Tatizo lako ni kwamba umefungwa uelewa na mfumo duni wa kiutawala. Tuache mifano ya Ulaya na America.
Hapo Ghana tu, mfanyabiashara mdogo halipi kodi yoyote wala hauzi vitu vyake vikiwa na VAT.
Na kwa tafsiri ya mfanyabiashara mdogo kwa Ghana, ni mfanyabiashara ambaye mauzo yake hayafikii dola 50,000 kwa mwaka. Huyo halipi kodi yoyote.
Kodi huwa ina malengo mawili. La kwanza ni kwaajili ya huduma za jamii. Pili ni kwaajili ya kuwasaidia watu wa kipato cha chini ili waweze kuinuka. Sasa huwezi ukawa unamwinua mtu wa hali ya chini halafu huyo huyo unamgandamiza kwa kodi. Atanyanyukaje?
Falsafa ya Rais wa Ghana ni kuwa, 'mwache mfanyabiashara mdogo akue, akiwa mkubwa atalipa kodi". Ukianza kumpiga kodi wakati mtaji wake wenyewe ni wa kusuasua, atafia hapo hapo. Na hiyo kodi uliyoichukua toka kwake haitakuwa sustainable.
Shida ya mashabiki wengi wa CCM na Rais Magufuli, ni uelewa mdogo. Mngekuwa mnajibidisha kupata maarifa kabla ya kupwayuka mambo msiyo na uelewa nayo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umefafanua vizuri sana sasa tatizo hawa mboga mboga kuelewa huwa ni shida sana ndiyo maana hata mgombea wao anasimama jukwani anasema kuna mgombea amesema watu wasilipe kodi utadhania. Angepelekewa huu uzi na mataga ausome.