Lissu ni kama vile ameshashinda uchaguzi huu kwa hoja zake 7 ambazo zimepata nguvu na kuaminiwa na jamii. Na hii inajidhihirisha maeñeo mbalimbali ambayo amepita kufanya kampeni.
Lissu ni kama vile mhubiri wa injili, kila eneo analopita shetani anapoteza nguvu na neno linabaki mioyoni mwa watu. Maeneo ambayo bado hajapita ndio yamebaki kuzungumzia habari za CCM, lakini yatakapofikiwa na habari njema ya injili ya wokovu na ubatizo wa maji mengi na wao wataachana na CCM.
Hoja 7 ambazo Lissu zimemwongezea nguvu toka kwa makundi mbalimbali ambazo CCM wamekosa majibu yake
1. Vitambulisho vya wajasiliamali;
Ni hoja ambayo imepokelwa vizuri na watamzania, kila kona.CCm wameshindwa kujibu hadi sasa, wamebaki tu kudema dema kwenye majibu yao kwamba magufuri anawapenda wamachinga, Mara vitambulisho sio lazima ,wakati wamevitungia na sheria tayari. Lissu shikilia hapo hapo kwa mpaka waeleze ni lini wamachinga walioomba wauziwe vitambulisho visivyo na picha wala jina
2. Maslahi ya watumishi, nyongeza ya mshahara.
Hoja ambayo haijajibiwa hadi Leo, na ccm wamekosa majibu wakaeleweka kwa wananchi. . Nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria na sio takwa la mtu . Alisikika Mara moja akisema hajapandisha mshahara ila edhibiti mfumuko wa bei, na akapata majibu yake toka kwa Lissu kwamba bei ya sukari ya 2015 na Leo 2020 ipo sawa, ? "Wananchi hapana" Lissu " anatuambia nini. Baba shikilia hapo hapo wameshalegea na hawana majibu
3. Suala la pension na kiinua mgongo kwa wastaafu
Watu wengi walikuwa gizani na suala lakini baada ya kulitolea maelezo sasa nalo limepata hamasa miongoni kwa watanzania kwamba kuanzia mwakani wastaafu hawatapata pension zao zote baadala yake watapata nusu. Hilo limeonekana kuwa chuki kwa makundi hayo na CCM wameshindwa kutolea majibu ya kueleweka . Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyooka tayari
4. Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato na hifadhi ya wanyama
Hoja hapa sio ujenzi ,hoja inayoonekana hapa ni namna mradi unavyotekelezwa kwa ufisadi mkubwa wa kupeana tenda na Ndugu yake Mayanga . Mpaka Leo hoja hiyo Magufuli na CCM yake wameshindwa kuitolea majibu, kwa nini aingilie mchakato wa tender na kuagiza apewe ndugu yake na watu sasa huku wanasema ni kama mtu ameamua kupitishia di kwa ndugu yake. Amenipigia pasi kwa mbele ,na suala la hifadhi pia ndio hawana majibu kabisa .Baba Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyong'onyea tayari
5. Suala la ununuzi wa ndege
Hii hoja ilianza kwa kasi mwanzoni kunadiwa na ccm lakini baada ya Lissu kuanza kushughurika Nayo wameshakimbia. Lissu amezungumzia masuala ya Faida na mchakato wa ununuzi wa midege hiyo imegubikwa na ufisadi mkubwa na kwamba anayejua ni Magufuri na mjomba wake Dotto James. CCM mpaka Leo wamepoteana na ajenda ya ndege sio ajenda yao tena kwenye kampeni zao.Lissu wabananishe hapo hapo kwenye kona washindwe pa kutokea.
6: Ukosefu wa Ajira kwa makundi mbalimbali
Eneo hili limepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa makundi mbali mbali ya vijana. Tangu 2015 ajira zimetolewa kwa walimu wa sayansi na kada za afya. Kada nyingine hazijaguswa kabisa . Hoja yake hapa magufuri imebaki kuwa ni watu wajiajiri wakati yeye mtoto wake Jesca amemwajiri wizara ya mambo ya nje, mwingine amempa RAS iringa .hao walishindwa kujiajiri hadi awaajiri. Watoto wa wanyonge ndio wanaohimizwa kujiajiri. Hapo napo Lissu shikilia hapo hapo pana tija na kundi kubwa la wahanga
7: Waathirika wa vyeti feki
Hii ni hoja ambayo imepata kusemwa na Lissu, kwamba hao walio wa ajiri ni wao ccm na kinachozungumzwa hapa ni watu kufukuzwa kama mbwa bila kupewa mafao yao, ambayo wamechangia kwa miaka mingi halijulikani lilipo enda. Hao ni watanzania wenzetu na sio wakenya wala wamalawi, wamelitumikia na kutufundishia watoto wetu kwa miaka mingi hadi wengine wamekuwa maprofesa. Michango yao ipo wapi kama hawajapewa, Magufuri na ccm yao iliyojaa roho ya kuumiza watu waseme wamepeleka michango yao ya pension waliyokuwa wanachangia kwenye mifuko ya hifadhi
8: Magufuri amesambaza wasio julikana kila kona
Hii inasababisha watu ukiikosoa tu serikali unakamatwa soon.
Wasio julikana inafanya watu tunashindwa kunya wala kukojoa usiku
Nashauri Lissu sasa kwa kuwa kwenye miji yote na vijijini amefanikiwa kuiteka sasa ajikite katika kuwaaminisha watanzania ni namna gani walinde kula zao. CCM wamebaki na mbinu moja tu ya kuwategemea wakurugenzi na NEC, ili wawavushe hapo walipo kwenye tope kwenda nchi kavu. Katika hotuba zake sasa ajikite kuwahimiza wananchi kulinda kura zao, hii ngoma imeshaisha . Wakurugenzi na hawa watendaji kata ambao wamepewa maelekezo marafuku kuwatangaza wapinzani kwenye maeneo yao ndio imekuwa mwiba na Wapinzani wasipo jipanga vizuri mwishoni wataumizwa na hao watu.
Ushauri wangu Lissu sasa ajikite katika kulinda kura. Watendaji wa kata si wa kuchekewa na kuendelea kuachwa kwani kwanza ni watu wa chini mno, lakini ni watu ambao wameshapokea vitisho, hivyo inabidi kazi ya ziada ifanyike. Umati kwa umati Huo Huo wanaojaa kwenye mikutano yao wahimizwe pia wawepo hivyohivyo kwenye kulinda kulinda kura zao kwenye vituo vya kata na ofisi za wakurugenzi. Kwa umati ule wa mwanza wakifanikiwa kukaa kwenye kata na ofisi za wakurugenzi kazi itakuwa imeisha.
Kama una hoja nyingine ambayo unaona bado Lissu bado hajaizungumzia ambayo inaweza kuteka mioyo ya watu iweke hapa ,lakini pia unaweza kupendekeza mbinu sahihi ya kulinda kura
Chaaaaao, tuonane 28 oktoba