Wasababishi wote waliovuna mabilioni kwa kuwaibia watu baada ya kuwabambika kesi yafaa wataifishwe pesa zao zikalipe fidia.
 
Daaaa, Kesi 147 zote za kutunga!!
Upuuzi kabisa,
Hivi unamtungia mtu kesi ili upate nini?

Nadhani polisi wanazo nyingi za aina hiyo.
DPP futa kesi ya UAMSHO, ile ni kesi ya kubambika tu.
 
Shida ya maccm ni kulindana majizi ya awamu iliyopita yote yapo uraiani badala ya kuwa jela,yalijifichia kwenye ukali Ili kuficha uhalifu wao.
 
Inatakiwa wachukue nafasi zao wao wakakae ndani miaka 6 kusubiria ushahidi kukamilika Ili nao waonje waliyowafanyia wenzao
Shida kwa mtu asiyekuwa mwaminifu hufanya mambo hats maovu iliawezekutengeneza fursa zisizo halali ama kwa mhusika mwenyewe, au kwa ndugu wa karibu wa mhusika wa ubambikaji nao waweza kuwa ni wakukomoa, ama ni lengo la kumega alichokuwa nacho mhusika au familia yake. Hivyo ya faa kuchunguza sababu za bambika hizi keanu zaweza ibua yaliyojificha nyuma yake.
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Tunatesena wenyewe kijinga kabisa.
Bara lina watu wapuuzi sana hili
 
Kwa kweli, “Zilongwa hovyo zitendwa chaka.” mama aache kuimba “madumbatu” na mataarabu , inatosha sasa afanye kazi kwa vitendo tuone, arudishe umoja wetu ulioparaganywa na Magufuli.

Kauli tu ya kusema waachiwe huru, wafungwa wa kisiasa, wateteahaki na wanahabari ingeleta faraja na tungemuona ni rais mwenye msimamo.
 
Wamepiga pesa nyingi Sana hawa watu sema tu Utawala wa kulindana tu
 
Kwakweli Samia suluhu amejifunza mambo mengi kupitia mapungufu ya mtangulizi wake. Hapendi kuendeleza mabaya. Tutarajie hata sheria kandamizi hapo mbeleni zitakuja kupelekwa Bungeni kwa marekebisho
Mkuu hata sheria nzuri zilizopo zilikiukwa kwa visingizio vya kunyoosha nchi.
Wananchi wameumizwa sana kinyume kabisa cha sheria kwa chuki na ubabe wa mtu mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…