Bila kujali uvyama Bali uhalisia wa nini mhusika amekua akikitetea,maono na ndoto ya nini hatima ya nchi yetu kiuchumi, kijamii na kisiasa huyu Mheshimiwa ameonyesha umahiri mkubwa kuelezea nini ataifanyia nchi hii.
Hakuna kama Lissu. Aisew Mungu ni mwema ameamua kutufuta machozi
 
Usitujumuishe "watanzania" wewe sio msemaji wetu na wala hatujakutuma, mapenzi yako kwa lissu ni wewe na familia yako (maybe) sisi wengine kura yetu kwa magufuli ebo!
 

Umemaliza yote Mkuu. Watanzania wanayasoma haya na kuyaelewa.
 
Kama mtu hana uwezo wa kutatua matatizo hata akijilazimisha kuyaongea hataweza kuyatimiza
Tundu hajui anataka uraisi ili afanyeje zaidi ya kuhisi akimtoa magufuli atapata sifa
 
Very good ideas zifanyiwe kazi na team ya kampeni ,halafu Kuna yule msrmaji wa mgombea ubunge Jimbo la nyamagana aongezwe kwenye msafara wa Lissu wa kampeni .
 
Rais Museveni wa Uganda amesema aliamua kuwasomesha wataalamu wa ndani maswala ya mafuta baada ya wataalamu wa kizungu kumletea figisu baada ya Russia kugundua mafuta mengi huko kwao.

Museveni amesema kwa sasa Uganda ina wataalamu wabobezi wa mafuta na hawamtegemei mtu yoyote.

Tundu Lissu mgombea urais wa CHADEMA amesema akishinda atawarudisha nchini wataalamu wa gas kutoka Ulaya walioletwa na Kikwete lakini sasa wamekimbilia Msumbiji kutafiti gas huko.

My take; Huyu Tundu Lissu anataka kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kweli Lumumba hata propaganda hamuwezi! Kwa iyo wanaochimba mafuta UGANDA ni waganda????

Siku hizi Total ni kampuni ya Uganda eeeh????😂😂
 
Mseven ana wasomi lakini nani anachimba mafuta uganda, nani anajenga bomba la mafuta!!!!, Suala la nishati hasa gesi na mafuta ni suala mtambuka sio la siasa za majukwaani hasa kwa nchi zetu hizi
Achana na Uganda ajiulize tu Middle east makampuni mangapi yakizingu ndo yanachimba mafuta . Wana technologia na capital pia . Sasa tunawataalam wanamaliza Kwenyw vyuo vyetu wamekariri notes na petroleum engineering unawapa tender vipi? Tuseme wana skills basi , capital unayo? Technology unayo?
 
Rais Museveni wa Uganda amesema aliamua kuwasomesha wataalamu wa ndani maswala ya mafuta baada ya wataalamu wa kizungu kumletea figisu baada ya Russia kugundua mafuta mengi huko kwao...
Tutegemee kuzika matrillioni kwenye mradi wa hovyo wa bomba la mafuta.
 
Tundu Lisu pia amesema Serikali imefilisi mifuko ya jamii kwa mikopo isiyo na mikataba ya kulipa, na mpaka Sasa hawajalipa.

Pia, Lisu akasema mwaka huu Ccm wamechukua Pesa kutoka Psssf na NSSF kwa ajili ya Kampeni. Ndio maana waliopoteza kazi na wastaafu hawalipwi.

Waziri au Serikali waje watoe Taarifa, hizi sio tuhuma ndogo, kupora haki za wanyonge
 
Lissu anasema ataweka bima kwa kila Mtanzania, ni jambo jema. Ila kama hakuna hospitali, hakuna vituo vya afya, zahanati, vifaa vya mahospitalini, ambulance nk. Bima itasaidia nini? Kuna mashine nyingi sana mahospitalini zinahitaji umeme wa uhakika muda wote.

Kama hakuna njia nzuri za Mawasiliano, barabara, reli nk maisha lazima yawe ghali hata iweje, vyakula vingine vinatakiwa kufika kwenye masoko haraka unakuta vinaharibika.

Sijamsikia mbunge hata mmoja wa CHADEMA akipiga kampeni kwa kujisifu kwamba ameimarisha uhuru wa kujieleza jimboni kwake, bali wote wanakimbilia miradi ya serikali wanayopinga bungeni halafu kwenye kampeni wanasema wamefanya wao. Wote wanajisifia barabara, maji, umeme, elimu, afya nk

Maendeleo hayana vyama.
Twende na Magufuli 2025.
 
Magufuli usipoteze muda kwenda kwenye huo mdahalo.

Magufuli tunamjua na misimamo yake tunaijua na faida ya misimamo yake tumeiona

Huyo mzee wa tutashitakiwa MIGA acha apoteze muda na pesa alizohongwa na mabeberu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…