Kutokana na sera mbovu za CCM chini ya kiongozi wao Magufuli, Nchi ilikuwa na imo katika hatari ya kugawanyika ki kabila, ki dini na kieneo.
Tumshukuru Mwenyezi Mungu kutuletea mtu wa kuturejesha tena katika upendo , umoja na kuaminiana.
Tundu Lissu katika muda mfupi tu ameweza katika kampeni zake kuwaleta watu wote pamoja . Utaona watu wa dini zote , makabila na maeneo wamekuwa wakihudhuria mikutano yake wakiwa na furaha na matumaini mazuri kupitia kwake. Kila mahali anapokwenda watu wana shauku ya kumwona na kumsikiliza .
Kwa hali hii , Watanzania tusifanye makosa ya kuitupa bahati hii .
Sote kwa pamoja tumchaguwe hapo October , atuletee amani na upendo na haki nchini.