Amani iwe nanyi wadau!
kama nilivyosema hapo juu mwaka 2015 sikumpigia kura Lowassa kwa sababu kadhaa ikiwemo kuwa sikuamini kama yeye ndo mtu sahihi anayebeba maono ya Tanzania. Nilimuona kama opportunist aliyekosa nafasi CCM basi akaenda chadema ili atimize ndoto zake. Miaka 5 sasa nimejilidhisha kuwa Lowasa niliyegoma kumpa kura 2015 yupo vilevile kama nilivyomuona mwaka ule. Sasa amerudi CCM na anakula meza moja na CCM.
Mwaka huu 2020 nimejilidhisha vya kutosha, na bila shaka yeyote nasema rasmi nitampa kura yangu Tundu Lissu na nitawaelimisha watanzania wengine wampe kura zao Tundu Lissu. Sababu zangu za kumpa kura Tundu Lissu mwaka huu ni hizi
1. Tanzania inahitaji Katiba Mpya haraka iwekezanavyo. Na sioni Magufuli kama anaweza kutupa iyo katiba mpya ambayo ni ya wananchi.
Kwenye hili Ni kweli kuwa katika miaka 5 ya serikali ya Awamu ya Tano ndo kipindi ambacho nimeona umuhimu wa katiba mpya. Katiba inayopunguza nguvu za Raisi na kuweka Uhuru wa Mahakama, Bunge na vyombo vingine .
Mambo nikiyoyaona kwenye Awamu hii hasa bunge kutunga sheria za hovyo, Mahakama kushindwa kusimamia wajibu wake wa kulinda haki za wananchi huku watu wakionewa mchana kweupe na taasisi mbalimbali vikiwemo vyombo vya Habari kinyanyaswa vibaya sana ni dhahili kuwa Ni sasa na si vinginevyo, Tanzania tunaitaji katiba Mpya. Na kwa sababu Magufuli hawezi kutupa katiba mpya ya wananchi basi lazima nimchague Tundu Lissu.
2. Mfumo wa Tanzania wa Elimu kuhitaji mabadiriko ya haraka ili kulinusuru Taifa.
Wandugu, tuseme tu ukweli , Elimu ya Tanzania ni ya hovyo kupindukia. Ni elimu inayohimiza mtu kuwa na uwezo wa kukariri huku akiwa hawezi kudeliver kwenye kazi. Ni elimu iliyopitwa na wakati ambayo haimuandai mtu kuweza kushindana kwenye soko la ajira sio ndani ya nchi Bali hata nje ya nchi. Nimeshihudia hata kwenye makampuni yetu makubwa ya ndani yanayofanya vizuri, wakuu wa haya makampuni hata kama amesoma tanzania basi huwa wengi wamesoma vyuo ya nje au shule la nje. Huu ni uthibitisho tosha kuwa elimu yetu iko sehemu mbaya sana.
Ni mara Chacha sana kukuta Mtanzania Ameshika nafasi kubwa nchi za wenzetu( na hao wachache huwa wanechanganya elimu ya nje ya Tanzania pia) lakini ni mara nyingi watu wa nje unawakuta kwenye nafasi kubwa katika makampuni ya ndani yanayofanya vizuri.
Kwa sababu hii nakubaliana na Lissu kuwa mfumo wetu wa elimu lazima ubadilishwe, hivyo nitamchagua Lissu mwaka huu!!
3. CCM imetengeneza madaraja makubwa katika raia na kuwafanya wengi wa watanzania kuona kama umaskini ni haki yao.
Katika suala la uchumi, napenda kukiri kuwa CCM haijafanya kazi kubwa katika kuwatengeneza watanzania kiuchumi. Na kuwa fanya watanzania kuwa aggresive kwenye kutengeneza maisha bora kwa ajili yao na vizazi vyao.
Kati ya nchi nilizotembea ni Tanzania tu ambayo nimeona watu wanaridhika kukaa mazingira ya hovyo na hawana namna ya kufanya. Mtu anaridhika kukaa kwenye eneo chafu ambalo halihapimwa na anaona hiyo ndo stahili yake. Leo hii Kuna maneno Kama wakishua, ushuani, uswahilini kwa sababu CCM imetengeneza madaraja na mbaya zaidi kuwafanya wananchi kuridhika na madaraja hayo na kuwa proud kuwa kwenye mfumo huo wa madaraja ya kiuchumi. Watu hadi wamefungwa akili na kufanywa mtu ndoto yake kubwa iwe kununua gari!! Tumekuwa na nchi hadi wahubiri wanahuburi watu kununua magari ndo ionekane kama maendeleo makubwa mtu anaweza kufanya huku akiwa anakaa kwenye eneo chafu ambalo halijapimwa wala kupangiliwa vizuri!!
4. Chadema na Lissu kuja na Sera ya kukuza uchumi kwa kutegemea sekta Binafsi.
Napenda kusema wazi katika tafiti nikizofanya maeneo mbalimbali , sijaona nchi wala taifa lililopiga hatua kubwa kimaendeleo bila sekta binafsi kuchukua sehemu kubwa kwenye uchumi. Na hili ndo lilifanya hata China, nchi tunaowaiga kila siku kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Hapa Tanzania serikali ya Awamu ya Tano tunaona inarudisha nyuma sana sekta binafsi, sasaivi Tunaona kandarasi za ujenzi wakipewa majeshi, shughuli za kufanywa na sekta binafsi zikifanywa na serikali Mf biashara ya kuuza mafuta.
Hili Ni bomu ambalo hatujui ukubwa wake utakuwaje. Duniani pore, sekta binafsi ndo walipa kodi wakubwa, ndo waajiri wakubwa. Hakuna namna vijana wetu wote wataajiliwa serikalini kwa sababu kamwe serikali haijawai na haitowai kuwa na huo uwezo. Hivyo kwa sababu Chadema wamekuja na Sera ya kuendesha Uchumi wa nchi kwa kutegemea sekta binafsi, hivyo nasema wazi, kura yangu mwaka huu nampa Tundu Lissu.
5. Haki ya Mlipa Kodi!!
Baada ya magufuli kuingia madarakani na TRA kuanza kuwabana wafanyabiashara, niliwai kutana na mfanyabiashara ambayo aliniambia, vyovyote vile Tanzania itakuwa nchi ya wachuuzi na sio wafanyabiashara.
Na huu ndo ukweli niliouona. Ndani ya miaka 5 biashara nyingi zimefungwa kutokana na ubabe na uonevu wa Tra. Wengi wameona bora watumie wamachinga na kuwapa bidhaa wakapange barabarani. Hili limefanya taifa kama taifa kukosa kodi kwa kiwango kikubwa. Hii ni kwa sababu mchuuzi halipi kodi. Ila mfanyabiashara Mwenye TIN no na sehemu rasmi ya kufanyia biashara ni lazima atalipa kodi.
Kwenye hili Lissu amesema atakuja na haki ya mlipakodi. Kusema kweli kwa hili lazima nimchague Lissu!!!
Napenda kumaliza kwa kusema, Lissu amenishawishi, na nitampa kura yangu na kumuombea awe raisi wa Tanzania 2020- 2025