Kama kwenye mpira wa miguu hii ni dakika ya 40, hivyo mgombea wa Chadema usikate tamaa. Ushindi unaweza kupatikana.
Ukiwa jukwaani mwaga sera za Chadema, kwa umakini bila kupanick na kuhamaki.
Hoja ambazo zinakupa ushindi wa wazi ni kuwaeleza watanzania kwa unagaubaga jinsi JPM alivyoua sekta binafsi huku akitaka watu wajiajiri.
Eleza namna alivyonyima wakandarasi binafsi tender na kulazimisha kujenga kwa kutumia forced account na sasa wakandarasi wengi kampuni zao zimekufa.
Eleza kwa uwazi kama alikuwa anatumia forced account kwa nini Mayanga Contractors ipewe hiyo tender na sio Tanroads kujenga uwanja wa Chato
Eleza jinsi alivyonyima wizara na ofisi za umma pesa za matumizi, sasa hakuna tender za kusupply stationary na vitu vya kiofisi, wajasiliamali wengi wamefirisika.
Eleza jinsi Wachina wanavyopewa kandarasi ambazo hata wazawa wanaweza kuzifanya,sasa mzunguko wa pesa haupo,sababu wakilipwa pesa zinaenda China. Ila wazawa hawapewi hizi kazi wakati wanao huo uwezo kuzifanya.
Anza na haya kwa leo,hii ni dakika ya 45 unaweza kupindua matokeo anytime.