Rafiki yangu na kaka yangu Lissu, watanzania wameumia vya kutosha chini ya utawala wa zaidi ya nusu karne wa ccm na pegnine zaidi, katika utawala wa awamu hii. Wanahitaji Sera mbadala, faraja na ahueni ya maisha ambayo umekuwa ukiinadi vyema, lakini kuna kitu umekuwa ukijisahau katika kampeni zako.
Wakati ukielezea mambo makubwa ya kitaifa, ivute hadhara yako kwa kutaja kero mahususi ndani ya local area yao na toa ahadi ya kushughulika na hizo kero mahususi ndani ya jimbo husika huku ukiwashawishi wamchague mbunge atakaye kusaidia kutatua hizo kero mahususi.
Ongea kama Rais mtarajiwa kwa mambo ya kitaifa kwa ujumla, lakini pia ongea kama mbunge kwa kutaja kero za eneo husika. Hapo jamii itakuelewa na kukuamini kuwa unazijua kwa dhati kero zao na utaweza kuzitatua.
Mfano ulipokuwa Tabora wakati ukihutubia kulikuwa na shouting kutoka kwenye crowd kuhusu vipalata, nashukuru ulisikia na kuliongelea. Juzi bagamoyo wakawa wanashout kuhusu bandari, n.k. Hiyo ni mifano michache tu niliyokupa naomba we we binafsi na timu yako kwa ujumla mlifanyie kazi.
Sent from my TECNO F3 using
JamiiForums mobile app