Kunguru hao waoga kauli za mtu muoga BM-21 silaha ndogo sana na hata FARDC pia wanazo zingepelewa BM-27 na BM-30 si wangekimbia hovyo ila BM-21 zinatisha pamoja na udogo wake na zilichangaia sana ushindi wa vita vya Kagera.
 
tofauti yake ni nini? na sisi tunazo zipi?
Ni mifumo ya kubeba na kurusha rokect nyingi kwa mkupuo.

BM-21 mrl 122mm ni mfumo mwepesi(light) wa kurusha rocket nyingi unaweza kurusha rocket mpaka 50 Km.

BM-27 mrl 220mm ni mfumo wa wastani(medium) wa kurusha rocket nyingi,unaweza kurusha rocket kutoka 0.5 mpaka 70 Km.

BM-30 mrl 300 mm mfumo mzito wa kurusha rocket nyingi unaweza kurusha rocket mpaka km 120, yaani unaweza kuzirusha rocket kutoka Goma mpaka Kigali au kutoka Rusumo mpaka Kigali.Kuna kipindi mwezi 12 mwaka jana Rais Felix Tshisekedi wa DRC alinikuliwa akisema anaweza kuipiga Kigali na mabomu bila kuvuka mpaka kama ataendelea kuvuga usalama East DRC hii mifumo FARDC pia wanayo

Hi mifumo yote TZ ipo mingi tu ya kutosha.
 
Kwahiyo mkuu wataka kusema hiyo hiyo Bm21 inawatosha??
 
So unadhani nini shida pale DRC?
Maana hakuna maelezo yakumake sense popote pale !!
 
M23 ni askari wa Rwanda asilimia kubwa. Wako pale kwasababu za kiuchumi. Uchumi wa Kongo unategemea wizi wa madini ya Kongo mashariki.

Siku za hivi karibuni m23 wanekuwa wakipoa kichapo kutika wapiganaji wa kundi la wazalendo linaloungwa mko o na serikali. Tofauti na serikali, Wazalendo wamekuwa wakitumia njia ya kuvizia na kustukiza hivyo kuwapa wakati mgumu m23. Kumbuka hawa wazalendo ni wenyeji wa maeneo kuliko wanyarwada.

Kwa sasa Uganda ameingia kwa upande wa m23 kumsaidia ndugu yake Rwanda anaechezea kichapo.
Angalia hiyo pich ya majeruhi wa askari wa Rwanda kutokana na kipigo wanachooata kutoka Kongo


Pamoja na kuwa SADC imepeleka majeshi kupigana DRC lakini majeshi kutoka Tanzania ndio yenye kuogopwa na kuchukiwa na hao m23 pamoja na mabwana zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…