Hii issue inaibua mijadala mingi kwa sababu prof Jay ni mwanasiasa, lakini tukiichukulia Jay kama defend na mmoja wa mziki wetu wa bongofleva anadeserve support ya ya serikali, isingekua busara sana kuwaachia mashabiki pekee waubebe mzigo huu
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.


hii sio sawa, anatibiwa kama nani..

gharama za wagonjwa wengine hapo muhimbili wasio na mbele wala nyuma nazo Serikali itazibeba? tuwe serious kidogo.
 
Hii issue inaibua mijadala mingi kwa sababu prof Jay ni mwanasiasa, lakini tukiichukulia Jay kama defend na mmoja wa mziki wetu wa bongofleva anadeserve support ya ya serikali, isingekua busara sana kuwaachia mashabiki pekee waubebe mzigo huu
Walipa kodi walalahoi wenyewe hawahitaji support ya serikali?
 
Za kuchangia mawakili wamtoe mtu, mahabusu zinapatikana,
Lakini za kuchanga matibabu apate mtu, watu wa chama mashati washikana,
Chama cha mgonjwa cha "watu", ukitaja mgonjwa mwapishana,
Heko Mheshimiwa Ummy Mwalimu, utu wa mtu kuupambania.
Chuki zako kwa chadema zitakuua ndugu. Unakurupuka ovyo bila facts. Kwa taarifa yako michango imekuwa ikiendelea na tayari hao unaowakebehi wameweza kukusanya zaidi ya million 13 mpk juzi.
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Kujipendekeza kwa akina Ummy pesa hna au alipokuwa mbunge si alikuwa na bima ya kibunge au wamezingua sana
 
Lakini kweli, wengi wetu ni mbumbumbu na mazuzu ila wachache wenye uelewa (20% ya waliotaka vyama vingi???) watadharau hii move na ni halali yao mbele za Mungu.

Ukienda Muhimbili kwenye jengo la watoto basement floor (kwenye clinic ya kidney dialysis) ndio utajua kuwa watu tuna shida na wengi wanashindwa kuhimili karibia milioni kila week.

Sasa tumekuwa tukishuhudia kijana Malisa Godlisten akichangisha pesa na kufanikisha hata kuwapeleka watu india na wakapona. Kwa vile michango ilishaanzishwa na lengo lilikuwa Tsh 20m, basi waziri angeliwauliza zimeshachangwa ngapi (kujumlisha 2m ya CEO wa clouds) then walau wakatop up ili 'kwa vile wana pesa' wakawasaidie hao Watz wengine walio hoi kama Prof. J.

All in all kuugua na kupona hukutegemei una bima, account yenye billion ngapi wala nini bali ni mapenzi ya Mungu. Kama ni pesa tu basi wazee wetu kama Hans Pope, Subash Patel au JPM mwenyewe tungelikuwa nao. Wanajidhihirisha kuwa kila dogo au kubwa hawana plan ya maana na ya kudumu pali ni kutafuta cheap popularity
 
Acha kushabikia dhulma hatukatai serikali kumtibu pro.j lakini wajibu wa serikali ni kuwatibu raia wake wote bila ubaguzi wa aina yoyote vile.
Mm naona ni kheri Angeenda kumsalimia tu alafu akae kimya?
 
Kuna umuhimu wa kuboresha sekta ya afya ili huduma ziweze kufikiwa kwa watu wote.

Maswala ya kukopa fedha ili kujenga vyoo na madarasa tuyaache sasa na kufanya mambo ya msingi zaidi kama haya ya Afya.

You can imagine tunachukua trilioni za pesa wakati hatuna hata dawa hospital.
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Nchi hii imebadilika sana.

Tangu watawala wa CCM wagawane Mali za umma na kujiwekea mishahara na mafao makubwa na kujilimbikizia Mali ,Watanzania wamekua na roho mbaya sana .
Watu wanaombeana na kutakiana mabaya tu Kwa sababu ya tofauti za kisiasa.

Shetani inaonekana amefanikiwa kuweka Ubalozi Tanzania.

Prof. Jay alitumikia Taifa hili Kwa uamunifu mkubwa .
Mama Samia Kwa Upendo wake na utu wake ameamua kufanya jambo jema tofauti na awamu zilizopita waliokua wanamtaja Mwenyezi Mungu midomoni mwao ila nafsini mwao walikua watu waovu wakubwa.

Kwa Mwislam yeyote matendo kama hayo ni Ibada na thawabu Kwa Mwenyezi Mungu.
Lakini Kwa wanaoweka Siasa mbele na umaarufu wa kishetani kwao ni kupinga tu .

Rais ana mafungu Mengi sana. Kwa wale Marais wenye Imani zisizokataza ukevi na ufuska anaweza akatumia tu mabilion ya pesa Kununua pombe Kali na za bei kubwa kutoka Ulaya ,huku akiwa anabadlisha nyumba ndogo.

Tanzania awamu ya SITA tumebahatika kumpata Rais mcha Mungu wa kweli.
Anayejua maana ya kumwogopa Mungu na kuwatumikia watu huku akijua kuna kuulizwa kesho ahera, lakini Cha ajabu Bado watu wanapinga mpaka matendo mema ya huruma.

Ama kweli wahenga walisema " Tenda mema uende zako usisubiri shukrani" . Na wengine wakasema " Shukrani ya Punda ni Mateke."

Watanzania Itatuchukua miaka mingi sana Kuja kupata Rais kama Mh. Samia Suluhu kupitia CCM ,Chama kilichojaa watu katili kimfumo na wanye kuweka mbele maslahi Kwa namna yoyote.
Tumempata Mama hasa tushukuru Mungu. Tungelimia meno. Mwenyezi Mungu ni mkubwa kutuletea Mh. Samia.

.Tuacha Roho Mbaya.
 
Maneno Makali sana lakini nakuhakikishia ungepewa hiyo wizara usingeweza kuiendesha hata miezi miwili . Maamuzi yake ni sahihi sana na zipo sababu zilizofanya seeikali Kuingilia hili Suala. Utakakatishaji fedha una njia nyingi sana na fedha za kufanya Uhalifu zina njia nyingi. Serikali ina macho kama imeshaamua kuingilia hili Suala wananchi tukae kimya tufanye mambo mengine mf. Kuhudumia familia yake n.k
 
Upo sahihi, lakini vipi kwa wale wasio na uwezo hata wa kulipa elfu 10 kumuona daktari? Wao wanasaidiwa na nani?
 
Wewe kama sio Mbunge wa Sasa wa jimbo lile ,Utakua, ndugu yake au rafiki yake au Utakua unawaza kugombea jimbo lile kupitia Chadema mana unajua wanachama wa Chadema pale ni wengi. Mana sio Kwa hizo roho mbaya za kumwonea wivu mpaka mgonjwa mahututi. Acheni hizo bwana. Utakuta ni mtu kabisa anamtaja mpaka Mwenyezi Mungu lakini anachuki kubwa hivi .

Kuna shida gani Prof.Jay akagharamikiwa matibabu halafu akipona ndipo tukamwambia Rais kuwa wapo wengine wanaohitaji Matibabu pia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…