Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Chaga Development Manifestoes kila mtu anatoa maonyo kana kwamba serikalini wote ni mbumbumbu hawajui kitu nyie tu ndo mnajua.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na sera mbovu za CCM chini ya kiongozi wao Magufuli, Nchi ilikuwa na imo katika hatari ya kugawanyika ki kabila, ki dini na kieneo.

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kutuletea mtu wa kuturejesha tena katika upendo , umoja na kuaminiana.

Tundu Lissu katika muda mfupi tu ameweza katika kampeni zake kuwaleta watu wote pamoja . Utaona watu wa dini zote , makabila na maeneo wamekuwa wakihudhuria mikutano yake wakiwa na furaha na matumaini mazuri kupitia kwake. Kila mahali anapokwenda watu wana shauku ya kumwona na kumsikiliza .

Kwa hali hii , Watanzania tusifanye makosa ya kuitupa bahati hii .

Sote kwa pamoja tumchaguwe hapo October , atuletee amani na upendo na haki nchini.
 
Mgombea wa CHADEMA rais wa mioyo ya watanzania Tundu Lissu amesema atawafuta machozi watanzania waliofukuzwa kazi na Magufuli kutokana na vyeti. Kauli hii aliitoa jana akiwa Kigoma akinadi sera zake.

Lissu amesema watanzania hao hawakustahiki adhabu hiyo kwani wameitumikia nchi kwa moyo mmoja kwa muda mrefu.

Watanzania maelfu waliohudhuria walilipuka kwa shangwe wakiona Lissu ndiyo mkombozi wa kweli.
 
Back
Top Bottom