Kufanya kosa sii kosa Ila kurudia kosa.Watu wanabaini kichaka Cha uzalendo was kinafiki kwa Kasi ya 6G
 

Kazi mnayo. Buku 7 zitapatikana kweli kwa mtaji huu?
 
Ulikuepo? Na aliyeleta Ndege za maonyesho ni nani?
 
Dar haijafanya uamuzi wa kuwapiga chini Chadema. Nina picha kubwa sana ya Dar . Naona kama Dar ndo sehemu ambayo Lissu ataongoza kwa kura!!! Time will tell.
 
Kama ni mtu sahihi na mwenye maono sahihi kabisa, mwenye kuhitajika kutokana na wakati kuwaongoza Watanzania kwa sasa, basi mtu huyo si mwingine bali ni Tundu Lissu. CCM, chama ajuza kimepitwa na wakati, na kikapumzike kwa amani.
 
Usiishi jana ..hiyo 2015 Lissu wakati wake ulikuwa bado
 
Kwa kweli tangu juzi kawe, jana segerea na Leo Arusha Tundu Lissu ameanza kutema sera kali kweli
Zinahusu maisha ya mwananchi mmojammoja na Taifa kiujumla
Uzuri wa sera zake kuna zile ambazo ziko specific kwa mji husika na kuna zile ambazo zinahusu nchi nzima

1. Lissu kazungumzia ugumu wa maisha ya mfanyakazi na jinsi atakavyoyaboresha kwa kulipa malimbikizo yote wanayodai na kuwalipa nyongeza zao za mishahara za kisheria(annual increments)

2. Amezungumzia uonevu wanaofanyiwa wafanyabiashara wetu na kwamba ataundoa

3. Amezungumzia kuhusu elimu bora na siyo bora elimu, amezungumzia kuhusu elimu ya ujuzi wa kazi siyo ya kukariri

4. Amezungumzia kuhusu viwanda na kuvutia mitaji ili kutoa ajira kwa vijana wetu

5. Amzezungumzia kuhusu diplomasia yetu iliyoshuka na jinsi atakavyorudisha mahusiano bora ya kimataifa

6. Amezungumzia bima ya afya kwelikweli siyo hii ambayo wazee wetu wakishastaafu wanaambiwa waongeze hela ili waweze kuwekwa kwenye bima ya magonjwa nyemelezi ya wazee

7. Amezungumzia kuhusu kuirejesha Arusha kuwa kitovu cha utalii

8. Amezungumzia kuhusu katiba mpya, ameonyesha ubovu wa katiba ya sasa ambayo imelinyima hata bunge uwezo wa kuanzisha hoja ya namna ya kutumia pesa za nchi isipokuwa tu kama hoja hiyo imeanzishwa na serikali.

9.Amezungumza kuhusu haki za watu, ametetea masheikh walio jela kinyume cha sheria, kwa mfano amesema Arusha peke yake kuna Masheikh 70 wako jela achilia mbali wale masheikh wa uamsho.

10. Amezungumzia kuvunjia wananchi nyumba kikatili etc

11. Kszungumzia mzigo mzito wa makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na amesema atashusha makato hayo kwa mwezi kutoka 15% hadi 3% ya mshahara kwa mwezi

12. Amezungumzia kuhusu adha za vitambulisho vya kimagumashi vya wamachinga amesema ataondoa mzingo wa shilingi 20000 ya kitambulisho cha wamachinga pesa iliyoanzishwa na Bashite na Magufuli

13. Amesema ataanzisha sheria ya haki ya mlipa kodi "Bill of taxpayers rights" ili waweze kulindwa kisheria badala ya utaratibu wa sasa ambao wafanyabiashara wanaonewa sana na TRA na hawana pa kukimbilia, kila wanapokimbilia wameshafungwa minyororo

14. Amezungumzia kuhusu uhuru wa habari, kuwa ataondoa sheria kandamizi zilizotungwa na Magufuli kumlinda yeye badala ya kusaidia taaluma kukua

15. Amesema ataomesha matumizi ya hovyo ya pesa za serikali, siyo rais akiamka asubuhi anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake ambapo ndege inatua mara mbili kwa mwaka siku anayoenda kula Christmass na pasaka

16. Lissu anazungumzia kuhusu UHURU, HAKI, MAENDELEO

Kwa kweli Lissu unatisha baba endelea kupiga spana mwana wa Tanzania
 
Dah kanigusa sana.

Hayo mambo yote ndio tunataka.
 
Missile of the Nation tutafutie clip tafadhali!
 
2015 nilimchagua JPM, 2020 nitamchagua tena JPM , ikiwezekana hata 2015 nitafanya hivyo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…