Kenge maji😂😅
 
Hizi ndio akili za mwafrika, tena mtanzania. Mchele umeuzwa nje leo tunaenda kununua mchele nje.
Tatizo ni umaskini we mkulima avune leo anashida leo umwambie autunze mpaka demand itakapokuwa kubwa...hana akiba, hana ghala za kuhifadhia...kinachofuata ni mchele unauzwa tena ukiwa shambani kabla hata ya kuvuna...
 
Mtaji mkubwa wa wanasiasa ni jamii kuwa na wajinga kama wewe

USSR
 
Nipo Holili hapa nashangaa ati mchele unatoka Kenya unaingia Tanzani na ni mwezi uliopita tu mchele ulikua unatoka huku unaenda kule, hivi Kenya wanakilimo gani cha mpunga?
 
Blah blah, blah, blah...pumba tupu
 
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji, amesema serikali imetoa vibali kwa baadhi ya wafanyabiashara nchini kuingiza mchele tani elfu tisini, ambazo zinatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri Kijaji amesisitiza kuwa, serikali haitarajii ongezeko la bei ya bidhaa zinazotumika kwa wingi katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kwaresma, ikiwemo sukari na unga wa ngano.
 
Si walisema wanamwinua mkulima?
 
Hiiya mchele kutoka nje Zanzibar ipo sana na still maisha magumu vile vile. Huku Kuna mchele unaitwa Mapembe ukiiiva ukiumwaga kwenye sahan kama umemwaga mchanga na hauna Radha kabisa pia Kuna mchele unaitwa jasmini nk
 
Ni mtizamo hasi tu mbona Zanzibar karibu 90% ya mchele wanaotumia miaka yote unatoka nje?!!ndio maana kule unakuta mchele siku zote unachezea 1200-.1500/kilo .labda mwaka huu tu.Kule mchele wa bara ni anasa!!wao kitu mapembe.
 
Hilo ni jambo jema.
Sasa wajipange kwenye suala la kusimamia mara hizo tani za mchele zitakapo wasili.

Nashauri;
Vyombo vyote visimamie ili wafanyabiashara na wenye tamaa wasije kuhujumu lengo lililo kusudiwa.
 

Wasije kutuletea michele ya "Kitumbo" au "VIP" yenye kudunda kama mpira wa plastic ,TFDA inatakiwa mfanye kazi yenu ipasavyo kabla mchele haujaingia sokoni.
 
Dr Venance Fupi.
 
Wiki hii katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, Prof Lipumba alizungumza mengi. Mojawapo alishauri serikali kuingiza chakula chake kwenye soko ili bei ya chakula ishuke.

Sasa inaonekana serikali imefanyia kazi ushauri wa Lipumba kwa kuruhusu kuagiza nje.

Vipi serikali inasubiri nini kuingiza mahindi yake sokoni ili bei ishuke mana muda wa mavuno umekaribia itanunua tena? (Lipumba) au kiuchumi inagoma?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Blah blah, blah, blah...pumba tupu
Bora umefungua brain yako nimeishajua imejazwa na Nini na Ni ngumu kuobadili so ngoja nikuache. Ni sawa mtu mwaathirika na drugs ama kamari ama sex ama amejaa chuki na wivu unadhani utamuweza. Iko cheap mno your mind. Make your mental to be strong pyschologically since you're lacking mental skills
 
Tatizo ni umaskini we mkulima avune leo anashida leo umwambie autunze mpaka demand itakapokuwa kubwa...hana akiba, hana ghala za kuhifadhia...kinachofuata ni mchele unauzwa tena ukiwa shambani kabla hata ya kuvuna...
Tatizo ni sera si wakulima.

Ukiwa na sera nzuri utapata wakulima wakubwa na wale wadogo kisha wahakikisha wakulima wakubwa wazalisha mazao yote muhimu kufikia kuwa na akiba ya kutosha.

Tanzania bado haina wakulima wengi wakubwa ambao waweza kuendesha sekta ya kilimo kiuhakika.

Ni jukumu la waziri wa kilimo na chakula akishirikina na wataalam wake kuhakikisha Tanzania inakuwa na chakula cha kutosha.
 
Wasije kutuletea michele ya "Kitumbo" au "VIP" yenye kudunda kama mpira wa plastic ,TFDA inatakiwa mfanye kazi yenu ipasavyo kabla mchele haujaingia sokoni.
Mchele utaokuja ni ule ulokuwa ghalani kitambo.

Mkuu, wapenda mchele gani Basmati ya India (Tropy Indian) huu ni ghali hivyo sahau.

Halafu kuna Tilda Pure Basmati, Long Grain essential kwa wale vegans.

Yaani kuna aina nyingi sana ukichanganya na ule mchele GM, lakini yote ina matumizi tofauti kama kwa pilau, biriani, Paela na sushi.

Eee Mungu baba wa mbinguni, tusaidie watanzania tupache mchele mzuri.
 
0.0%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…