Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
..mimi nataka pawe na ushindani wa wagombea watatu[act,cdm,ccm], au three-way race.

..kura zikigawanyika namna hiyo vyama vya siasa vitaheshimiana na tutapata utawala unaoheshimu haki na demokrasia.
Tatizo CCM,CDM au ACT wataweka vyama vingine vya ziada kupunguza wingi wa kura. Tunatakiwa kwenda kwenye vyama vikuu viwili tu
 
Nisamehe! Tatizo munaweka wagombea wenye IQ ndogo!
Nisamehe tena; Miaka ile ya akina Lissu kusoma sekondari, aliyesoma HGL, HKL, na the likes walikuwa ni watu walioshindwa kuielewa sayansi. Hawakuwa na kisingizio cha kukosa waalimu wazuri kama ilivyo sasa hivi. Hivyo, nikimuona eti ni mwanasheria, aliyesoma masomo ya aina hiyo, najua brain power yake ndogo!! Hawezi fikiria mambo makubwa na ndo maana kila siku utasikia risasi 16! Wauaji anawajua Magufuli! Matibabu yangu... bhla! Bhla!

Bahati mbaya, Jopo lote la uongozi wa juu la CHADEMA lina watu wa aina hii. Ni wale ambao hata ukiwauliza mbolea ni nini, hawana majibu vichwani. Ukiwauliza mbinu gani tuitumie kuondokana na ukame watasema tumeeleza kwenye ilani ya chama, maana hawakumbuki waliandikiwa nini. Watu wa aina hii ndo akina Mkumbo ambaye pia alikuwa huko huko kabla ya kuhama. Midomo na maneno meeengi kama insha za daarasa la 6.
Umeonyesha rangi yako halisi ya utanzania,uvivu.bibi yangu ambaye hakuliona darasa hana hata wasaa wa kuuliza swali.je wewe mvivu ambaye uliuona mwanga kidogo unashindwa pia kupitia ilani ya chama na iko humu.kimsingi Lissu ameshaeleza yote sera yao ya elimu,bima ya afya kwa wananchi wote,kupitia kodi na tozo mbalimbali,soko huru la mazao linalomnufaisha mkulima mkulima hatakopwa.alishaeleza kuhusu utalii,madini.nk.ACHA UFINYU WA MAWAZO MKUU.na leo saa 3 usiku ITV DAKIKA 45 Lissu atakuwa hewani.kaangalie uondoe tongotongo za ujinga unaokusumbua.Badilisha namna yako ya kufikiri.
Hawa wagombea sanasana atakupa muhtasari wa yale mambo muhimu zaidi.usitarajie MAGUFULI akuonyeshe etie Ilani aliiandaa yeye so amemeza kurassa zote .
Pia kusema waliandikiwa ilani ni kuonyesha upeo mdogo wa kufikiri.kila chama cha siasa kina mambo ya msingi kinayoyasimamia,ikiwa ni sera ,imani nk. Na si katka uchaguzi tu.Mara nyingi hizi ilani zinarekebishwa na kufanyiwa maboresho tu kuendana na mda na wakati.
 
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu amesikia vilio vya Wafanyakazi kote nchini.

Katika sheria Kandamizi kwa Wafanyakazi iliyotungwa na Serikali ya CCM na kupitishwa na wingi wa wabunge wa CCM kwa Sasa mtu yeyote anayeacha kazi kabla hahafikisha umri wa kustaafu hatalipwa chochote katika stahili za Mafao yake mpaka atimize miaka 60 hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30

Lissu amesema hiyo Sheria ni ya kipuuzi na kikandamizaji na akasema Mara tu atakapoapishwa baada ya kuchaguliwa ataifuta Mara moja sheria hiyo na kurejesha Fao la Kujitoa.

Wafanyakazi wengi wamefurahishwa na ahadi hii na kusema itakuwa ni ajabu kwa mtu aliyeajiriwa kuacha kumpigia kura Lissu huku akifahamu wazi kuipigia kura CCM na kutafuta umasikini na kifo chake atakapoacha kazi au kufukuzwa kazi kabla ya umri wa kustaafu.
 
Tegemeo la wafanyakazi anajua shida za wafanyakazi huyo? Aliajiliwa ofisi gani.
 
Safi kabisa.
Hizi mbinu ziamie kwa waswahili wetu huku mtaani, humu mtandaoni tumazipa haki inayotakiwa.
 
Naendelea kuamini kweli akili ni nywele kila mtu na zake. Mnamo ona huyu mtu ni mbeba maono endeleeni tu kwani mna nywele zenu bana. Mimi zangu siyo za kuona maono bali naona ni mbeba tope chafu. Japo najua wengi wetu tu ao ona maono ni wale wale wafanyakazi hewa wa mtu yuleee. So mwageni mate na matusi lakini werevu tunaelewa ushabiki wenu ni tope.
Tope umebeba ww kichwani mwako na matakoni mwako..shenzi kbsaaa
 
Nimejaribu kupekua mafaili yote ya wizi na ufisadi ndani ya Nchi hii yaliyojaa kila ofisi lakini sikufanikiwa kuona andiko hata liliofutika linaloeleza kashfa ya Mgombea Urais wa Chadema ambaye pia ni Rais Mtarajiwa wa Tanzania Mh Tundu Lissu.

Huyu mtu ni msafi kama theluji , hajawahi kudokoa , kudhulumu chochote popote , hajawahi kudhulumu nyumba ya Serikali wala ya mtu yeyote , hajawahi kuiba mtumbwi wa mtu, hajawahi kudhulumu boti ya uvuvi pale feri wala hajawahi kuiba Meli yoyote , ni mtu asiye na makandokando yoyote .

Tunaamini kwamba ameletwa na Mungu Mwenyewe kuja kuleta Uhuru kamili ndani ya nchi hii na amekuja kuleta furaha iliyotoweka kwa zaidi ya miaka mitano
FB_IMG_1578677028602.jpg


Ukifuatilia sera yake ya Elimu utagundua kwamba ameletwa maalum kuboresha elimu ya nchi hii ambayo mara zote imeshindwa kumkomboa mwanafunzi
FB_IMG_1577871864627.jpg


Wananchi wote wamemkubali na wameapa kumpa kura zao ili awaondolee dhiki kwa kuleta maendeleo ya kweli ya watu wa nchi hii
FB_IMG_1575390806699.jpg


Njia pekee ya kumdhibiti mtu huyu kutwaa Urais wa Tanzania ilikuwa ile ya risasi 38 iliyofeli baada ya Mungu aliye hai kuikataa , na sasa tunahesabu masiku machache kabla ya Tanzania kujitwalia Uhuru kamili .

Mungu mbariki Tundu Lissu
 
Yaan mnaendelea kujidanganya Lissu kushida, labda twiter na JF,
Hatuwezi mpa inchi kibaraka wa wazungu, ilishindikana kwa Lowasa na mafuliko ije kuwa huyu kibara, jana nimeona kwa macho yangu mkutano wake ,utadhani yupo wilayani kumbe yupo mkoani, mahudhulio tu yanatoa picha
 
Yaan mnaendelea kujidanganya Lissu kushida, labda twiter na JF,
Hatuwezi mpa inchi kibaraka wa wazungu, ilishindikana kwa Lowasa na mafuliko ije kuwa huyu kibara, jana nimeona kwa macho yangu mkutano wake ,utadhani yupo wilayani kumbe yupo mkoani, mahudhulio tu yanatoa picha
Nothing lasts longer , Lissu akidhulumiwa hakutakuwa na mswalie mtume
 
Back
Top Bottom