Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Yani Jangili, jambazi Suleiman Nchambi mmelipitisha tena liwatumikie miaka 5 ijayo!!!!

Inauma Sana kwa kweli.

Nmeambiwa jamaa kagawa mkwanja kwa kila Mjumbe laki moja ,hapo si mnawauza mnaowawakilisha.

Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Mbunge wa Kishapu(CCM), Suleiman Nchambi aliyekutwa na silaha 16 aburuzwa mahakamani, asomewa mashitaka 12
Kumbe tayali kachaguliwa kuwa mbuge !!! Uchaguzi Ni October 2020
 
Mwenye dar yake sasa anatakiwa arudi Koromije.

Dar sio pa kisoro arifu.
 
Kasoro nyingine ni kuwa nimeona kwa mfano Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ambaye anawajua wajumbe wote wa mkutano wa kumchagua mbunge nae anaamua kuchukua fomu ili agombee ubunge, kwa mtu kama huyu utakuta tayari kawasuka hao wajumbe wasiozidi 500 na ni rahisi kwake kupita kwa kuwa katika miaka mitano ya uenyekiti amekuwa karibu na wajumbe wote,huu si utaratibu mzuri,ungewekwa utaratibu kuwa anayetaka kutia nia akiwa kama ni mbunge ,au waziri ,au mwenyekiti wa CCM kwenye jimbo basi anatakiwa ama atoe notisi kabla ya miaka 3 au 5 kuwa ama achague kuendelea na vyeo alivyonavyo au aachie akisubiri kuja kugombea ubunge katika msimu mwingine wa uchaguzi.Watia nia masikini na ambao hawana nyadhifa serikalini inakuwa vigumu kuweza kupata nafasi ya kuteuliwa kwa huu mfumo, sasa nafasi zitakuwa ni za wenye nyadhifa serikalini na kwenye chama,huu si mfumo rafiki kwa mlala hoi.



Uko sawa mkuu! Mfumo wa baadhi ya wajumbe kupiga kura za kumpitisha mgombea rushwa haitoisha.

Naanza kuona dalili za wapinzani wengi kurudi bungeni.
 
🤗🤗🤗usitukane ukunga na uzazi ungalipo


Leo ndiyo nimepata maana ya hii methali tangu mwaka 1980 nilipoijua kwa mara ya kwanza
 
Hawa wapuuzi flani walihama wakapewa nafasi CCM saivi wamewanyoosha, Shukwani ziwaendee CCM na mwenyekiti wao. Mwenyekiti kashamaliza teuzi za UDAS, URC, UDC, U-RAS, U-DED waliopoteza watajutia nafasi walizopoteza.

  • Mtulia
  • Katambi
  • Kafulila
  • Nassari
  • Silinde
  • Lijualikali

Wateule walioacha teuzi nao wamegaragazwa
  • Makonda

Wasanii waliojiforogoa kwamba wanaipenda CCM nao CHALIIIII

Wanaharakati CHALIIII!!

Vigogo CHALIII!
  • Kimei
  • Mwakyembe
Hivi Musiba alitia nia kule Mwibara?
 
Mwakyembe haamini [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
2461756_EdZkIJLXYAQhx5c.jpg
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa kasi aliyonayo Mh. Rais na kwa sababu nchi inataka kuelekea uchumi mkubwa wa kati yaani higher middle economy country, hii kazi ya kuchagua wagombea wasingeachiwa wajumbe peke yao maana wao wanaweza fanya kwa maslaahi yao au kwa ushabiki ni bora hawa wagombea ubunge wangeteuliwa tu kwa maslahi ya taifa.
Kuna kitu hujaeleweka pia, unasema "hii kazi ya kuchagua wagombea wasingeachiwa wajumbe peke yao" lakini hujasema wateuliwe na nani. Na kama hutaki wajumbe ndio wateue, unataka mtu mmoja ndiye ateue? maana kama kuna kamati unafikiri ndiyo ingefanya kazi hiyo then ujue kamati hiyo nayo itakuwa na wajumbe na wajumbe hao ndio watakapofanya uteuzi!

Bado una nafasi ya kurekebisha maamuzi yao; katika uchaguzi mkuu kutakuwepo wagombea toka vyama mbalimbali. Kama uliyemtarajia CCM hawatampitisha angalia katika vyama vingine, Na kama ikitokea kuwa hata huko usione anayefaa, basi angalia tatizo lisije kuwa ni wewe mwenyewe!
 
CCM siyo chama rafiki kwa wanyonge. Pamoja na muamko mkubwa uliooneshwa wanyonge ktk uchaguzi huu kuchukuwa fomu za kugombea ubunge, lkn hakuna hata mmoja ambaye ni mnyonge atapata nafasi ya kupitishwa.

Kwanini? Kura za maoni wengi wao wamepata sufuri kabisaa! Ndiyo kisema hata majina yao hayawezi kupelekwa kwa " "mzee wa mood" (a.k.a inategemea nimeamkaje).

Wenye nazo tu ndiyo wamejizolea kura nyingi karibu kila Jimbo.

Shauri zenu......!!!!
hayo waulize wapiga kura
 
Bado mapema Sana kusema kapita..
Bado jina lake halijapita kwa watu wa wilaya, mkoa mpaka Taifa naamni huko pote hawezi kutoboa.
 
Na hii ndio sababu iliyochangia watu wengi wakachukia ccm naamini ccm mpya itakuwa na sura mpya nyingi zenye kiu na uwezo wa kulipeleka taifa mbele sioni sababu ya mtu aliyekuwa mbunge kwa vipindi kadhaa na hakufanya lolote kurudi tena bungeni.

Taifa lina vijana wengi wazalendo ambao wangeweza kuwa viongozi wazuri lakini hata pesa ya kuchukua form walikosa naimani sana JPM hatotuangusha.
Acha kulalamika, October utakuwa na wagombea wengine wengi maana huu wa ccm ni mchakato wa kupata mpeperusha bendera wao, na chadema nao watakuwa na wa kwao, viyo hivyo kwa cuf, act nk. Kama utaona katika wote hao hakuna anayefaa, basi nalo litakuwa ni neno!
 
Back
Top Bottom