Uchaguzi 2020 Ahadi na Sera za Tundu Lissu katika Uchaguzi Mkuu 2020
Kuna mambo wanasiasa huwa wanasema utafikiri huwa wanaambia mbuzi na sio watu mwanasiasa unawaambia watu kuwa utafuta kodi halafu mwisho wa kuongea hayo unaanzisha kodi nyingine mpya kabisa ya kuchangia kampeni.

Tundu Lissu anaponda serikali ya CCM kwa ukusanyaji kodi mwingi ili tuweze kujenga nchi sababu anaona ni kama unyonyaji, sasa ningependa kumuuliza kama anaamini bila michango ya wanachama wake hawezi kufanya kampeni kwanini anaamin bila kodi za Wananchi anaweza kuijenga nchi?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Hujachangishwa lakini unateseeeka,
 
Hujui tofauti?
Michango ni kwa hiari ya watoaji, Kodi ni kwa shuruti na Kama huna unafilisiwa, nk
 
Naam lissu atashinda Urais 28 oct ! Ngoja tuwape salaam
IMG_20200924_193812_123.jpg
 
Uzi umetulia. Hongera sana mleta mada!

Pia aeleze namna atakavyoondoa ubaguzi kwenye teuzi za utumishi wa serikali.

Teuzi za utawala wa awamu hii zinanuka udini.

Waislamu wanaokerwa na teuzi zilizojaa udini, tarehe 28 october wana Jambo lao!
 
Nashukuru kila unapoenda unaongelea madhila yanayowasibu katika eneo husika.

Ushauri wangu ni huu: Ukishamaliza hayo, toa mhitasari wa ilani ya chama chako.

Kwa mfano
1. Kupunguza makato ya HESLB kutoka 15% hadi 3%

2. Kuongeza mishahara, kupandisha madaraja kwa watumishi

3. Kuondoa kodi za mazao

Na mengine yaliyo kwenye ilani ya chama. Yaorodheshe yote ili uchukue kama dakika tano tu kuyasoma kabla hujafunga mkutano wa kampeni katika eneo husika. Hii itasaidia kwa sababu wananchi wengi hawapati hotuba zako kupitia redio kama ilivyo kwa CCM
 
Huyu Lisu haeleweki.

Anakuwa kama mwanafunzi aliyekaririshwa majibu ya maswali.

Kila mkutano wake wa kampeni utamsikia akisema kuwa ilani yetu ya uchaguzi ni haki,uhuru,na maendwlwo.

Hivi ndio hoja tu mlizo nazo CHADEMA?

Sawa huenda ni mada za iilani.
Kwnini basi msizinyabulishe zaidi kwa kila kituo cha kampeni baada ya kingine,badala ya kurudia yale yale.

Wananchi wanayo mengi ya kuongelewa.
Angalau mngekuwa mnayatafiti kwa kila eneo na kuyaoanisha kwenye vipengele vya ilani zenu.

Vipi kuhusiana na biashara baada ya Corona,mipangilio mizuri ya miji yetu ili iwe sehemu nzuri za kuishi sawa na ilivyo vijijini,vipi kuhusu utunzaji wa mazinguira,mipango miji mizuri,ULIPWAJI MICHANGO KUTOKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KWA MUJIBU WA SHERIA KWA WAFANYAKAZI WASTAAFU KWA WAKATI PINDI WANAPOSTAAFU.

Wafanyabiashara kupeleka makusanyo ya VAT mara walipwapo madai yao na wateja badala ya kudaiwa pindi watoapo ankara za madai kwa wateja wao?

Natamani CCM wangeyaongelea haya katika ilani yao kwani hawa wapinzani ni wakaririshwaji tu.

Natamani kero ziendelee kutatuliwa ili tuendellee kuaminika mbele ya wananchi.

Tusiuache utalii ukadorora TZ.

Makazi mazuri na utunzaji wa mazingira ni kivutio kikubwa cha watalii kuja kupunzika kwetu.

Tuwe na viwanja vya kutosha na vizuri vya michezo kwa kila kitongoji,sio tu mahoteli ya kifahari au mbuga za wanyama.
Viwanja vya mazoezi ni zaidi ya hospitali au vituo vya afya kwani ni maeneo ya kuzuia maradhi badala ya kuingia gharama kubwa za tiba ktk nchi maskini kama yetu.

Pia inakuza akili ya kufikiri na kuchangamanisha jamii,achilia mbali kuepusha muda na gharama za ulevi na uhalifu.
 
Uliyoyaahidi ni mengi Sana sasa najiuliza pesa ya kutekeleza utaitoa wapi wakati vyanzo vya pesa vyote unavitoa kasoro ~umeahidi fidia na kuwarudisha kazini wafanyakazi hewa na vyeti feki wapatao 19k~nyongeza ya mishahara~Katiba mpya~uanzishaji wa majimbo~kulipa fidia waliobomolewa nyumba zao waliojenga maeneo ya wazi na hifadhi za barabara~kuanzisha mfumo mpya wa elimu~kufuta mikopo elimu ya juu~kuwapa chakula wanafunzi 1std+Advance~ NK:,tunataka kujua vyanzo vya mapato kwa sababu utaki wafanyabiashara walipe kodi, utaki sheria zisimamiwe,utaki watu wafanye kazi na kujituma,unataka kuua viwanda vya ndani kwa kuruhu kila bidhaa kuingia na kila mkulima kuuza mazao yake nchi yoyote na hakutokuwa na mageti ya ushuru, hivyo ata mimi nitabeba korosho zangu naenda kuuza Vietnam,ruksa kupitisha meno ya tembo,Mbao,silaha,na kila aina ya uchafu wewe utakuwa rais wa aina gani utatetea katiba ipi?, usemi kama utapambana na wala rushwa,wahujumu uchumi,wauza madawa ya kulevya,maghendo,wezi wa maliasili zetu kama madini,miti,wanyama vitaachwa vifanywe kama kipindi kile ili tu mwanachi awe na pesa mfukoni kweli wewe unataka kuwa rais wa nchi au rais wa chini.
 
Nimemisi Post za Lemutuz sana hivi jamaa yupo kweli ama baada ya RC kuhenguliwa naye akawa ameondoka naye. Mzee wa down town you know Bongo Tambaralee na mabebez you know nyie wa uswekeni huko tulieni. Guys ni ijumaa nipo Five Star Hotel you know

Ila RC Makonda alikuwa anaenda kuibadilisha Dsm iwe kam London
 
Uliyoyaahidi ni mengi Sana sasa najiuliza pesa ya kutekeleza utaitoa wapi wakati vyanzo vya pesa vyote unavitoa kasoro ~umeahidi fidia na kuwarudisha kazini wafanyakazi hewa na vyeti feki wapatao 19k~nyongeza ya mishahara~Katiba mpya~uanzishaji wa majimbo~kulipa fidia waliobomolewa nyumba zao waliojenga maeneo ya wazi na hifadhi za barabara~kuanzisha mfumo mpya wa elimu~kufuta mikopo elimu ya juu~kuwapa chakula wanafunzi 1std+Advance~ NK:,tunataka kujua vyanzo vya mapato kwa sababu utaki wafanyabiashara walipe kodi, utaki sheria zisimamiwe,utaki watu wafanye kazi na kujituma,unataka kuua viwanda vya ndani kwa kuruhu kila bidhaa kuingia na kila mkulima kuuza mazao yake nchi yoyote na hakutokuwa na mageti ya ushuru, hivyo ata mimi nitabeba korosho zangu naenda kuuza Vietnam,ruksa kupitisha meno ya tembo,Mbao,silaha,na kila aina ya uchafu wewe utakuwa rais wa aina gani utatetea katiba ipi?, usemi kama utapambana na wala rushwa,wahujumu uchumi,wauza madawa ya kulevya,maghendo,wezi wa maliasili zetu kama madini,miti,wanyama vitaachwa vifanywe kama kipindi kile ili tu mwanachi awe na pesa mfukoni kweli wewe unataka kuwa rais wa nchi au rais wa chini.
Kwani pesa ya kutengeneza uwanja wa ndege chato mlipata wapi???
 
Huyu Lisu haeleweki.

Anakuwa kama mwanafunzi aliyekaririshwa majibu ya maswali.

Kila mkutano wake wa kampeni utamsikia akisema kuwa ilani yetu ya uchaguzi ni haki,uhuru,na maendwlwo.

Hivi ndio hoja tu mlizo nazo CHADEMA?

Sawa huenda ni mada za iilani.
Kwnini basi msizinyabulishe zaidi kwa kila kituo cha kampeni baada ya kingine,badala ya kurudia yale yale.

Wananchi wanayo mengi ya kuongelewa.
Angalau mngekuwa mnayatafiti kwa kila eneo na kuyaoanisha kwenye vipengele vya ilani zenu.

Vipi kuhusiana na biashara baada ya Corona,mipangilio mizuri ya miji yetu ili iwe sehemu nzuri za kuishi sawa na ilivyo vijijini,vipi kuhusu utunzaji wa mazinguira,mipango miji mizuri,ULIPWAJI MICHANGO KUTOKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KWA MUJIBU WA SHERIA KWA WAFANYAKAZI WASTAAFU KWA WAKATI PINDI WANAPOSTAAFU.

Wafanyabiashara kupeleka makusanyo ya VAT mara walipwapo madai yao na wateja badala ya kudaiwa pindi watoapo ankara za madai kwa wateja wao?

Natamani CCM wangeyaongelea haya katika ilani yao kwani hawa wapinzani ni wakaririshwaji tu.

Natamani kero ziendelee kutatuliwa ili tuendellee kuaminika mbele ya wananchi.

Tusiuache utalii ukadorora TZ.

Makazi mazuri na utunzaji wa mazingira ni kivutio kikubwa cha watalii kuja kupunzika kwetu.

Tuwe na viwanja vya kutosha na vizuri vya michezo kwa kila kitongoji,sio tu mahoteli ya kifahari au mbuga za wanyama.
Viwanja vya mazoezi ni zaidi ya hospitali au vituo vya afya kwani ni maeneo ya kuzuia maradhi badala ya kuingia gharama kubwa za tiba ktk nchi maskini kama yetu.

Pia inakuza akili ya kufikiri na kuchangamanisha jamii,achilia mbali kuepusha muda na gharama za ulevi na uhalifu.
Kama haeleweki Leo Chakubanga alikuwa anajibu nini?
 
Atazitoa wapi wakati yeye ameruhusu wakulima na wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao nje ya nchi bila kukaguliwa na mageti yote amesema atayatoa.
Professor Magufuli promised the opposition will die out by 2020 (and worked so hard to achieve it).

Result? It doubled.

I now understand why he says these large crowds are "fake". You can't spend 5 yrs repressing people's basic freedoms and still expect to win their hearts and minds or else you are so dumb
 
Lissu ni kama vile ameshashinda uchaguzi huu kwa hoja zake 7 ambazo zimepata nguvu na kuaminiwa na jamii. Na hii inajidhihirisha maeñeo mbalimbali ambayo amepita kufanya kampeni.

Lissu ni kama vile mhubiri wa injili, kila eneo analopita shetani anapoteza nguvu na neno linabaki mioyoni mwa watu. Maeneo ambayo bado hajapita ndio yamebaki kuzungumzia habari za CCM, lakini yatakapofikiwa na habari njema ya injili ya wokovu na ubatizo wa maji mengi na wao wataachana na CCM.

Hoja 7 ambazo Lissu zimemwongezea nguvu toka kwa makundi mbalimbali ambazo CCM wamekosa majibu yake

1. Vitambulisho vya wajasiliamali
Ni hoja ambayo imepokelwa vizuri na watamzania, kila kona.CCm wameshindwa kujibu hadi sasa, wamebaki tu kudema dema kwenye majibu yao kwamba magufuri anawapenda wamachinga, Mara vitambulisho sio lazima ,wakati wamevitungia na sheria tayari. Lissu shikilia hapo hapo kwa mpaka waeleze ni lini wamachinga walioomba wauziwe vitambulisho visivyo na picha wala jina

2. Maslahi ya watumishi, nyongeza ya mshahara

Hoja ambayo haijajibiwa hadi Leo, na ccm wamekosa majibu wakaeleweka kwa wananchi. . Nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria na sio takwa la mtu . Alisikika Mara moja akisema hajapandisha mshahara ila edhibiti mfumuko wa bei, na akapata majibu yake toka kwa Lissu kwamba bei ya sukari ya 2015 na Leo 2020 ipo sawa, ? "Wananchi hapana" Lissu " anatuambia nini. Baba shikilia hapo hapo wameshalegea na hawana majibu

3. Suala la pension na kiinua mgongo kwa wastaafu
Watu wengi walikuwa gizani na suala lakini baada ya kulitolea maelezo sasa nalo limepata hamasa miongoni kwa watanzania kwamba kuanzia mwakani wastaafu hawatapata pension zao zote baadala yake watapata nusu. Hilo limeonekana kuwa chuki kwa makundi hayo na CCM wameshindwa kutolea majibu ya kueleweka . Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyooka tayari

4. Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato na hifadhi ya wanyama
Hoja hapa sio ujenzi ,hoja inayoonekana hapa ni namna mradi unavyotekelezwa kwa ufisadi mkubwa wa kupeana tenda na Ndugu yake Mayanga . Mpaka Leo hoja hiyo Magufuli na CCM yake wameshindwa kuitolea majibu, kwa nini aingilie mchakato wa tender na kuagiza apewe ndugu yake na watu sasa huku wanasema ni kama mtu ameamua kupitishia di kwa ndugu yake. Amenipigia pasi kwa mbele ,na suala la hifadhi pia ndio hawana majibu kabisa .Baba Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyong'onyea tayari

5. Suala la ununuzi wa ndege

Hii hoja ilianza kwa kasi mwanzoni kunadiwa na ccm lakini baada ya Lissu kuanza kushughurika Nayo wameshakimbia. Lissu amezungumzia masuala ya Faida na mchakato wa ununuzi wa midege hiyo imegubikwa na ufisadi mkubwa na kwamba anayejua ni Magufuri na mjomba wake Dotto James. CCM mpaka Leo wamepoteana na ajenda ya ndege sio ajenda yao tena kwenye kampeni zao. Lissu wabananishe hapo hapo kwenye kona washindwe pa kutokea.

6: Ukosefu wa Ajira kwa makundi mbalimbali

Eneo hili limepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa makundi mbali mbali ya vijana. Tangu 2015 ajira zimetolewa kwa walimu wa sayansi na kada za afya. Kada nyingine hazijaguswa kabisa . Hoja yake hapa magufuri imebaki kuwa ni watu wajiajiri wakati yeye mtoto wake Jesca amemwajiri wizara ya mambo ya nje, mwingine amempa RAS iringa .hao walishindwa kujiajiri hadi awaajiri. Watoto wa wanyonge ndio wanaohimizwa kujiajiri. Hapo napo Lissu shikilia hapo hapo pana tija na kundi kubwa la wahanga

7: Waathirika wa vyeti feki
Hii ni hoja ambayo imepata kusemwa na Lissu, kwamba hao walio wa ajiri ni wao ccm na kinachozungumzwa hapa ni watu kufukuzwa kama mbwa bila kupewa mafao yao, ambayo wamechangia kwa miaka mingi halijulikani lilipo enda. Hao ni watanzania wenzetu na sio wakenya wala wamalawi, wamelitumikia na kutufundishia watoto wetu kwa miaka mingi hadi wengine wamekuwa maprofesa. Michango yao ipo wapi kama hawajapewa, Magufuri na ccm yao iliyojaa roho ya kuumiza watu waseme wamepeleka michango yao ya pension waliyokuwa wanachangia kwenye mifuko ya hifadhi

8: Magufuli amesambaza wasiojulikana kila kona

Hii inasababisha watu ukiikosoa tu serikali unakamatwa soon. Wasio julikana inafanya watu tunashindwa kunya wala kukojoa usiku

Nashauri Lissu sasa kwa kuwa kwenye miji yote na vijijini amefanikiwa kuiteka sasa ajikite katika kuwaaminisha watanzania ni namna gani walinde kula zao. CCM wamebaki na mbinu moja tu ya kuwategemea wakurugenzi na NEC, ili wawavushe hapo walipo kwenye tope kwenda nchi kavu. Katika hotuba zake sasa ajikite kuwahimiza wananchi kulinda kura zao, hii ngoma imeshaisha . Wakurugenzi na hawa watendaji kata ambao wamepewa maelekezo marafuku kuwatangaza wapinzani kwenye maeneo yao ndio imekuwa mwiba na Wapinzani wasipo jipanga vizuri mwishoni wataumizwa na hao watu.

Ushauri wangu Lissu sasa ajikite katika kulinda kura. Watendaji wa kata si wa kuchekewa na kuendelea kuachwa kwani kwanza ni watu wa chini mno, lakini ni watu ambao wameshapokea vitisho, hivyo inabidi kazi ya ziada ifanyike. Umati kwa umati Huo Huo wanaojaa kwenye mikutano yao wahimizwe pia wawepo hivyohivyo kwenye kulinda kulinda kura zao kwenye vituo vya kata na ofisi za wakurugenzi. Kwa umati ule wa mwanza wakifanikiwa kukaa kwenye kata na ofisi za wakurugenzi kazi itakuwa imeisha.

Kama una hoja nyingine ambayo unaona bado Lissu bado hajaizungumzia ambayo inaweza kuteka mioyo ya watu iweke hapa ,lakini pia unaweza kupendekeza mbinu sahihi ya kulinda kura

Chaaaaao, tuonane 28 oktoba
 
Back
Top Bottom