● Mfumo wa kodi zetu utajengwa juu ya Uhuru wa watu wetu, haki za watu wetu na Maendeleo ya watu wetu, kwahiyo mfumo huu utafumuliwa na kujengwa upya ili uwe rafiki kwa walipa kodi.
● Tutapandisha mishahara ya wafanyakazi kila mwaka na kuwalipa mapunjo (arrears) wafanyakazi wote ambao hawakupandishwa mshahara kwa Miaka mitano ya serikali ya hapa kazi tuu.
● Watanzania wote walionufaika na mkopo ya Elimu ya Juu,watarejesha 3%
tu ya deni lao kama mkataba wao na bodi ya mikopo unavyojieleza na siyo 15% kama wanavyokatwa sasa.
● Tutaimarisha sekta ya ujenzi ya ndani na makampuni ujenzi kwa kuzipatia tenda mbali mbali za ujenzi wa miundombinu ya serikali na umma.
● Tutatengeneza mfumo ambao utamwezesha kila mtanzania kuwa na Bima ya afya.Hivyo kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote
● Serikali yetu itabadili falsafa nzima ya elimu, Elimu yetu iwe wezeshi katika kutatua matatizo ya watu wetu, watu wetu waajirike na elimu itakayowafanya wawe na uwezo wa kushindani katika soko la Ajira na na kufundisha vijana stadi za maisha, ili wawese kujiajiri kwa urahisi wakiwezeshwa, siyo Elimu ya Pass mitihani tuliyonayo leo.
● Katiba mpya, tutaunda katiba mpya kuzingatia maoni ya wananchi kupitia tume ya Warioba
●ustawi wa sekta binafsi iwe injini wa uchumi wa nchi.
Hivi ni baadhi ya vipaumbele vya Tundu Lissu Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema.