Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Uhalifu kwa mujibu wa sheria za nchi, dhambi kwa mujibu wa sheria za Mungu/dini
Kwa mfano kumtazama mwanamke kwa kumtamani ni dhambi lakini kwa sheria za nchi siyo kosa/uhalifu
 
... Ukiwakaribisha watu wa namna hii nyumbani kwako wakaishi hapo, lazima mtoto wako atapata ukoma huu kama sio wewe. Kuwakaribisha kanisani ni kuingiza huu ukoma sehemu takatifu ya kumuabudu Mungu.
Hawa mazombi walitakiwa watengwe sehemu wasaidiwe kutolewa mapepo ya kizombi mpaka warudi kwenye ubinadamu kamili ndio waruhusiwe kanisani.
Kwa hiyo unataka kusema huyu mchungaji wa kilokole alifanya makosa kumpokea kanisani Anti Asu?

1674668732099.png

Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga Mwingi Kwa Kuunga mkono ushoga na kusema Mashoga sio wahaliifu, na kwamba ni Wana wa Mungu pia.🙄🙄

Haijaeleweka mara Moja ikiwa huu ndio Msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni ya binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.

Chanzo: BBC Swahili
Nlishawahi sema huyu Nyangumi ni Bigfela!!😲
 
Ww umesema ushoga sio uharifu bali ni dhambi na mm nimekujibu kuwa jambo fulani huwa lina hesabika kama uharifu kwa mujibu wa sheria za nchi husika na si vinginevyo.

Mfano kenya kuuza na kula mirungi sio uhalifu kwa mujibu wa sheria zao ila Tz ni uharifu kwa mujibu wa sheria zetu na ukikamatwa unaenda jera.

Kwa hiyo na ushoga sio uharifu kwa mujibu wa sheria za nchi fulani lakini ni uharifu kwa mujibu wa sheria za nchi zingine hivyo sio sahihi kuisemea dunia nzima.
I'm trying to serve your face, wewe unazidi kujikakamua tu hapa.
Hivi hapa hata mjadala unaoendelea unauelewa kweli?
Unajua hata aliyeyaongea hayo? Umesoma hata tafsiri ya uharifu imerejewa kutoka wapi na ya dhambi kutoka wapi?
usipoelewa kitu jifunze kufuatilia kilipoanzia, siyo unatunga sentensi zako ambazo hata sielewi namna ya kuzijibu zaidi ya kuzidi kukuuliza maswali tu ambayo nayo badala ya kujibu unaleta story zingine
 
MK254 hii habari nafikiri itakuwa ni njema kwake,,, maana yeye ni mfuasi mzuri wa upinde,, Haya njoo upinge na hapa,,
"Hii ni habari nnnjemaa chioni ya leo na mbengo zikafongoke haleloyaaaa "
 
Pope aliyefariki juzi alitumia kigezo cha umri kuachia nafasi ya upapa kwa outside meaning ( maana ya nje ) lakini kwa watafiti wa mambo wanasema na ni kweli kabisa aliamua kwa maana ya ndani ambayo yeye binafsi alipinga kanisa katoliki kuwa chini ya freemason alisema atamkosea Mungu wake akaona hawezi wakwepa au pingana na freemason akaona busara akae pembeni kwa kusingizia tatizo la umri. Huwa ni nadra Sana pope kujiuzulu. Mapapa huwa wanafia madarakani.
Aliyepo ni member wa freemason hata kauli zake za kindumila kuwili yaaani anaingia KISHA anatoka kidogo kuwaacha hewani wasiojua meaning yaani anawaacha watu katikati,anakuwa anasapoti jambo indirect way. Huwezi tenganisha dhambi na uhalifu. Papa aliyekufa papa msomi aliona heri kuachia kuliko kupokea maagizo toka KWA black pope. Papa mweusi ni invisible pope lakini anatenda kazi na white pope.
Freemason ni concept ya kupumbaza watu, wala haipo
 
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga Mwingi Kwa Kuunga mkono ushoga na kusema Mashoga sio wahaliifu, na kwamba ni Wana wa Mungu pia.[emoji849][emoji849]

Haijaeleweka mara Moja ikiwa huu ndio Msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni ya binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.

Chanzo: BBC Swahili

N dhambi ila sio uhalifu hii n sabab haiathiri maisha ya mtu mwingine papa yuko sahihi kbsa na hajajiweka kutetea hao watu mtu ashakua gay utamfanya nn utamuua au utafanyeje lazma umuweke karb mjua vipi mtamsaidia kuondokana na hilo janga
 
Anachukua maagizo toka KWA black pope, ofisi ya black pope ipo vatican ghorofa la saba kwenda chini.
Black pope anapewa maagizo direct toka KWA lusifer.
White pope uchukua maagizo toka kwa Black pope na kuyaleta kwa wanadamu.
Papa huyu huyu ndie aliunga mkono utoaji mimba.
Leo anaunga mkono ushoga.
Inasikitisha na kufedhehesha sana. Amelivua nguo Kanisa Katoriki. He is not a Christian.

Pope is a pure Devil.
 
Wezi na Majambazi ni Wahalifu,
Ndio maana Papa kasema Ushoga sio uhalifu japo ni dhambi
Mtu anamlala mtoto wako wa kiume hadi anageuka shoga unasema hajafanya uhalifu ?

Hivi upo timamu kweli wewe ?
Au ndio usha possesses mi demons.
Kumkosea Mungu ni uhalifu namba moja.
Huyo papa kawazuga tu. Katumwa na Rusifer.
 
Hebu nishushiee wine kidogo..nikiendeleaa kutafakarii maneno haya ya baba mtakatifu wetuuu....
 
Back
Top Bottom