Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Hongera wa uthubutu Mh. Rais.
Hongera kwa kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali, bandarini palikuwa pananuka; kubadili tairi, kung'oa redio nk.Matumaini ni makubwa sasa.Inshaalah.Takbir
 
Mmh! Hata kwenye gesi ya Mtwara tuliambiwa sasa Mtwara itakuwa kama NewYork na umeme utakuwa bure kama mwanga wa jua.

Wakati kiwanda cha Dangote kinajengwa, tuliambiwa bei ya sementi itapungua na kuwa sh elfu 5.

Lakini Sasa yako wapi??
Umesahau mwendazake livyofuta mikataba yote ya gas na madini, sasa inatutokea puani?


Hivi mpo duniani nyinyi?

Papai ni papai tu hata liwekwe kwenye embe dodo linabaki kuwa papai.
 
Kwa andiko hili kuanzia leo na ku ignore kumbe wewe ni mjinga kiasi hiki? Sikutegemea kabisa kuwa unaweza kuwa na mawazo kama haya kichwani kwako.
Kama inamiliki cheti fake Hadi Leo,

Upeo wa kuelewa mambo utautoa wapi?

Wamiliki wa DP World ndio wafadhili wa Royal tour.
 
Bado TEC+MWABUKUSI , SILAA, wanaendelea kua Mashujaa wa Taifa hili.

Hili limethibitishwa na Makamo wa Rais, kukiri ya kwamba, wamesikiliza maoni ya Watanzania, na hatimaye wamekuja na Mikataba hii!!.


Mwabukusi Oyeeee
Kabisa kelele zao zimesaidia sana,tofauti na hapo tulikua tunapigwa mchana kweupee.Nashangaa wanaowabeza sijui wanawaza kwa kutumia nini.
 
Wale mliozoea wizi na ubadhirifu hapo bandarini sasa mjipange inafungwa mitambo ya kisasa hapo haiingii mtu ndani ya meli kukagua container
 
Huku Mama, pale Mbarawa, kule Hamza. Ukirudi hivi Sultan.


Ni maendeleo kwa kwenda mbele tu.
 
BANDARI YA DAR ES SALAAM INA JUMLA YA GATI 12, NA ZOTE KUENDESHWA KWA AINA YA UBINAFISHWAJI
1697973244714.png


Magati kuanzia gati 0 hadi 11 ya bandari sasa kuwekwa katika hali ya aina ya ubinafsishwaji taarifa inasema : magati namba 4-7 pia magati 0 -3 na upande wa kuanzia gati 8 hadi 11 mwekezaji tofauti na DP World anaswakwa.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania​

Nyenzo zilizopo ambazo husaidia uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es salaam ni kama ifuatavyo: -
  • Kuna magati ya shehena mchanganyiko (0-5) kwa ajili ya shehena kavu na magari.
  • Magati ya makasha (5-11) .
  • Vihenge vya kuhifadhia nafaka (silos) vyenye uwezo wa tani 30,000, vituo vya makasha vya nchi kavu (ICD) vyenye uwezo wa kuhifadhi 24,300 TEUs na CFs yenye uwezo wa kutunza magari 6,000 kwa wakati.
  • Pia kuna Single Point Mooring (SPM) yenye uwezo wa kuhudumia meli zinazobeba hadi tani 150,000 za mafuta ghafi na mafuta yaliyosafishwa.
  • Bomba la Mafuta Kurasini (KOJ) kwa ajili ya bidhaa ambazo zimesafishwa inapokea meli zenye ukubwa wa tani 45,000 (MT) kwa KOJ1 na tani 5,000 kwa KOJ2.
Source : Bandari ya Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom