Rais Samia: TAKUKURU wamefuta kesi za kubambikizia 147, Polisi na nyie jitazameni
Mdude Nyagali, kiongozi wa CHADEMA Songwe, alitekwa nyara na kuteswa na wanaUsalama wa Taifa kwa kupinga na kukosoa udikteta wa Magufuli. Rais Samia anaimba kuhusu maridhiano lakini Mdude bado ni mmoja wa wafungwa wengi wa kisiasa wa utawala huu. Zilongwa mbali na zitendwa mbali!
1621350020564.png
 
Wasababishi wote waliovuna mabilioni kwa kuwaibia watu baada ya kuwabambika kesi yafaa wataifishwe pesa zao zikalipe fidia.
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====




Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.
Daaaa, Kesi 147 zote za kutunga!!
Upuuzi kabisa,
Hivi unamtungia mtu kesi ili upate nini?

Nadhani polisi wanazo nyingi za aina hiyo.
DPP futa kesi ya UAMSHO, ile ni kesi ya kubambika tu.
 
Shida ya maccm ni kulindana majizi ya awamu iliyopita yote yapo uraiani badala ya kuwa jela,yalijifichia kwenye ukali Ili kuficha uhalifu wao.
 
Inatakiwa wachukue nafasi zao wao wakakae ndani miaka 6 kusubiria ushahidi kukamilika Ili nao waonje waliyowafanyia wenzao
Shida kwa mtu asiyekuwa mwaminifu hufanya mambo hats maovu iliawezekutengeneza fursa zisizo halali ama kwa mhusika mwenyewe, au kwa ndugu wa karibu wa mhusika wa ubambikaji nao waweza kuwa ni wakukomoa, ama ni lengo la kumega alichokuwa nacho mhusika au familia yake. Hivyo ya faa kuchunguza sababu za bambika hizi keanu zaweza ibua yaliyojificha nyuma yake.
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Tunatesena wenyewe kijinga kabisa.
Bara lina watu wapuuzi sana hili
 
Kwa kweli, “Zilongwa hovyo zitendwa chaka.” mama aache kuimba “madumbatu” na mataarabu , inatosha sasa afanye kazi kwa vitendo tuone, arudishe umoja wetu ulioparaganywa na Magufuli.

Kauli tu ya kusema waachiwe huru, wafungwa wa kisiasa, wateteahaki na wanahabari ingeleta faraja na tungemuona ni rais mwenye msimamo.
 
Shida kwa mtu asiyekuwa mwaminifu hufanya mambo hats maovu iliawezekutengeneza fursa zisizo halali ama kwa mhusika mwenyewe, au kwa ndugu wa karibu wa mhusika wa ubambikaji nao waweza kuwa ni wakukomoa, ama ni lengo la kumega alichokuwa nacho mhusika au familia yake. Hivyo ya faa kuchunguza sababu za bambika hizi keanu zaweza ibua yaliyojificha nyuma yake.
Wamepiga pesa nyingi Sana hawa watu sema tu Utawala wa kulindana tu
 
Kwakweli Samia suluhu amejifunza mambo mengi kupitia mapungufu ya mtangulizi wake. Hapendi kuendeleza mabaya. Tutarajie hata sheria kandamizi hapo mbeleni zitakuja kupelekwa Bungeni kwa marekebisho
Mkuu hata sheria nzuri zilizopo zilikiukwa kwa visingizio vya kunyoosha nchi.
Wananchi wameumizwa sana kinyume kabisa cha sheria kwa chuki na ubabe wa mtu mmoja
 
Back
Top Bottom