Lissu!
Tumesikia kwa miaka 3 iliyopita juu ya mkasa uliokupata. Ni kweli ulipigwa risasi, ni kweli umesoma sheria, nk. lakini sisi wapiga kura tuambie unachotaka kutufanyia kama Watanzania. Yaonekana huna mpango wowote wa elimu, afya, kilimo, sayansi na hata husemi lolote juu ya uchumi. Tuambie mipango yako ni ipi?
Hayo ndo utakuwa mtaji wa kura dhidi ya wapinzani wako akina Membe Rungwe, Magufuli, nk. Kuendelea kusimulia risasi, haituhusu na haina manufaa nasisi huku vijijini. Kama ni kuponyoka kifo, huku tunafiwa kila siku kwa huduma duni. Sema utatusaidiaje???