, nyie mnaounga mkono (ikiwemo serikali) ni jukumu lenu kupangua hoja kwa kutaja uzuri wa vipengere vinavyoleta hofu. Mkendelea na blah blah zenu mtaongeza idadi ya watu wanaoweza kutoka hadharani kupinga. HEBU ANGALIA JINSI SUALALAUHAINI LILIVYOWEZA KUWA NA DHAMANA..!! Nikwa sababu tu kuna watu waliashataka kwenda mahakamani kuharakisha washitakiwa wanaondolewa polisi ndani ya masaa wanayostahili kuwepo polisi. Sasa hali kama hiyo itaendelea.

4. Wakipinga TEC mtataja udini, wakipinga akina Prof Shivji mtasema maprofesa uchwara, wakipinga UWAKA (Wanaume wakatoliki) mtasema wanampinga mwanamke, wakipinga CDM mtasema wapinzani kawaida yao kukataa kila kitu etc etc. Yaani majibu mnayotoa yanategemeana na nani anapinga. HUKU NI KUHANGAIKA NA KUNASABABISHWA NA KUKOSA HOJA

CONCLUSION
Serikali haitakiwi kuendelea na mchakato wowote juu ya mkataba huo hadi pale mashaka yatakapoondolewa kwa wanaopinga. Tulishawahi kuwa na mambo kama haya kwa akina RICHMOND, NBC etc na tukapigwa. Hivi karibuni tumeshalipishwa mamilioni ya fedha kwa mikataba ya namna hii. Hii maana yake tuna uzoefu wa serikali kuja na jambo na kulazisha liendelee kama lilivyo na mwishotunalipa mamilioni ya fedha za wananchi/

JIBU HOJA ZINAZOTAJWA NA WANAOPINGA.
 
Maaskofu walidhani bandari ni yao kwa waliokuwa wanayafanya pale.

Wamejeruhiwa vibaya sana.
Maaskofu wametoa tamko moja pekee, tangu juzi mpaka leo hamtulii, nani aliyejeruhiwa vibaya kati yenu na wao?

Hizi stress zitawamaliza na mama yenu dhaifu asiyejielewa.
 
Hivi DPw kuwa na haki miliki kutoka bandari ya Tanga hadi Mtwara ni hali ya kawaida? Bado bandari zote around lake Tanganyika, Victoria Na Nyasa? Tena bila ukomo?
Hawezi kuwa na haki miliki hiyo.DPW anakwenda kumiliki eneo la asilimia nane tu ya bandari nzima ya Tanzania.

Mnalishwa matango pori na nyinyi mnayatafuna mazima mazima bila hata ya kuumiza vichwa vyenu.
 
Kuna ujinga mwingi sana kwa hao jamaa, hizi mbinu za kijinga wamekuwa wakizitumia miaka mingi, bahati mbaya safari hii kazi wanayo, hakuna kurudi nyuma mpaka bandari zetu zirudi kwetu.

Wqcha wapige kelele mpaka vichwa viwaume.
 
YESU NI MUNGU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…